Tundu Lissu akamatwa na Polisi akiwa Ngorongoro hotel Wilayani Karatu
Kuna tetesi kuwa Tundu Lissu amekamatwa na Polisi asubuhi hii akiwa hotelini huko Karatu.

Taarifa zaidi kukujia hapahapa jukwaani.

UPDATE:
Waliokamatwa Karatu hadi sasa ni
  1. Makamu Mwenyekiti CHADEMA Tundu Lissu
  2. Walinzi wote wa Tundu Lissu
  3. Katibu wa BAWACHA Catherine Ruge
  4. Mzee Hashim, Mwenyekiti Wa Baraza La Wazee CHADEMA Taifa
  5. Suzan Kiwanga na
  6. Mwandishi wa Jambo TV (Oscar).

Polisi wanaendelea kuwatafuta wengine walio ambatana na Tundu Lissu Wilayani Karatu

View attachment 2744826

====

Leo Septemba 10, 2023 Majira ya saa nne asubuhi Jeshi la Polisi wilaya ya Karatu lilifika Hotel ya Ngorongoro iliyopo Karatu na kuizingira, Polisi hao wakiwa na mitutu ya bunduki pamoja na mabomu. Jeshi hilo liliwaeleza wahudumu wa hotel hiyo kuwa wanataka kujua chumba alicholala Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara Mhe. Tundu Lissu wakaelezwa na kwenda kwenye chumba hicho.

Baada ya purukushani ya Jeshi la Polisi na walinzi wa Mhe. Lissu, Jeshi hilo lilingia kwa nguvu katika chumba alichofikia Mhe. Lissu na kuondoka nae bila kueleza wanaenda nae wapi.

Baadae wengine waliokamatwa na Jeshi hilo ni Mhe. Susan Kiwanga, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mhe. Catherine Ruge Katibu Bawacha Taifa, Mhe. Twaha Mwaipaya, walinzi wa Mhe. Lissu pamoja na watu wengine.

Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea Karatu.
View attachment 2744848
Samwel Welwel

===

Jeshi la Polisi wilaya ya Karatu wameamuru kufungwa kwa ofisi ya Chadema wilaya ya Karatu na kuwakamata watu wengine wakiwemo viongozi wa Chadema wa wilaya hiyo.

1. Joseph Mtui
2. John Malle
3. Fabiola Niima
4. Daniel Mnyampanda
5. Eliya Kibola, Katibu wa Chadema wilaya ya Karatu
6. Valerian Qurama
7. Samwel Welwel, Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Karatu
Wakamatwe na washughulikiwe kisawasawa wasituharibie amani yetu washinzi hawa wengine hawakawii kukimbilia ubalozi kikiwaka na kusindikizwa hadi airport kwenda ughaibuni. Siwapendi watu kama hawa.
 
Katika hali ambayo sasa ni dhahiri kwamba ni kuvuka Mstari Mwekundu , Jeshi la Polisi limeamuru kufungwa kwa ofisi za Chadema Karatu .

Pamoja na hilo Polisi wameendelea kukamata watu hovyo kwa maelekezo ya ccm .

Bali tunachotaka kukumbusha ni kwamba Kazi ya Polisi ni ajira ya muda mfupi tu , na tunaweza kuthibitisha yaliyowakuta Polisi wakubwa sana kuliko huyo RPC wa Arusha .

Omari Mahita aliyekuwa IGP katili zaidi kuliko yeyote Tangu kuundwa kwa Jeshi la Polisi Tanzania , baada ya kustaafu tu ALIKAMATWA NA KUBURUZWA MAHAKAMANI KWA KESI YA AIBU YA KUBAKA HOUSE GIRL WAKE MWENYEWE NA KISHA KUMJAZA MIMBA NA KUKIMBIA MATUNZO YA MTOTO .

Kutokana na Aibu hii Mahita leo hawezi kusimama popote na akaheshimiwa , hata Ule Msikiti alioujenga Morogoro Mjini , Waislam wameukataa , umebaki kuwa mazalia ya popo na mijusi .

Ushahidi umo humu humu JF , kwahiyo kumbe upolisi wako hautakusaidia chochote huko mbele , ni vema kazi ya polisi ikafanywa kwa weledi kwa vile askari hana kinga yoyote ile , hata kama anatumwa na ccm kama alivyotumwa Mahita .

Screenshot_2023-09-10-15-14-31-1.png

Screenshot_2023-09-10-15-14-56-1.png
 
Duh

Kikosi cha Kisasi

Njama

Kikomo

Hujuma

Hivi Vitabu viliandikwa na mzee Musiba na sterling alikuwa Willy Gamba 😂😂🔥
 
Hao badala ya kufanya siasa wamegeuka kua wanaharakati wakudandia matukio na kuchonganisha serikali na raia, sisi upinzani hatujui siasa,....tumeshindwa kujenga grassroot ofisi za chama na kufungua matawi kwa kuuza philosophy za chama tunatafuta umaharufu kupitia matukio mbali mbali.
Kuna haja ya kupata chama cha siasa ambacho kinaweza kujenga sera mbadala ya chama tawala sio kupunga kila jambo bila kuonyesha mbadala wake, Lissu amakua mwanaharakati sio mwana siasa tena bora angefungua NGO ya kutetea hakati zake, kama ni mazingira au haki za binaadamu ili ajulikane iko wapi.
Wanaofanya siasa ndio hawa wanaopora uchaguzi kila siku? Vyama karibia vyote vina sera mbadala wa hizo za CCM, tatizo wakati wa uchaguzi wanaoamua nani atangazwe mshindi ni hao hao Makada wa CCM. Kwa kukusaidia tu, CCM haiko madarakani hadi leo kwa ubora wa sera, bali ni kwa sababu za kihistoria na katiba ya mfumo wa chama kimoja inayokibeba.
 
