Mkuu Ndo maana Nimekusisitiza sana kusoma "Journal" mbalimbali za Kitaifa na za Kimataifa Sanasana jikite kwenye Journal za Reseaerch pamoja na Statistics Kadhaa utagundua kinachosemwa kwenye siasa hakina UHALISIA zaidi ya kuwapa moyo wananchi ila kwakuwa kaka yako nipo ni jukumu langu kufanya facts check mbalimbali kwako ili nikujengee uwezo wa kupambanua vitu...
Wamasai wanamiliki 'Ngombe wengi huko Kenya alafu hao wamasai ndiyo wenye mifugo mingi kwenye Taifa lenye n'gombe wengi hapa Afrika mashariki na kati wakiwa Tanzania. Hivi hizi ni akili kweli?
FACTS CHECKS....
Nakubaliana na Wewe kabisa kwamba Tanzania Ni Nchi yenye Ng'ombe zaidi Katika East Africa na inakadiriwa kufikia mpaka Milion 33 na pia kwa makadirio kama 24.5 mbuzi na kondoo kama 8milion ikifuatiwa na kenya ambayo yenyewe inakadiriwa kufikia 27miliion ya Ng'ombe....
Sources ya data kutoka (statistics Africa pamoja na nbs) pia unaweza kusoma jarida la LIVESTOCK SECTOR TRANSFORMATION PLAN (LSTP) 2022/23 - 2026/27....lililotolewa na MINISTRY OF LIVESTOCK AND FISHERIES
Sasa mimi Sikuzungumzia Mifugo yote Tanzania Mainland Mkuu naona umenichangany Nilizungumzia mifugo iliyoko Ngorongoro ambayo ni only 1.5% ya mifugo yote iliyopo Tanzania bara ambayo kwa hesabu ya haraka ni kama laki tano hivi...
Differ from Tanzania (ambapo tuna makabila Zaidi ya 120 na makabila ya wafugaji Yanafika makabila zaidi ya 50) na only makabila machache sana sio wafugaji...
kenya wana makabila machache zaidi ya wafugaji na la kwanza likiwa ni kabila la wamasai...
mbali na kuwa wafugaji naendelea kusisitiza kuwa kwa mujibu wa sensa ya kenya bado wamasai wamekuwa ni kabila linalokuwa zaid huko kwao na bado hawahamishwi kwenye Hizo mbuga...
nakupa kidogo statistics ya makabila kwao....
(Wamasai 23 % ,Waluhya 14%,Wajaluo 13%,Wakikuyu 12%,Wakalenjin 12%,Wakamba 11%,Wasomali 8%,Wakisii 6%,Wameru (Meru) 6%,Waturkana 10% e.t.c)
sasa nafikiri kwa hoja hiyo nimeweka wazi na nimeionyesha....
Mtu anasema eti mbona hifadhi za Kenya awaondolewi? Hivi wanachofanya Kenya ni lazma nasi tufanye hivyo? Hizo Mbuga za Kenya zinayo hadhi kama ya Ngorongoro au na ili mpaka turudi darasani?
Yeah sina maana kwamba tuanze kufikiria kama wanafikiria wakenya au tufanye kama wanavyofanya wakenya ila nna maana ifuatayo kama Hilo swala lilikuwa lina Faida sana kufanya hivyo nafikiri kenya wangeanza kulifanya kwani wao wana Idadi kubwa ya Wamasai kuliko hata idadi tulionayo sisi....
kenya hawana mbuga zenye hadhi ya ngorongoro...
Hivi wewe ndo unasema au mtoto kachezea simu kaandika ulichoandika
Natamani Nikwambie Urudi darasani lakini Hapana wewe ni Mtu mzima mwenzangu Pale unapokosea tunarekebishana tu....
ngoja nikupe report ndogo ya Hifadhi za Taifa za Africa zenye Ubora wa kuwa mbuga bora na maeneo makubwa zaidi ....
kwa Africa inayoshika namba moja mpaka sasa Bado ni serengeti inaukubwa wa eneo la Kilometa za mraba 14,750 ikifuatiwa na Hifadhi ya kruger ya afrika kusini yenye ukubwa wa mraba kilometa 19,485 ikifuatiwa na chobe ya botswana ambayo ina ukubwa wa km za mraba 11700 halafu inafuatiwa na Masai Mara ya kenya Yenye kilomita za mraba 1510 cha ajabu mpaka utafika namba kumi bado hakuna tena Mbuga au hifadhi yoyote ya Africa mashariki.....
