Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

View attachment 1543623
Mgombea Urais wa Chadema katika uchaguzi mkuu ujao mwishoni mwa mwaka huu, ametoa madai mazito mjini Njombe jana katika ziara zake za kutafuta wadhamini, akimuhususisha Rais, kuhusu jaribio la kuuawa kwake, lililofanyika September 7 mwaka 2017.

Akihutubia umati wa wananchi, alikumbushia historia ya tukio lake la kumiminiwa risasi, ambapo aliponea chupuchupu kuuawa na kukimbizwa nchi za nje kwa matibabu.

Akisimulia mkasa huo alieleza kuwa kuna "connection" kati ya hotuba aliyoitoa Rais Magufuli, ya uzinduzi wa ripoti ya tume ya madini, masaa takribani mawili, kabla ya kupigwa kwake risasi, aliyotoa akiwa Ikulu, jijini Dar-es-Salaam.

Aliendelea kueleza kuwa katika hotuba hiyo aliyotoa Rais Magufuli, ambayo alidai ipo ndani ya YouTube, alimnukuu Rais akiyatamka maneno yafuatayo "Katika mapambano ya kijeshi, huwa wana kawaida ya kumwua, askari yeyote ambaye anawasiliti katika mapambano yao, vile vile katika vita ya kiuchumi ambayo nchi yetu inapigana hivi sasa, hatuwezi kuruhusu ku-survive kwa mtu mmoja, ambaye imebainika amekuwa akiwasiliana mwanasheria wa kampuni hiyo ya madini, Deo Mwanyika, ili kumwibia taarifa mbalimbali nyeti, katika lengo lao wakishirikana na mabeberu kutoka nje ya nchi, katika kutuhujumu malipo yetu ya madini, hastahili kabisa ku-survive" mwisho wa kunukuu.

Tunajua kuwa katika tukio hilo la kupigwa kwake risasi mwaka 2017, Tundu Lissu, Jeshi la Polisi limekuwa likutaaminisha kuwa uchunguzi wa tukio hilo unakwamishwa na Tundu Lissu, muhanga mkubwa wa tukio hilo, pamoja na Dereva wake, ambao wote walikuwa wameenda nchi za nje kwa matibabu.

Hivi sasa Tundu Lissu amesharudi nchini na amewapa "hints" ya kilichompata siku ile ya kutisha sana, ambapo "watu wasiojulikana" walimpiga risasi mfululizo 16 mwlini mwake katika jaribio la kutaka kumwua na ameeleza mwenyewe nini kilimtokea siku ile, ambapo Jeshi letu la Polisi, limekuwa likidai kuwa limekwamishwa kuendelea na uchunguzi wake, kutokana na kukosekana ushahidi huo wa Tundu Lissu

Kwa hiyo nadhani Jeshi la Polisi lingeanza kufanyia uchunguzi wa tukio lile sasa, kwa "hints" alizozitoa yeye mwenyewe muathirika wa tukio lile Tundu Lissu.
msaliti hatakiwi kusurvive hata kidogo
 
Ukiunganisha "dots" hapo unapata jawabu

Mbunge ananyimwa haki yake ya kutibiwa ambayo ni haki yake kisheria.

Mbunge ananyimwa mshahara wake pasipo sababu za msingi.

Hatimaye mbunge anavuliwa kabisa ubunge wake kwa madai kuwa Bunge hilo halijui alipo Mbunge huyo, wakati dunia nzima inajua kuwa mbunge huyo anatibiwa nje ya nchi, baada ya kumimiwa risasi mfululizo!

Hili tukio ndilo linafunga kazi na kum - discredit kabisa Magufuli na serikali yake....

Hii moja kwa moja linamweka kwenye uhusika Rais Magufuli, hawezi kukwepa wala kujificha....
 
Deo kapewa nafasi ya Ubunge kama pole kwake kwa kukaa gelezani kwa miaka 3 na ushee !!

Sasa kampeni zikianza atuambie watanzania hayo makosa yote 90 na ushee yameishaje ishaje?
 
Sasa kwanini baada ya kuona Magufuli amekuwa serious kuhusu madini badala ya kuungana nae yeye akageuka snitch?
Mkuu nasisitiza kuwa Magufuli ndio snitch namba moja.

Lissu aliweka wazi kuwa sisi hatuibiwi madini, tunaibiwa kwenye mikataba hivyo kama tunataka kukomesha huu wizi turekebishe mikataba yetu upya.

