Tundu Lissu akamatwa na Polisi akiwa Ngorongoro hotel Wilayani Karatu
Katibu mkuu wa Chadema mh John Mnyika amesema wamewafuatilia Viongozi wao Waliokamatwa kwenye Vituo mbalimbali vya Polisi Bila Mafanikio

Mnyika ameliomba Jeshi la Polisi liufahamishe Umma walipo Viongozi hao

Ahsanteni
Kuna gari lisilojulikana limepinduka karibu na kundi la fisi karibu ya ngorongoro. Tatizo la fisi hawaachi hata mfupa.

Dah isijekuwa lussu kawa chakula cha fisi?
 
Serikali ipo sahihi kabisa katika Hilo suala la kuwahamisha maasai hapo ngorongoro ila chadema wanataka kutumia suala Hilo kisiasa baada ya kufeli katika ishu ya DP World na bandari
Yaani wewe kibwengo maji unaongea nini? DP World ashinde nani huyo Bibi yenu? Ngedere hawana lolote lile
 
Mwambulukusi, mdudu, slaa na askofu wao anaevaa gauni Ia pinki, mbona wapo kimya mpaka saa hizi?
 
Jeshi lindeni Mali za nchi kama wakati Magufuri.
 
Hata wakikamatwa, tunataka hoja zijibiwe...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Mkuu nimecopy ntakuwa naisema kila mahali
 
Kwa sababu huyu Tundu Lissu ni naturally kind. Hana hasira kama nyati. Halafu lengo la kumkamata limekwishatimia. Alikuwa anataka kwenda Ngorongoro kuwalaghai wale Wamasai illiterate. Lakini polisi wamemzuia.

Nitaandika zaidi,lakini sasa nataka kwenda kwenye sala ya Ishaa. No,labda niandike zaidi. Huyu Tundu Lissu afya yake siyo nzuri.

Ukimweka detention inabidi utafute muuguzi. Halafu,Tundu Lissu akipata matatizo sasa hivi mahabusu reaction ya Watanzania inaweza kuwa unpredictable.

Uzuri wa Polisi wa Tanzania ni kwamba they are very professional katika utendaji kazi. Hawawezi kukaa na mtu huko halafu wakamdhalilisha.
 
Kuna tetesi kuwa Tundu Lissu amekamatwa na Polisi asubuhi hii akiwa hotelini huko Karatu.

Taarifa zaidi kukujia hapahapa jukwaani.

UPDATE:
Waliokamatwa Karatu hadi sasa ni
  1. Makamu Mwenyekiti CHADEMA Tundu Lissu
  2. Walinzi wote wa Tundu Lissu
  3. Katibu wa BAWACHA Catherine Ruge
  4. Mzee Hashim, Mwenyekiti Wa Baraza La Wazee CHADEMA Taifa
  5. Suzan Kiwanga na
  6. Mwandishi wa Jambo TV (Oscar).

Polisi wanaendelea kuwatafuta wengine walio ambatana na Tundu Lissu Wilayani Karatu

View attachment 2744826

====

Leo Septemba 10, 2023 Majira ya saa nne asubuhi Jeshi la Polisi wilaya ya Karatu lilifika Hotel ya Ngorongoro iliyopo Karatu na kuizingira, Polisi hao wakiwa na mitutu ya bunduki pamoja na mabomu. Jeshi hilo liliwaeleza wahudumu wa hotel hiyo kuwa wanataka kujua chumba alicholala Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara Mhe. Tundu Lissu wakaelezwa na kwenda kwenye chumba hicho.

Baada ya purukushani ya Jeshi la Polisi na walinzi wa Mhe. Lissu, Jeshi hilo lilingia kwa nguvu katika chumba alichofikia Mhe. Lissu na kuondoka nae bila kueleza wanaenda nae wapi.

Baadae wengine waliokamatwa na Jeshi hilo ni Mhe. Susan Kiwanga, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mhe. Catherine Ruge Katibu Bawacha Taifa, Mhe. Twaha Mwaipaya, walinzi wa Mhe. Lissu pamoja na watu wengine.

Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea Karatu.
View attachment 2744848
Samwel Welwel

===

Jeshi la Polisi wilaya ya Karatu wameamuru kufungwa kwa ofisi ya Chadema wilaya ya Karatu na kuwakamata watu wengine wakiwemo viongozi wa Chadema wa wilaya hiyo.

1. Joseph Mtui
2. John Malle
3. Fabiola Niima
4. Daniel Mnyampanda
5. Eliya Kibola, Katibu wa Chadema wilaya ya Karatu
6. Valerian Qurama
7. Samwel Welwel, Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Karatu
Mwanakulitafuta mwanakuligeti.
 
Wanawapaisha tu.
Chadema hairudi nyuma tena.
 
Back
Top Bottom