Na tunapozungumzia Ubora wa Mbuga au hifadhi hatuzungumzii Ukubwa wa eneo tunazungumzia idadi ya wanyama,Aina ya wanyama sanasana upatikanaji wa Big5,Wonders na baadhi ya Family Au upatikanaji wa species za wanyama mbalimbali....
na ndo maana utaona hapo Yenye ukubwa zaidi ni kruger ila haikuwHi kushika namba moja Africa...
Sasa Kwa Ubora wa Mbuga Ngorongoro haifiki hata kidogo kwa Masai mara ya Kenya....
ambapo sasa Ngorongoro eneo walilopo wanyama ni eneo dogo Tu ambalo ni eneo la crater au Eden ila eneo zima la Ngorongoro ukijumlisha Ngorongoro Crater ukiniuliza kwa ukubwa ni 8292 kilometa za mraba...
Nafikiri umenieleza And thats Why haiitwi Natinal Park inaitwa Ngorongoro Conservation Area...
Ni hasara hipi nchi inapata kuwaondoa watu hao wanao leta madhara kwenye hifadhi ya Ngorongoro?
Mkuu samahani kidogo.kwa hili swali inabidi nikufanyie "sarcastic" kidgo Una miaka Mingapi?????
maana Kama ni mtu mzima ulichoandika kinaenda kinyume na umri wako kama ni Mtoto jitahidi upitie historia za wakubwa waliokutangulia utajifunza mengi...
Mkuu kwanza unajua Maana Ya Ngorongoro Kutoitwa National Park na ikaitwa Conservation Area "ok then nafurahi kukupa Elimu hiyo"
NGOJA NIKUCHAPE SHULE....
Kwanza Ngorongoro Conservation Area ilikuwa established Mwaka 1959 ikiwa ni Jitihada za serikali Kutambua mchango wa Watu wenye Asili ya kutoka mwambao wa mto nile ( Au unaweza waita nilotic people) au kwa sasa wanafahamika kama Wamasai.....
Story Iko hivi Maa-speaking people au maasai walikuwa wakitoka kutoka huko Mwambao wa mto nile wakipits sudani,Ethiopia na nchi zingine kuja Afrika ya Mashariki ili kutafuta Makazi na malisho ya Mifugo yao Mnamo miaka ya 1800s Kwa bahati nzuri walifika sehemu za huko Kaskazini mwa Tanzania ndo wakavumbua Ngorongoro....
japo walipigana ili kuwaondoa watu wa kabila la mbulu ambao wao walikuwa wakulima katika eneo hilo...Wamasai wamekuwa wahifadhi wa eneo hilo Tangi miaka hiyo kwa miaka takribani 250 sasa.....
Sasa Masai wamekuwa ni kivutio katika Ngorongoro na kama kitambulisho cha Mbuga hiyo kwa miaka zaidi ya 200 halafu unakuja unauliza kabisa kwamba Eti
wakiondolewa kuna hasara gani...Wazungu hawaji kuwaona Simba ngorongoro au swala wangetaka wangeenda serengeti au manyara...Wanaenda kuona pia utamaduni wa kimasai ambal pia ni kivutio cha utalii...
Sasa Nataka UJUE kingine hiki kwamba Ngorongoro Haiko chini Ya TANAPA iko chini ya NCA Ngorongoro Conservation Area...
ngoja nikupe key za eneo kuchukua sifa hizo... Yaani kuwa na conservative property ...
kwanza huwa ni Multiple land Uses,Human settlements,Cultiral and historical significant, Geological Features na Management approach
So nakuomba please kama hujaelewa ruksa kuuliza ili usije kuongea vitu usivyovijua tena