Kitendo cha kukamata haya makinikia na kuyazuia itafanya tushtakiwe na kulipa gharama kubwa, kitu ambacho ni kweli ulitumika ubabe tukaambiwa tunawadai zaidi ya trilion 450 za kodi, ila mwisho wake leo wote mashahidi hakuna tunachodai, nchi imeshtakiwa, makinikia yameondoka na jamaa wataendelea kuchimba tofauti na tulivyo aminishwa na Meko.

Bungeni pakapelekwa mikataba kwa hati ya dharura kurekebishwa kuwa kuanzia sasa (hii haihusishi migodi iliyoingiwa mikataba huko nyuma) tutanufaika 50/50. Ila ukweli ni kwamba hatuna maeneo mapya yaliyopo, yote yalishaingiwa mikataba mibovu huko nyuma.

Sasa huyu Lissu anaye waeleza ukweli ndio mnataka kumnyamazisha kwa risasi ili muendelee kuiba. Meko angepiga risasi wale maprofesa waliomdanganya kuwa eti makontena yanaondoka na tani za dhahabu.

Meko akasema tutachenjulia hapa hapa, ni nani ajenge smelter kwa hivi vimakinikia vilivyopo hapa nchini? Mnaijua smelter nyie? Wajuzi walisema hilo halitawezekana labda tungekuwa na nchi zingine zinazoleta makinikia hapa kuchenjua ili tuwe na load ya kutosha.

Sasa mtu anayekushauri hivi unawezaje kumuita msaliti ndugu?

Me nadhani Rais angemuita atoe mapendekezo ya nini kifanyike badala ya kumuita msaliti.
 
Kwenye vitabu hivyo hivyo vitakatifu, tunaambiwa Shetani alikuwa malaika mwenye cheo kikubwa. Inasemekana shetani bado anadunda humu duniani. Someni vitabu hivi vitakatifu vyote na kwa ufasaha! Je. Unakubali shetani anarandaranda duniani ama la?
Achana na shetani, justify adhabu ya Lissu. Kwa mujibu wa maandiko shetani alitolewa mbinguni na adhabu yake ilikuwa ni kutupwa kuzimu hivyo ilitimia adhabu yake haikuwa kuuawa.

Je kwa Lissu nayo ilikuwa kumpiga tu risasi nyingi kisha apone na kuendelea na mishe zake.
 
Ile video haikuendelea lakini pale mwanzo lisu wakati ananza kuongea lisu alisema turudi kwenye hotuba ya rais 'rais anasema Na Yule mpiga kelele ashughulikiwe ambaye ni mh Lissu mpigania madini nchi hii.

Hapa dhairi kabisa rais aliona lisu anaharibu maslai yake

Mkataba serikali iliyoingia ubia mpya na hawa waliokuwa wa makanikia unaenda kunufaisha Watanzania wote.

Lissu asiwe mjinga amekubali alikuwa anawasiliana na Mwanyika. Anajua Mwanyika baadaya kugeuka kuwa mzalendo na kutoa ushirikiano kasema mangapi kuhusu Lissu na mabeberu? Kwa nini ashangae Mwanyika kuwa mgombea kupitia ccm.

Kwa nini hazungumzii yule Doctor ambaye JPM alisema Lissu alikuwa akimsumbua kutafuta apate taarifa za kamati ya makanikia. Alizitaka za nini wakati anajua tume iko na inashughulikia suala hilo?. Tukisema alizitaka ili akawauzie hao wabia wake mabeberu tutakosea? Alishanogewa na fedha za kukodisha cdm kwa EL akataka kuchonga mzinga kupitia Acassia.

Kwa nini Lissu hakutumia fursa hii ya JPM kuunda tume ya kushughulikia mikataba mibovu mibofu kutoa ushirikiano kwa tume? Kinyume chake Lissu akageuka kuwa mhujumu namba moja wa juhudi na kazi za tume hii. Na kilicho mfanya ageuke ni wazi kuwa umaarufu utaenda kwa CCM, serikali yake na JPM. Kingine ni kuwa alikuwa na maslahi binafsi kwa watu wa makanikia. Akiwaomba awe mwabasheria wao.

Fikiri, jaribu kufikri, ndio fikiri, fiiikiri, fikiri, hapa ni kwa sauti ya Lissu. Mtu wa aina hii anayeweza kugeuka taifa zima kwenye vita vya uchumi anastahili.? Eti, eti eti! Leo bila aibu anarudi kutafuta huruma kwa Watanzania.
 
......Je kwa Lissu nayo ilikuwa kumpiga tu risasi nyingi kisha apone na kuendelea na mishe zake.?
Swali lako tamu sana. Hongera kwa kufuatilia maadiko matakatifu. Yaani swali lako nimelipenda hasa. Nina imani swali hili limefunua vitu ambavyo wengi hatukuvitarajia. Nimefurahishwa sana na swali lako.
 
