Tundu Lissu akamatwa na Polisi akiwa Ngorongoro hotel Wilayani Karatu
Yes. na kama hatufanyi kama Americans solution sio kuwahamisha wamasai kwa excuse ya uhufadhi.

Wamasai kwa namna ya pekee wana Co exist na ecology ya NCA, hakuna endangered spp ambae anawindwa kwa namna yeyote na wamasai, tena wao ndio wenye interests na indigenous knowledge ya conservation ya hizo endangered big mammals.

Kuwaondoa Wamasai haisaidii kabisa ku preserve NCA.. ni hisia za wahifadhi uchwara kuliko sayansi.
Nilidhani unakuja na tafiti kumbe bado ni hisia basi. Population ya Wamasai Kumbuka inaongezeka kitu ambacho ni hatari kwa hifadhi. Kuhamishwa pale na kupewa nyumba,hati ya Ardhi ni jambo jema sana kwa ngudu zetu hao
 
Nilidhani unakuja na tafiti kumbe bado ni hisia basi. Population ya Wamasai Kumbuka inaongezeka kitu ambacho ni hatari kwa hifadhi. Kuhamishwa pale na kupewa nyumba,hati ya Ardhi ni jambo jema sana kwa ngudu zetu hao
Nimekuliza swali rahisi hujibu..
Population inaongezeka NCA peke yake? Encroachment ya makazi ipo NCA pekee? Au mbuga zote ? Ukinijibu nitaendelea.. uache kupambania vitu vilivyo nje ya uwezo wako.
 
Kwahiyo na yale matusi ulifanya sarcism kamanda? Utafiti tayari umefanyika ndiyo maana Serikali ikafanya uamuzi wa hivyo. Population ya Masai Tz na Kenya ni tofauti,alafu Kenya wanaweza kua na njia tofauti nasio lazma tufanye kama wao.
Aisee nahisi Lowasa alikuwa Sahihi tunahitaji ELIMU SANA...
cha kwanza sijakutukana Cha kabisa...
Cha pili kama uliweza kuleta Evidence inaonyesha hiyo Tafiti,I will be gratifull sana Maana me nakupa Facts Tu...

Kusema kwamba Population ya Masai ilin kenya na Tanzania ni Tofauti nakubaliana na wewe kabisa ila kwa mlengo upi.? Sikiliza ...

Kenya kuna eneo Dogo sana wanalokaa wamasai Tofauti ma Tanzania ambao eneo ni kubwa cha ajabu ni kwamba Pamoja ya kuwa na eneo Dogo Masai wa kenya Wako Half a milion yaani zaidi ya laki tano huku Tanzania ikiwa na wamasai kwa Takwimu waliotaja Juzi walisema zaid ya Laki mbili ikiwa ni Pungufu kwa kenya kwa Watu laki Tatu....

Ramani Ifuatayo inaonyesha Mgawanyiko wa Eneo la wamasai kwa Tanzania na Kenya
Maasaimap.gif

Kama utaangalia Ramanin utagundua Sehemu kubwa ya eneo La wamasai lipo Tanzania Japo kuna idadi ndogo sana ya Masai na Kenya kuna eneo dogo ila kuna idadi kubwa sana ya masai...

Sasa ikiwa kenya eneo ni hilo Na wanaishi wamasai zaidi ya laki tano (500,000s) huku tanzania. Eneo likiwa ni kubwa na walikuwa wanaishi wamasai only 200,000..
Unafikiri Rais wa Kenya Hakuona kuna haja ya enviromental RESERVATION ...

I THINK KAMA KUNA MTU ALIYUROGA BASI NAONA SASA NI ULE MUDA AFANYE ZINGUO MAANA TUNATESEKA SANA MAANA HATA UKWELI KWETU HATUUONI....NI KAMA TUMEFUMBWA MACHO

Some sources
 
Jeshi la Polisi wilaya ya Karatu wameamuru kufungwa kwa ofisi ya Chadema wilaya ya Karatu na kuwakamata watu wengine wakiwemo viongozi wa Chadema wa wilaya hiyo.

1. Joseph Mtui
2. John Malle
3. Fabiola Niima
4. Daniel Mnyampanda
5. Eliya Kibola, Katibu wa Chadema wilaya ya Karatu
6. Valerian Qurama
7. Samwel Welwel, Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Karatu

UCHAMBUZI YA YANAYOENDELEA MKOANI ARUSHA LOLIONDO, NGORONGORO NA ARUSHA

Mfumo wa kiubaguzi wa serikali ya CCM hauna tofauti na mfumo wa kibaguzi uliokuwepo nchini Afrika Kusini kabla ya kubomolewa mwaka 1994 .

