Tundu Lissu: Aliyenipa ushahidi wa pesa za Abdul na mama yake kwa sasa ni marehemu

Tundu Lissu: Aliyenipa ushahidi wa pesa za Abdul na mama yake kwa sasa ni marehemu

Hahahaa.

Sicheki Lissu kupigwa risasi.

Nacheka tu jinsi narrative inavyoanza kubadilika kidogo kidogo.

Mwanzoni villain alikuwa Magufuli.

Sasa hivi kibao kimeanza kubadilika kidogo kidogo.

Muda si mrefu kuna mtu atatapika yote aliyonayo moyoni.

Ila kwa huu ufa ulioanza kujionyesha, CHADEMA haitokuwa tena kama ilivyokuwa zamani.

Hii CHADEMA ya sasa na ijayo, ni dhaifu sana.

Na kuhusu Mbowe, kuna watu humu walikuwa wanahoji sana ushiriki wake katika kupotea kwa Ben Saanane na kushambuliwa kwa Lissu.

Hiyo ilikuwa ni kipindi kile cha Magufuli.

Lakini kwa vile Magufuli ndo alikuwa villain kwa wakati huo, jaribio lolote lile la hata kuhoji tu uwezekano wa labda Mbowe alikuwa anajua zaidi kuhusu hayo matukio kuliko na alivyokuwa anaonekana, lilikumbwa na push back kali sana toka kwa makamanda.

Like, how dare you question our dear chairman! Mbowe ndiye aliyekodi ndege binafsi kum airlift Lissu kwenda Nairobi akiwa hajitambui.

Anywho, ngoja niendelee kuangalia hii ngoma iliyo inogile.

Ila idea ya kwamba sasa Mbowe ameanza kuwa villain, ni tamu kuliko cranberry sauce iliyopo kwenye menu ya kesho kwenye mlo wa Krismasi 🤣.

It will be sweet to watch what transpires.
💯
 
wapi kasema Samia anaupiga mwingi? Unajua kama siyo "maridhiano" hata mikutano ya vyama ingelikuwa bado imefungiwa? Kesi 400 plus zingelikuwa bado mahakamani, etc etc. Sema kuwa huo ni mwanzo.... bado mengi ya kufaya kuleta utawala bora, katiba mpya tume huru y uchaguzi etc etc.

NIKUULIZE: Lisu atamlazimishaje samia alete katiba mpya? Tume huru ya uchaguzi? naomba jibu. kwanini hajafanya leo na jana, mpaka awe mwenyekiti?
Kwa vile Mbowe ameshindwa basi na Lissu naye hataweza??? Wewe jamaa una mahaba makali sana kwa Mbowe.
 
Mgombea Uenyekiti wa Chadema Tundu Lissu amefunguka kupitia Twitter space jinsi alivyokusanya ushahidi wa kutosha kuhusu rushwa ya pesa za Abdul na mama yake kwa viongozi wa Chadema.

Ameeleza kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati kuu ya Chama cha CHADEMA aliyempatia ushahidi wa kina kuhusiana na tuhuma hizo na aliyemsaidia kuthibitisha tuhuma hizo mbele ya kamati kuu ya Chama cha CHADEMA kwa sasa ni Marehemu. Hata hivyo Lissu alikataa kumtaja Mjumbe huyo akidai kwamba haitasaidia kitu chochote.

Na alipoulizwa iwapo kifo cha Mzee Ali Kibao kinahusiana na tuhuma za pesa za Abdul aliomba asilizungumzie Hilo kwa sasa.
Mpe 5
 
evidence, evidence, evidence...... anatoa revelations tu bila ushahidi.. kama akina Mbowe wangelikuwa kama yeye, wangelibwatuka tu na kumvika uongo kama anavyofanya yeye........

Fine sasa anashindwa nini kumuondoa Samia madarakani, kinamzuia nini ambacho atakipata kwenye uenyekiti?
Kumbe una utoto na mahaba hadi yamekutoa ufahamu.
 
Lisu anajua anachofanya! Lisu ni mropokaji ila anaropoka vitu ambavyo ni sahihi yaani hana uwezo wa kutunza siri li friji lake haligandishi. Anachosema sasa ndo ukweli wenyewe kwamba mauaji ya wanachadema yanafadhiliwa na mamlaka ya juu ndani ya Chadema yenyewe.