View attachment 1543623
Mgombea Urais wa Chadema katika uchaguzi mkuu ujao mwishoni mwa mwaka huu, ametoa madai mazito mjini Njombe jana katika ziara zake za kutafuta wadhamini, akimuhususisha Rais, kuhusu jaribio la kuuawa kwake, lililofanyika September 7 mwaka 2017.

Akihutubia umati wa wananchi, alikumbushia historia ya tukio lake la kumiminiwa risasi, ambapo aliponea chupuchupu kuuawa na kukimbizwa nchi za nje kwa matibabu.

Akisimulia mkasa huo alieleza kuwa kuna "connection" kati ya hotuba aliyoitoa Rais Magufuli, ya uzinduzi wa ripoti ya tume ya madini, masaa takribani mawili, kabla ya kupigwa kwake risasi, aliyotoa akiwa Ikulu, jijini Dar-es-Salaam.

Aliendelea kueleza kuwa katika hotuba hiyo aliyotoa Rais Magufuli, ambayo alidai ipo ndani ya YouTube, alimnukuu Rais akiyatamka maneno yafuatayo "Katika mapambano ya kijeshi, huwa wana kawaida ya kumwua, askari yeyote ambaye anawasiliti katika mapambano yao, vile vile katika vita ya kiuchumi ambayo nchi yetu inapigana hivi sasa, hatuwezi kuruhusu ku-survive kwa mtu mmoja, ambaye imebainika amekuwa akiwasiliana mwanasheria wa kampuni hiyo ya madini, Deo Mwanyika, ili kumwibia taarifa mbalimbali nyeti, katika lengo lao wakishirikana na mabeberu kutoka nje ya nchi, katika kutuhujumu malipo yetu ya madini, hastahili kabisa ku-survive" mwisho wa kunukuu.

Tunajua kuwa katika tukio hilo la kupigwa kwake risasi mwaka 2017, Tundu Lissu, Jeshi la Polisi limekuwa likutaaminisha kuwa uchunguzi wa tukio hilo unakwamishwa na Tundu Lissu, muhanga mkubwa wa tukio hilo, pamoja na Dereva wake, ambao wote walikuwa wameenda nchi za nje kwa matibabu.

Hivi sasa Tundu Lissu amesharudi nchini na amewapa "hints" ya kilichompata siku ile ya kutisha sana, ambapo "watu wasiojulikana" walimpiga risasi mfululizo 16 mwlini mwake katika jaribio la kutaka kumwua na ameeleza mwenyewe nini kilimtokea siku ile, ambapo Jeshi letu la Polisi, limekuwa likidai kuwa limekwamishwa kuendelea na uchunguzi wake, kutokana na kukosekana ushahidi huo wa Tundu Lissu

Kwa hiyo nadhani Jeshi la Polisi lingeanza kufanyia uchunguzi wa tukio lile sasa, kwa "hints" alizozitoa yeye mwenyewe muathirika wa tukio lile Tundu Lissu.
Kwahiyo T. Lisu amekiri hadharani kuwa yeye ndio msaliti wa nchi hii? Au nimeelewa vibaya.

MAGUFULI4LIFE.
 
Nadhani najadili hili na mtoto mdogo au MTU mzima asiye jielewa.
Mungu anaadhibu wakosaji lakini haadhibu kwa usiri kutumia watu wasiojulikana.
Anaogopa nini mpaka afanye kwa usiri mkubwa? Ukitaka kumhusisha Mungu jambo lolote kaa chini utafakari kwanza ukuu wake na sio kuropoka tuu

Jiongeze kujua ukweli Kaleb naYoshua walikuwa spies katika kazi za Mungu. Kanisa Katoliki linasifika duniani kote kwa wale mashushu wake mahiri. Mungu aliwaficha Sodoma na Gomora kuhusu kuangamizwa kwao. Tena akasema nimeshuka kuhakiki /jiridhisha kuhusu taarifa nilizozisikia/kupata za Sodoma na Gomora, kazisikia/pata kupitia wapi? Probably agents wake. Mungu anafanya mambo sawasawa na utashi wake. Lissu angekuwa na busara sanasana angalitakiwa kutafuta kutengeneza kwanza Mungu wake, wafuasi wa cdm na mwisho Watanzania wenzake.

Maana maneno aliyoambiwa Yuda na Yesu, kuwa huyu ninayechovya naye katika kikombe kimoja ndiye atakaye ni saliti. Ndicho kinachoendelea kwa Lissu. Huyu mnayefikiri ni mtetezi wenu Watanzania, ndiye alitaka kuwa msaliti wenu katika makanikia.