Vitendo vya serikali ya kikaburu ya CCM kuwaandama wapinzani kwa kuwakamata, kuwasweka rumande, kufunga ofisi za vyama vya upinzani, kuzuia vyombo vya habari kufanya kazi kwa uhuru, kuzuia mikutano mbinu hizi hazitofautiana na vyombo vya dola vya enzi ya kikaburu ya wachache Afrika ya Kusini kutumia vyombo vya dola kukandamiza wengine.

Afrika ya Kusini, Ubaguzi wa kimfumo ulianza enzi ya ukoloni: mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20, serikali ya kikoloni ya Uingereza iliweka upya vikundi vya rangi kwa kisingizio cha kukabiliana na milipuko ya magonjwa katika vitongoji vilivyojaa watu. Eneo ambalo sasa linajulikana kama Soweto lilikaliwa na watu weusi na watu wengine wasio weupe ambao walihamishwa baada ya kuzuka kwa tauni ya bubonic katikati mwa Johannesburg. Utengano wa mapema ulirasimishwa na kuimarishwa na sheria za kikoloni kama vile Sheria ya Ardhi ya Wenyeji ya 1913, ambayo ilihifadhi karibu asilimia 90 ya ardhi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya watu weupe walio wachache. Katika miongo iliyofuata, ambapo Afrika Kusini ikawa jamhuri huru, msururu wa sheria za kupitisha na kufurika zilizuia haki za watu wasio wazungu. Wakati wa Enzi ya Ubaguzi wa rangi, kuanzia 1948 hadi 1994, chama tawala cha Nationalist Party, kilichotawaliwa na Waafrika wazungu, kilipitisha sheria za upotoshaji, utengano wa kisheria wa kitaasisi, kurasimisha kategoria za rangi na vizuizi vya harakati, na kupachika ubaguzi wa rangi katika mazingira. Majiji yaliwekwa “kwa ajili ya wazungu pekee,” na miji midogo ikawa, kwa kweli, utaratibu wa kuwaweka wafanyakazi wasio wazungu. Sera kama hizo ziliharakisha ukuaji wa vitongoji tofauti nchini kote kwa viwango vyote - kutoka miji kama Cape Town na Johannesburg hadi vijiji vidogo zaidi. Soma zaidi source : South Africa after Apartheid: From Township to Town

Serikali ya CCM nayo imekopi kwa miaka mingi sera, mifumo na siasa za kibaguzi za kikoloni.

Kitendo na maamuzi ya vyombo vya dola kwa maagizo ya serikali ya CCM Tanzania kufanya maeneo fulani ya nchi kuwa yatengwe (no go zone), kuhamisha watu kwa nguvu, kufunga huduma za kijamii kama afya, elimu pia kuhamisha ofisi za serikali kutoka Loliondo ns Ngorongoro na kuzihamisha sehemu nyingine ili watu wateseke na kulazimika kuhama au kuishi kwa mateso wakibaki.

Na pia maeneo hayo ambayo serikali imeamua kutenda ubaguzi na kuyatenga kuzuia watu wengine kuingia kuongea nao au kufanya mikutano ni aina ya ubaguzi wa kikaburu wa iliyokuwa Afrika ya Kusini ilivyotawaliwa na wachache kwa kutumia nguvu kubwa ya dola vibaya.

Yanayotokea sasa na kuendelea Ngorongoro na maeneo mengine ya Tanzania yaliyo karibu au kupakana na mbuga au hifadhi kama Tarime, Serengeti, Geita, aKagera migodini n.k ni kiashiria kuwa CCM sasa ipo katika mikono ya wachache wabaguzi walafi wa Mali na maliasili na tutegemee pia suala la bandari kupewa wageni kama DP World litatekelezwa kwa nguvu zote kama inavyoendelea katika Ngorongoro Loliondo.

Hivyo watanzania ni wakati wa kuamka na kutambua kuwa ukiona wenzio wananyolewa basi kama hatutachukua hatua za kupinga na kupiga kelele basi tutie maji nywele zetu kusubiri kupunyuliwa kwa nguvu na sera hizi mbovu za CCM popote pale tulipo Tanganyika na Zanzibar.
 
Kuna tetesi kuwa Tundu Lissu amekamatwa na Polisi asubuhi hii akiwa hotelini huko Karatu.

Taarifa zaidi kukujia hapahapa jukwaani.

UPDATE:
Waliokamatwa Karatu hadi sasa ni
  1. Makamu Mwenyekiti CHADEMA Tundu Lissu
  2. Walinzi wote wa Tundu Lissu
  3. Katibu wa BAWACHA Catherine Ruge
  4. Mzee Hashim, Mwenyekiti Wa Baraza La Wazee CHADEMA Taifa
  5. Suzan Kiwanga na
  6. Mwandishi wa Jambo TV (Oscar).

