Tundu Lissu: Aliyenipa ushahidi wa pesa za Abdul na mama yake kwa sasa ni marehemu

Tundu Lissu: Aliyenipa ushahidi wa pesa za Abdul na mama yake kwa sasa ni marehemu

Wanaotekwa, Wanaouliwa Na wanaofanyiwa mambo ya Kinyama wote wanafanyiwa na Vyama vyao Ila Kisingizio mama samia na Serikali yake au Kisingizio Magu na Serikali yak..
Huu Ni ushahidi Kamili kwamba Chama Changu cha CCM Hakihusiki na Yote yanayotajwa Eeh Mungu nisamehe kwa Kuchukia Chama changu ns Kutamani Uongozi ubadilike..

Pia Lucas Mwashambwa Nisamehe Mdogo wangu Ukweli sasa Unaanza kidogo kidogo kufahamika
Kuwa Serikali haihusiki
You've missed the point.

Uhusika wa wapinzani ni tuhuma za kushirikiana na system/dola/CCM/serikali kuteka, kutesa na kuua. Dola ndio wenye vyombo na mfumo wa utekelezaji. Kisha kuzuia uchunguzi na kupoteza ushahidi. Hakuna chama cha upinzani kinachoweza kufanya utekaji na mauaji nchi hii kikabaki salama mbele ya serikali na vyombo vya dola.
 
CHADEMA wasikieni tu kwa uchafu, watu wanakifuata hiki chama sababu tu wanaichukia CCM. Wapenda rushwa, wazushi, wakabila, wajivuni, wana chuki na mengine mengi. If they are real serious ni wakati wa kumpa uenyekiti Lissu tuone kama watarudi kwenye misingi ya awali iliyo kijenga chama.
 
You've missed the point.

Uhusika wa wapinzani ni tuhuma za kushirikiana na system/dola/CCM/serikali kuteka, kutesa na kuua. Ndio wenye vyombo na mfumo wa utekelezaji. Kisha kuzuia uchunguzi na kupoteza ushahidi. Hakuna chama cha upinzani kinachoweza kufanya utekaji na mauaji nchi hii kikabaki salama mbele ya serikali na vyombo vya dola.
Huwezi jua Yaliyofichikana Huwenda Kuna Ushirikiano na Benefit fulani mutual Benefit ys Pande mbili
 
Hayupo kwenye system na hataweza kuwepo ni wale wa unampa laki 5 akusifie mtandaoni au asikuandike vibaya ndio maaisha ya vijana mtandaoni huko Twitter (x)
Hahaha, kuna mtu aliwahi kunipigia simu kimakosa akidhani mimi ni Yericko Nyerere, alinitukana sana. Maelezo yake alisema alimtumia Yericko hela ili amtumie vitabu (kama nakumbuka vizuri) lakini miezi sita ikapita bila jamaa kupata mzigo wake.
 
Mbowe anamsema Magufuli Kila Siku Bila kuweka Ushaidi lakin husemi kitu kuhusu hilo. Lakin Samia Kaharibu Uchaguzi , Watu wanatekwa na kuuawa lakini Mbowe anasema mama anaupiga mwingi na maridhianao yan maana kubwa kwake,

Je, maridhiano yana maana ipi kwa Chadema na Taifa kwa ujumla kama watu wanatekwa na kuuawa? inawezekana maridhiano yana maana kubwa kwake kwa kusamehewa Kesi ya Ugaidi na Lisu amesema Aliyempa maelezo ya kina Juu rushwa Kwenye Chama sasa ameuawa!!

Ally Kibao ameuwa Kipindi Cha mama lakini Mbowe anakwambia maridhiano yana maana. Je, Maridhiano yana maana gani Kama watu wanauwawa Na Chaguzi zinaharibiwa?

Kwa nini Mbowe amekomaa na Marehemu Magufuli ilihali watu wanakufa na Chaguzi zinaharibiwa na Samia na anaridhika na Uongozi wake?
Kipi kimejificha na kinachowaunganisha Mbowe na Samia?
Ukishaona mtu anakomaa na marehemu jua kwamba ameshindwa kutimiza wajibu wake. Kwa jamii zilizo staarabika mtu hawezi thubutu kutupa lawama kwa marehemu kwa matatizo ya wakati huo. Ni upumbavu wa hali ya juu watu kuendelea kumsingizia Magufuli kwa mambo mabaya yanayo endelea hivi sasa hapa nchini.
 
Aisee. Hard to believe.

CHADEMA has hit the bottom this time.

That Mbowe could fall from grace this hard i.e. from archangel to devil incarnate?

Anyway, naendelea kusoma. Wanasema ukweli hupanda ngazi.

Ikithibitika, basi nitaamini Mbowe ni "genius" wa aina yake. Mtu pekee aliyeweza kujenga chama makini cha upinzani kinachotikisa nchi nzima tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa uanzishwe nchini. Akaweza kutuaminisha wataka mageuzi wengi kuwa yeye na chama chake wamedhamiria kabisa 100% kupambania mageuzi nchini kwa miaka yote hii (>20). Never did we doubt CHADEMA.

HALAFU mtu huyo leo ijulikane kuwa alikuwa akikitumia chama hicho hicho kama mkakati wake wa kujiweka vyema zaidi na utawala hatari wa CCM ili kupata manufaa (yasiyoeleweka) hata kwa kuuza damu za makada wa chama chake? Such ruthlessness? LAZIMA atakuwa mtu muovu kweli kweli. inahitaji akili kubwa sana, subira ndefu sana, na roho mbaya sana kwa binadamu wenzako kuwa na mkakati wa aina hiyo: AN EVIL GENIUS.

Bado siamini. NASUBIRI ukweli.
 
Hahahaa.

Sicheki Lissu kupigwa risasi.

Nacheka tu jinsi narrative inavyoanza kubadilika kidogo kidogo.

Mwanzoni villain alikuwa Magufuli.

Sasa hivi kibao kimeanza kubadilika kidogo kidogo.

Muda si mrefu kuna mtu atatapika yote aliyonayo moyoni.

Ila kwa huu ufa ulioanza kujionyesha, CHADEMA haitokuwa tena kama ilivyokuwa zamani.

Hii CHADEMA ya sasa na ijayo, ni dhaifu sana.

Na kuhusu Mbowe, kuna watu humu walikuwa wanahoji sana ushiriki wake katika kupotea kwa Ben Saanane na kushambuliwa kwa Lissu.

Hiyo ilikuwa ni kipindi kile cha Magufuli.

Lakini kwa vile Magufuli ndo alikuwa villain kwa wakati huo, jaribio lolote lile la hata kuhoji tu uwezekano wa labda Mbowe alikuwa anajua zaidi kuhusu hayo matukio kuliko na alivyokuwa anaonekana, lilikumbwa na push back kali sana toka kwa makamanda.

Like, how dare you question our dear chairman! Mbowe ndiye aliyekodi ndege binafsi kum airlift Lissu kwenda Nairobi akiwa hajitambui.

Anywho, ngoja niendelee kuangalia hii ngoma iliyo inogile.

Ila idea ya kwamba sasa Mbowe ameanza kuwa villain, ni tamu kuliko cranberry sauce iliyopo kwenye menu ya kesho kwenye mlo wa Krismasi 🤣.

It will be sweet to watch what transpires.
Tuliwahi kuhoji tukatukanwa sana
 
Back
Top Bottom