Tundu Lissu akamatwa na Polisi akiwa Ngorongoro hotel Wilayani Karatu
Siasa bila hoja ya kutembea nayo maana yake umeshindwa kuwa mbadala wa alie madarakani,sasa lazima utafute hoja ya kuzungumza ili wananchi wajue kuwa upo active, ndicho wanachofanya chadema,ila ukweli wanaujua vizur kuwa CCM wako sahihi katika Hilo
Hizo sio hoja ni utetezi unajua akili za watanzania wanajua vyama vinafanya haya kwa Kujitetea wao wenyewe ....Wanatetea Watu wsioweza kupaza sauti na wanapaza kwa sababu yao.....UKITAKA KUJUA KUWA MPINZANI NI KAZI SUBIRI CCM AWW MPINZANI NDO UTAJUA KUWA NI NGUMU NA INAUMIZA
 
Katibu mkuu wa Chadema mh John Mnyika amesema wamewafuatilia Viongozi wao Waliokamatwa kwenye Vituo mbalimbali vya Polisi Bila Mafanikio

Mnyika ameliomba Jeshi la Polisi liufahamishe Umma walipo Viongozi hao

Ahsanteni
Duh...!. It's high time Chadema wajifunze kutumia the legal remedies prescribed kwenye sheria zetu, wa file kitu kinachoitwa Habeas corpus
P
 
As population keep on growing mazingira ya mbugani ambalo wamasai wanaishi na mifugo Yao watagharim future ya mbuga zetu na wanyama,labda kama hujafika maeneo hayo basi huwezi jua uhalisia uliopo
Kwanza karibu. pole na buku 7 kwa cku naona imerudi kwa kasi ya kuelekea 2025. Jipange lakini
 
Hata wakikamatwa, tunataka hoja zijibiwe...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Hapa ndiyo mara zato unaweza kuwashangaa wasomi wetu. Hivi hapo wanapoishi wamasai nchini Kenya kuna hifadhi gani? Je,unajua kua Wamasai wa Tanzania wanayo mifugo mingi kuliko hao wa Kenya?
Kila wakati huwa nasema ni vyema kuficha ujinga( sio tusi) ili kutokujua kwako wasije wanao wakasoma hizi comments baadae wakaona mshua wao chenga...

Sasa nilipost Ramani kwenye post za nyuma kidogo kukuonyesha Hifadhi zilizopo au zilizo na wamasai zilizopo Kenya ila kwakuwa lengo lilikuwa ni kuja kuAttack na sio kupta knowledge hukuziona sasa nakupa tena kwa majina Hifadhi za Taifa zilizo na wamasai kenya....

Kwanza naomba kumake Kwanza correction...
Idadi ya Wamasai wa Kenya ilihesabiwa kuwa 1,189,522 katika sensa ya mwaka 2019 na sio 500,000 kama nilivyosema.... Hilo ni eneo la masai na eneo lote ni eneo la hifadhi kwa Tanzania na kwa Kenya....

Nimeshangaa sana kutokujua kuwa wakenya nao wanaishi kwenye hifadhi na hii ni iliteracy ya hali ya juu sana...Sasa nakusaidia chache....

  • Hifadhi ya Taifa ya Amboseli
  • Hifadhi ya Taifa ya Ol Donyo Sabuk
  • Hifadhi ya Taifa ya Sibiloi
  • Hifadhi ya Taifa ya Mlima Longonot
  • Hifadhi ya Taifa ya Mlima Elgon
  • Hifadhi ya Taifa ya Masai Mara
Maasaimap.gif

Tukisema ongezeko la population nadhani inabidi tusifungie kwenye watu tu....nenda zaidi mpaka kwenye livestock.

Wamasai wa kenya ndo wanaMiliki Ngombe na mifugo wengi sana kuliko Tanzania fanya Research....

Hii ndo Ramani Ya Kenya Isome mkuu usiongee kitu usichojua....
Nationalparker_i_kenya.png
 
Katibu mkuu wa Chadema mh John Mnyika amesema wamewafuatilia Viongozi wao Waliokamatwa kwenye Vituo mbalimbali vya Polisi Bila Mafanikio

Mnyika ameliomba Jeshi la Polisi liufahamishe Umma walipo Viongozi hao

Ahsanteni

Sauti na zipazwe relentlessly...
 
Wamemmiss wanataka wazunguke nae kisha watamuachia tu.
 
Back
Top Bottom