Polisi wanaendelea kuwatafuta wengine walio ambatana na Tundu Lissu Wilayani Karatu

View attachment 2744826

====

Leo Septemba 10, 2023 Majira ya saa nne asubuhi Jeshi la Polisi wilaya ya Karatu lilifika Hotel ya Ngorongoro iliyopo Karatu na kuizingira, Polisi hao wakiwa na mitutu ya bunduki pamoja na mabomu. Jeshi hilo liliwaeleza wahudumu wa hotel hiyo kuwa wanataka kujua chumba alicholala Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara Mhe. Tundu Lissu wakaelezwa na kwenda kwenye chumba hicho.

Baada ya purukushani ya Jeshi la Polisi na walinzi wa Mhe. Lissu, Jeshi hilo lilingia kwa nguvu katika chumba alichofikia Mhe. Lissu na kuondoka nae bila kueleza wanaenda nae wapi.

Baadae wengine waliokamatwa na Jeshi hilo ni Mhe. Susan Kiwanga, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mhe. Catherine Ruge Katibu Bawacha Taifa, Mhe. Twaha Mwaipaya, walinzi wa Mhe. Lissu pamoja na watu wengine.

Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea Karatu.
View attachment 2744848
Samwel Welwel

===

Jeshi la Polisi wilaya ya Karatu wameamuru kufungwa kwa ofisi ya Chadema wilaya ya Karatu na kuwakamata watu wengine wakiwemo viongozi wa Chadema wa wilaya hiyo.

1. Joseph Mtui
2. John Malle
3. Fabiola Niima
4. Daniel Mnyampanda
5. Eliya Kibola, Katibu wa Chadema wilaya ya Karatu
6. Valerian Qurama
7. Samwel Welwel, Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Karatu
Huyu maza ni gaidi haswa ila lilikuwa ni suala la muda tu kuonyesha sura yake halisi, amejificha kwenye dini
 
Kwenye nchi za watu weusi inataka moyo wa chuma kutetea raia wake ambao kimsingi hata hawaelewi haki zao na faida ya mwanaharakati kama tundu lissu, freeman Aikaeli, John pambalu, twaha mwaipaya na wengine wengi.. Itafika wakati mapinduzi yafanywe na wachache tu tukitegemea watanzania waandamane kudai haki hapo hatutaweza

Kifuatacho ni Chama kuandaa mbinu kabambe za kukabiliana na ccm pasipo nguvu ya umma maana umma wenyewe hawana meno ndio maana serikali inajitafunia nchi inavyotaka.. Tundu lissu inabidi ajuwe kuwa hao anaowatetea ndohaohao wakishapewa ardhi ya ngorongoro watamshukuru Samia Kwa kuwaacha waendelee kuishi ndani ya hifadhi kuliko lissu aliepambana kuwatetea
Umesema kweli haswa
 
Kwenye nchi za watu weusi inataka moyo wa chuma kutetea raia wake ambao kimsingi hata hawaelewi haki zao na faida ya mwanaharakati kama tundu lissu, freeman Aikaeli, John pambalu, twaha mwaipaya na wengine wengi.. Itafika wakati mapinduzi yafanywe na wachache tu tukitegemea watanzania waandamane kudai haki hapo hatutaweza

Kifuatacho ni Chama kuandaa mbinu kabambe za kukabiliana na ccm pasipo nguvu ya umma maana umma wenyewe hawana meno ndio maana serikali inajitafunia nchi inavyotaka.. Tundu lissu inabidi ajuwe kuwa hao anaowatetea ndohaohao wakishapewa ardhi ya ngorongoro watamshukuru Samia Kwa kuwaacha waendelee kuishi ndani ya hifadhi kuliko lissu aliepambana kuwatetea
Asante
Ila jifunze kuandika MAJINA ya watu kwa herufi husika.
 
Jeiwii mbona mnatazama tu huu uonevu kwa raia wema wa nchi hii,wanaotetea wenzao dhidi ya ukandamizwaji wanaofanyiwa. Tena hawavunji Sheria za nchi ila polisi ndio wanaokiuka katiba na Sheria. Tunawaomba JWTZ mtusaidie raia wa nchi hii. Tumechoka kunyanyaswa ndani ya nchi yetu. Maadui sio lazima watoke nje ya mipaka ya nchi yetu! Tumegundua maadui wabaya zaidi wapo ndani ya mipaka. Kweli Bora wakoloni wazungu warudi kututawala kuliko kutawaliwa na hawa viongozi wanaotunyanyasa na kuharibu nchi kiasi hiki. Ee Mwenyezi Mungu tusaidie.
Jeiwii hii ya Mkunda?? Au nyingine
 
Kawaite tec wasome waraka wakuipangia serekali tuna mabaraza mawili tu tec na binge ndiowanaisimamia serekali au unaongeza latatu nachadema?
Ndio umeandika nini mama mkwe?
 
Back
Top Bottom