Kwenye nchi za watu weusi inataka moyo wa chuma kutetea raia wake ambao kimsingi hata hawaelewi haki zao na faida ya mwanaharakati kama tundu lissu, freeman Aikaeli, John pambalu, twaha mwaipaya na wengine wengi.. Itafika wakati mapinduzi yafanywe na wachache tu tukitegemea watanzania waandamane kudai haki hapo hatutaweza

Kifuatacho ni Chama kuandaa mbinu kabambe za kukabiliana na ccm pasipo nguvu ya umma maana umma wenyewe hawana meno ndio maana serikali inajitafunia nchi inavyotaka.. Tundu lissu inabidi ajuwe kuwa hao anaowatetea ndohaohao wakishapewa ardhi ya ngorongoro watamshukuru Samia Kwa kuwaacha waendelee kuishi ndani ya hifadhi kuliko lissu aliepambana kuwatetea
Kimantiki ninakubaliana na wewe.
Ila nadhani tutapishana kwenye hiyo nguvu ya umma unayoitegemea wewe.
Hakuna nchi yoyote ambako watu wote ndani ya nchi hiyo waliamka na kukataa yaliyokuwa yakifanywa na watawala wa nchi hiyo.

Kinachofanyika, ni kundi kubwa la watu wanaojizatiti na kuwa na moyo wa kufanya wanayonuia kuyafanya; hawa wengine wanafuata nyuma.

Ndiyo maana kila mara tunawasihi CHADEMA wawe na watu walio na msimamo dhahiri katika kusimamia wanayotaka kuyafanya, kuleta mabadiliko ndani ya nchi hii. CHADEMA hawawezi kusubiri umma wa waTanzania wote wawaunge mkono ndipo wafanye mageuzi hayo

Kwa hiyo, wanachotakiwa kukipa kipaumbele CHADEMA ni kuwa na mkakati maalum wa kujenga kundi hili lenye uaminifu kufuata na kutimiza adhma ya kuyaleta mabadiliko haya.

Tunasema hapa kila mara, pamoja na umuhimu wake, hizi juhudi za majukwaani na nyomi nyingi, lakini bila ya kuwa na mikakati nyuma yake ni kupoteza nguvu nyingi sana huku wakijua CCM wao kazi yao ni rahisi tu, kutumia DPLA kuwatia jambajamba hao wanaojaza nyomi zao.

Huko ndani ya CHADEMA, hasa Makao makuu, ni lazima wajipange vizuri na kuweka program za chama zinazokazia njia za kuzuia uhalifu unaofanywa na CCM kila mahali, na hasa kwenye kura nyakati za chaguzi.
 
Kuna tetesi kuwa Tundu Lissu amekamatwa na Polisi asubuhi hii akiwa hotelini huko Karatu.

Taarifa zaidi kukujia hapahapa jukwaani.

UPDATE:
Waliokamatwa Karatu hadi sasa ni
  1. Makamu Mwenyekiti CHADEMA Tundu Lissu
  2. Walinzi wote wa Tundu Lissu
  3. Katibu wa BAWACHA Catherine Ruge
  4. Mzee Hashim, Mwenyekiti Wa Baraza La Wazee CHADEMA Taifa
  5. Suzan Kiwanga na
  6. Mwandishi wa Jambo TV (Oscar).

Polisi wanaendelea kuwatafuta wengine walio ambatana na Tundu Lissu Wilayani Karatu

View attachment 2744826

====

Leo Septemba 10, 2023 Majira ya saa nne asubuhi Jeshi la Polisi wilaya ya Karatu lilifika Hotel ya Ngorongoro iliyopo Karatu na kuizingira, Polisi hao wakiwa na mitutu ya bunduki pamoja na mabomu. Jeshi hilo liliwaeleza wahudumu wa hotel hiyo kuwa wanataka kujua chumba alicholala Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara Mhe. Tundu Lissu wakaelezwa na kwenda kwenye chumba hicho.

Baada ya purukushani ya Jeshi la Polisi na walinzi wa Mhe. Lissu, Jeshi hilo lilingia kwa nguvu katika chumba alichofikia Mhe. Lissu na kuondoka nae bila kueleza wanaenda nae wapi.

Baadae wengine waliokamatwa na Jeshi hilo ni Mhe. Susan Kiwanga, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mhe. Catherine Ruge Katibu Bawacha Taifa, Mhe. Twaha Mwaipaya, walinzi wa Mhe. Lissu pamoja na watu wengine.

Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea Karatu.
View attachment 2744848
Samwel Welwel

===

Jeshi la Polisi wilaya ya Karatu wameamuru kufungwa kwa ofisi ya Chadema wilaya ya Karatu na kuwakamata watu wengine wakiwemo viongozi wa Chadema wa wilaya hiyo.

1. Joseph Mtui
2. John Malle
3. Fabiola Niima
4. Daniel Mnyampanda
5. Eliya Kibola, Katibu wa Chadema wilaya ya Karatu
6. Valerian Qurama
7. Samwel Welwel, Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Karatu
Mnatamba hamuogopi , mkiguswa kidogo mnataka dunia ielewe- kumbe mnaogopa
 
Watoto wa 2000 kuja huku juu ambao hawakuiona filamu ya Serafina ya kwa Zulu natali watizame karatu/Ngorongoro hakuna kilicho tofauti.
Freedom is coming tomorrow!!!
 
Back
Top Bottom