Kuna wanachadema wamepotea wengine hawakuwa hata na athari zozote kwa serikali hata wananchi wengi wamewajua baada ya kutangazwa kuwa wamepotea au wamekua akiwemo huyo babu Kibao.

Hao watu watakuwa walionekana threat kwa mtu au kundi flan ndani ya CHADEMA na kundi hilo likaamua kuwaondoa kikatili wakijua atakayesingiziwa ni serikali/usalama/polisi ila sasa ukweli unaanza kuonekana.

Yaani CHADEMA inaua Chadema
Hapo kwa Kibao nakukatalia,taarifa alizokuwa nazo ni very damaging kwa Dola,elewa tuhuma za fedha za Abdul zinamgusa moja kwa moja Rais wa nchi.
 
"Mbowe Kapokea pesa za Abdul, mmojawapo wa watu wa CHADEMA aliyetoa hii Siri, anauliwa kinyama! na execution squad ya CCM! "

If it walks like duck, smells like a duck, then it's a duck.

Mbowe anatumika, ni compromised na CCM kuiua CHADEMA kutokea ndani, yupo kwenye payroll ya state,! Anafanya alichowahi kufanya Mabere Marando ndani ya NCCR Mageuzi.

Kama ni kweli na sio conspiracy theory,
... quacks like a duck, then...

yo' dead right chief.
 
Mkuu, Kibao alikuwa ni mtu wa karibu sana wa Mbowe. Na alikuwa anajua mengi.

Tutafakari:
1. Mwenyekiti anafuatwa gerezani na ''watu wasiojulikana'' na kufanya mazungumzo ya kina.

2. Anatolewa gerezani na kwenda kwa mama moja kwa moja na wafanya mazungumzo ya faragha wao wawili tu.

3. Abdul na makapu yake yaliyojaa fedha anamtembelea mwenyekiti na baadhi ya viongozi wa chama na anaondoka makapu yakiwa tupu.

3. Mwenyekiti anaambiwa amuunganishe Abdul na Lissu ili naye apate mgao wake na anamteua Wenjele kufanya hiyo kazi.

4. Wenjele na Abdul wanakwenda na makapu yao yaliyojaa fedha kwa Lissu lakini Lissu anayakataa.

5. Lissu anafanya uchunguzi mkali na wa siri na mzee Kibao anampa details zote.

6. Lissu anaanika hadharani kuhusu makapu ya fedha.

7. Mwenyekiti anaitisha kikao ili amwadhibu Lissu

8. Lissu anatoa ushahidi wa kina na mwenyekiti anaufyata.

9. Mwenyekiti anagundua kumbe Kibao alitoa siri.

10. Mwenyekiti anamrudia Abdul na kumweleza alichofanya Kibao, na Abdul anamwambia mama, na mama anamwambia mkuu wa ''wasiojulikana'' na ''wasiojulikana'' wanatumwa kufanya waliyofanya.

11. Wakati wa mazishi ya Kibao, familia inakuja juu lakini mwenyekiti anaingilia kati kinafiki na kusema wawe na adabu.
Mkuu umepita mule mule,kifo cha Kibao ni colabo ya Mbowe na Dola.
 
Halafu kuna watu wanataka eti Lissu akayasemee vikaoni. Akasemee vikaoni mambo ya kutuumiza sisi wananchi huku waliomo kikaoni ni wahusika wa kutuuza?.

Wacha Lissu aseme ukweli ili tujue, kama tunaanza upya kwenye mageuzi tuanze upya!
Ukweli kwenye vikao aliyasema lakini akapuuzwa ndiyo maana ameamua kuyaketa kwenye mahakama ya umma ambayo haipokei rushwa na ndiyo kama hivi ukweli tumeujua hivyo kazi kwetu kuwakataa hawa vibaraka wa dola.
 
Ukweli kwenye vikao aliyasema lakini akapuuzwa ndiyo maana ameamua kuyaketa kwenye mahakama ya umma ambayo haipokei rushwa na ndiyo kama hivi ukweli tumeujua hivyo kazi kwetu kuwakataa hawa vibaraka wa dola.

Tena kafanya vyema kuyaleta la sivyo wangemmaliza kimyakimya kwa sababu anajua mengi!
 
Back
Top Bottom