Hivyo Watanznia huyu mnayefikiria ni mtetezi wa haki zenu, Lissu, Lissu ndiye aliyetaka kuwasaliti katika makanikia, ndiye ambaye ni mdau mkubwa hapo cdm akijaribu kuwaaminisha mambo ambayo hata yeye haya amini na ndio maana chama ambacho watu wengi walikipambania mwaka 2015 wakamua kumkodishia mtu kwa maslahi ya genge lao la watu flani. Bila, biiila, bila hatakushirikisha wanachama wenzao. Walikaa wakaamua walichoamua mara ikatoka ile kauli mbiu ya wakati ule, 'Tumebadili gia angani'.
 
Sasa kwani Magufuli alikuwa anatakaje?

Si alikuwa anataka huo wizi wa kwe ye mikataba ndio urekebishwe ikiwemo kuzuia makinikia.?
Mkuu tuelewane vizuri, naamini hakuna mtu (hata awe mpinzani wa Magu) atakataa kuwa tukidhibiti wizi wa rasilimali zetu (ikiwemo madini) wote tutanufaika.

Na alipoanza hiyo move hata wapinzani walionesha kumsapoti na ndio maana wakajitokeza kutoa maoni (Lissu na Zitto wakiwemo) kuhusu namna nzuri ya kulinda, kudai na kutetea rasilimali zetu.

Kinyume chake akawageuka na kujibinafsishia ule mchakato (sijui kwa nia njema au mbaya) na kuanza kuwaita wengine wasaliti. Ilibidi watu waanze kuhoji kama ana nia njema kwa nini hataki ushauri wa wengine kisa tu ni wapinzani wake kisiasa?

Akaanza kupiga vijembe kwenye press na mikutano yake na kuwaita wengine vibaraka wa mabeberu, ndipo nao wakatoka mbele ya umma kueleza kuwa anachokifanya kitaligharimu taifa na hatutafanikiwa badala yake tutaingia hasara zaidi.

Ndipo hapo issue ya kina Lissu kuomba taarifa Barrick ili wauoneshe umma kile kilichoingiwa kwenye mikataba kati ya serikali na Barrick ili waujue ukweli.

Kinyume chake Magu akatoka tena kusema hawa anaowaita wasaliti wanapeleka siri za nchi kwa Barrick. Sasa unajiuliza ni siri ipi inayozungumzwa wakati ni vitu vilivyo kwenye mikataba?

Miaka mitatu leo, kuna mtu anaweza bisha kuhusu ushauri aliotoa Lissu?
Kwamba hakuna tutakacholipwa, makinikia yataondoka bure, tutashitakiwa na tutaliingiza taifa kwenye mgogoro na wawekezaji?

Hadi leo migodi imesitisha uzalishaji, watu wamepoteza ajira, serikali inakosa mapato (hata yale kiduchu), wawekezaji wanaiogopa Tz, taswira yetu kimataifa imeharibika.

Na kibaya watu wanaangalia tu migodi ya Barrick, mkuu kuna mgodi wa Shanta mining mkubwa pale Ikungi kwenye jimbo la Lissu hadi leo jamaa hawajaufungua kutokana na sera za awamu hii. Jamaa wameuweka under maintainance hadi watakapo jiridhisha ni safe kwao wataweka pesa zao waanze kuzalisha. Tunakosa mapato, ajira na mzunguko wa fedha kwa sababu za hovyo kisa ubabe wa mtu mmoja asiyetaka kushauriwa.
 
Tunataka sera atasaidiaje wakulima, machinga, wasomi, ,viwanda,uchumi,siasa ,elimu ,aachane na mambo ya risasi
hebu tumieni akili hata kidogo, Sera lazima ziendane na usalama Wa raia, kama mgombea Wa sisiem moja ya Sera zake ni ' shooting from the hip' wapiga kura tujue !
 
Jiongeze kujua ukweli Kaleb naYoshua walikuwa spies katika kazi za Mungu. Kanisa Katoliki linasifika duniani kote kwa wale mashushu wake mahiri. Mungu aliwaficha Sodoma na Gomora kuhusu kuangamizwa kwao. Tena akasema nimeshuka kuhakiki /jiridhisha kuhusu taarifa nilizozisikia/kupata za Sodoma na Gomora, kazisikia/pata kupitia wapi? Probably agents wake. Mungu anafanya mambo sawasawa na utashi wake. Lissu angekuwa na busara sanasana angalitakiwa kutafuta kutengeneza kwabza Mungu wake, wafuasi wa cdm na mwisho Watanzania wenzake.

