Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amebadili upepo wa siasa. Watanzania tumuunge mkono

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amebadili upepo wa siasa. Watanzania tumuunge mkono

Ujio wa Lissu umewazindua Watanzania wengi wameona kumbe inawezekana...

Lisu pamoja na kujibu hoja anaenda samba na kufundisha somo la Katiba na Sheria kutambua haki zako zinavyolindwa kikatiba.
Mungu atusaidie tuamke wote
 
Kwa Watanzania wenye akili timamu mtakubaliana nami kuwa miaka 5 ya awamu hii ya 5, kimekuwa kipindi kigumu sana kilichojaa;

Hofu
Mashaka
Umasikini uliotopea
Ombwe la kiuongozi nk...
Tumuunge mkono kwa kila mbinu, hakuna namna. Miaka mitano ya Magufuli ya kuswaga binadama kama mifugo inatosha!
 
Magufuli amefanikiwa kuwajengea hofu kuhusu utawala wake, ndio maana ujasiri wa Lissu unawashitua wengi kwa sasa.

Watanzania wengi wetu taumwa ule ugonjwa niuitao "ukondoo wa Nyerere". Huyu baba kwa kutuingiza kwenye chama kimoja ambacho alihahakisha kinakuwa chamadola alitufunga akili. Akaweka katiba ya raisi wa kifalme na hata tulipokwenda vyama vingi katiba ile ilibaki kuwa ya chama kioja. Hakutumia maguvu waziwazi lakini ukipishana nae cha mtema kuni ulikiona hadi watanzania tukawa waoga. Huu uoga wetu na kujifanya mambo yako shwari ndio nauita ukondoo wa nyerere. Bahati mbaya huu hurithishwa toka kwa wazazi kwenda ka watoto.

Serikali zote baada ya Nyerere, kila moja kwa njia yake zimetukumbusha hayo mambo, wenyewe wakituambia tu kisiwa cha amani lakini polisi wao wakitushughulikia pale sauti zetu zilipopanda. Huyu wa sasa amekazia tu na sasa wengi wetu tunaimba mapambio na kulalama tukiwa huko mbali. Fikiria vyombo vyetu vya habari-mpaka vinakata matangazo au vinakata sauti za watu wanao zungumza.

Kudhibiti huu ugonjwa tunahitaji mtu wa aina yake na wa kipekee atuongoze na hapa ndiyo anapo ingia Tundu Lissu-aina ya mwana siasa ambaye ni nadra sana na anaefaa kupambana na ukondoo wa nyerere pamoja na mfumo wetu uliopo. Ashinde asishinde lakini kama atapata nafasi ya kupeperusha bendera ya Upinzani au Chadema siasa za Tanzania zitapita kwenye tanuru na wengi watapata elimu na hamasa zitakazo wafanya wawe imara zaidi kisiasa.
 
Watanzania wengi wetu taumwa ule ugonjwa niuitao "ukondoo wa Nyerere". Huyu baba kwa kutuingiza kwenye chama kimoja ambacho alihahakisha kinakuwa chamadola alitufunga akili. Akaweka katiba ya raisi wa kifalme na hata tulipokwenda vyama vingi katiba ile ilibaki kuwa ya chama kioja...
Tunahitaji kubadilika
 
Back
Top Bottom