Maana maneno aliyoambiwa Yuda na Yesu, kuwa huyu ninayechovya naye katika kikombe kimoja ndiye atakaye ni saliti

Hivyo Watanznia huyu mnayefikiria ni mtetezi wa haki zenu, Lissu, Lissu ndiye aliyetaka kuwasaliti katika makanikia, ndiye ambaye ni mdau mkubwa hapo cdm akijaribu kuwaaminishRa mambo ambayo hata yeye haya amini na ndio maana chama ambacho watu wengi walikipambania mwaka 2015 wakamua kumkodishia mtu kwa maslahi ya genge lao la watu flani. Bila, biiila, bila hatakushirikisha wanachama wenzao. Walikaa wakaamua walichoamua mara ikatoka ile kauli mbiu ya wakati ule, 'Tumebadili gia angani'.
Rubbish, kama huna hoja yoyote sio lazima kuandika
 
Mkuu tuelewane vizuri, naamini hakuna mtu (hata awe mpinzani wa Magu) atakataa kuwa tukidhibiti wizi wa rasilimali zetu (ikiwemo madini) wote tutanufaika.

Na alipoanza hiyo move hata wapinzani walionesha kumsapoti na ndio maana wakajitokeza kutoa maoni (Lissu na Zitto wakiwemo) kuhusu namna nzuri ya kulinda, kudai na kutetea rasilimali zetu.

Kinyume chake akawageuka na kujibinafsishia ule mchakato (sijui kwa nia njema au mbaya) na kuanza kuwaita wengine wasaliti. Ilibidi watu waanze kuhoji kama ana nia njema kwa nini hataki ushauri wa wengine kisa tu ni wapinzani wake kisiasa?

Akaanza kupiga vijembe kwenye press na mikutano yake na kuwaita wengine vibaraka wa mabeberu, ndipo nao wakatoka mbele ya umma kueleza kuwa anachokifanya kitaligharimu taifa na hatutafanikiwa badala yake tutaingia hasara zaidi.

Ndipo hapo issue ya kina Lissu kuomba taarifa Barrick ili wauoneshe umma kile kilichoingiwa kwenye mikataba kati ya serikali na Barrick ili waujue ukweli.

Kinyume chake Magu akatoka tena kusema hawa anaowaita wasaliti wanapeleka siri za nchi kwa Barrick. Sasa unajiuliza ni siri ipi inayozungumzwa wakati ni vitu vilivyo kwenye mikataba?

Miaka mitatu leo, kuna mtu anaweza bisha kuhusu ushauri aliotoa Lissu?
Kwamba hakuna tutakacholipwa, makinikia yataondoka bure, tutashitakiwa na tutaliingiza taifa kwenye mgogoro na wawekezaji?

Hadi leo migodi imesitisha uzalishaji, watu wamepoteza ajira, serikali inakosa mapato (hata yale kiduchu), wawekezaji wanaiogopa Tz, taswira yetu kimataifa imeharibika.

Na kibaya watu wanaangalia tu migodi ya Barrick, mkuu kuna mgodi wa Shanta mining mkubwa pale Ikungi kwenye jimbo la Lissu hadi leo jamaa hawajaufungua kutokana na sera za awamu hii. Jamaa wameuweka under maintainance hadi watakapo jiridhisha ni safe kwao wataweka pesa zao waanze kuzalisha. Tunakosa mapato, ajira na mzunguko wa fedha kwa sababu za hovyo kisa ubabe wa mtu mmoja asiyetaka kushauriwa.

Mtasema yote matapeli wakubwa nyie wa Watanzania. Kwa hiyo wao Lissu na Zitto walitaka wajipatie maslahi binafsi ikiwemo political mailage sio?! Na umesema vizuri na kuweka wazi kuwa wanajua kuna maslahi wanayapata katika mambo hayo. Wakafikiri wenzao watafaidi kama wao walivyokuwa wanafaidi hivyo pengine huko nyuma. Jawabu kwao likawa ni kuhujumu mchakato mzima sio. Hawa ndio baadhi ya viongozi wetu. Kazi ipo.
 
Mabeberu ndio waliong'oa CCtv camera na kuondoa walinzi eneo la tukio?
Ninyi kutwa kuchwa si mnasema hao jamaa hawashindwi kitu? Mbona sana kama unadharau uwezo wa 'mabeberu! ?
Ha ha haaa! Hamfurukuti ...this time. Ha ha haaa!
 
Back
Top Bottom