Tundu Lissu ameongea na Radio Citizen Kenya asubuhi ya leo, ameleezea hali ya usalama nchini pamoja na suala la Corona

Tundu Lissu ameongea na Radio Citizen Kenya asubuhi ya leo, ameleezea hali ya usalama nchini pamoja na suala la Corona

Lissu awe makini sana kutumia Media za Kenya maana tayari Tanzania na Kenya hatuko na maelewano mazuri.

Ningemshauri atumie Radio ujerumani na BBC hizi ni radio Neutral na zinaushawishi nchini.

Hiki kitengo cha propaganda cha CHADEMA siku hizi kimejaa vilaza watupu.

Fame aliyoijenga Lissu kwa miaka kumi anaweza kuiharibu kwa media talk ya nusu saa tu.

Sijui nani anamshauri kutumia media za Kenya

Cc.CHADEMA

Wakenya walimsaidia sana Lissu, ana haki ya kuipenda nchi hiyo
 
Nasikia wakenya watapiga Kura Tanzania Oktoba 28, 2020!

Kuna watu wanapenda umbea au ndio lisemwalo lipooo?
 
Pamoja na vyombo vyote kuegemea ccm lkn wananchi watz hawa wameikataa ccm.....

Mimi nashangaa ina maana uchumi wa kati upo kwenye koo za viongozi wa ccm? Maana malofa hawauoni kabisaaa
 
Unajua wakenya wamemsaidiaje huyu Nabii yetu........Wkt serikali yenu inataka afe wakenya walijitolea kwa hali na mali.

Alafu vyombo vyenu takataka mbona haviripoti matukio ya chadema???....
CHADEMA wanatakiwa kupeleka malalamiko rasmi tume ya uchaguzi na MCT kwa vyombo vya habari kugoma kutangaza matukio ya CHADEMA.
 
Unaposema "matusi ya binafsi" inakupasa uiweke hoja hiyo wazi zaidi hasa kuhusiana na hao wagombea wawili uliowataja hapo awali. Be explicit!

Maana neno "matusi" linaweza kutumika vibaya kuendana na uelewa wa watu tofauti tofauti. Kwa mwingine, mgombea anapozikosoa sera za mgombea aliyeko madarakani hudhani kuwa ni matusi.

Kuna shida kubwa nimeiona ya matumizi ya neno "matusi" kwamba limerahisishwa sana kimatumizi. Imefikia hatua hata mtu anapomkosoa fulani kwa hoja yenye mashiko kabisa, baadhi ya watu huishia husema anatoa matusi pengine kwa sababu tu ya kukerwa na hoja hiyo.

Ni vyema ukaiweka hoja yako wazi na kwa ufafanuzi wa kina kuhusu "matusi" na kuhusiana na hao wagombea wawili uliowataja hapo awali.
Naunga hoja yako mkono, na ikimpendeza atwambie kwa mfano walau matusi mawili ambayo Lisu na Membe wametukana toka waanze michakato ya uteuzi katika vyama vyao mpaka uchukuaji fomu tume ya Taifa ya uchaguzi.
 
Ni vizuri nchi jirani tushirikiane nazo kumuondoa nduli wetu huyu mpiga makelele.....

Rais Tundu Lissu Rais
 
Yaani mie huyu simuelewi kabisa, hivi wapiga kula wake wako kenya?, Watanzania wangapi wana access na hizo radio za kenya!
Wewe kiazi.. sasa Kama Tz jiwe amezuia matangazo yote afanye nini?

Hata wanao ukiwanyima chakula wanaenda kula kwa jirani
 
Yaani mie huyu simuelewi kabisa, hivi wapiga kula wake wako kenya?, Watanzania wangapi wana access na hizo radio za kenya!
Unadhani Tanzania kapewa access akakataa ? Ukiona hivyo ujue vyomba vyetu vya habari vina UKAKASI
 
Awe makini kuhusu maswali ya mtego kuhusu Korona.

Wakenya wanataka kumtumia Lissu kipropaganda kuhusu ishu ya Korona ili ionekane sisi watanzania tumefanya ujinga tulivyopambana na Korona halafu wao Wakenya eti wamefanya vyema na malockdown yao.

Lissu akumbuke tu wapiga kura wake watarajiwa yaani Watanzania wanamuunga mkono sana Magufuli kwenye ishu ya kutoweka lockdown, kwa hiyo asiwape Wakenya wanachotaka yaani "endorsement" kutoka ndani ya Tanzania kwa jinsi wao walivyodeal na Korona. Maana sasa hivi ndani ya Kenya kuna public pressure ya kutaka Kenya ifanye kama Tanzania!.

Swali la Korona inabidi Lissu alijibu kisiasa, ila akijaribu kuiponda approach ya Magufuli alivyohandle hilo suala atapoteza uungwaji mkono nchini. Magufuli alifanikiwa kuvurugavuruga vyanzo vya taarifa rasmi kuhusu Korona, kisha akapiga propaganda kubwa sana kuwa tumeidhibiti Korona kiasi kwamba sehemu kubwa ya umma inakubaliana naye. Kwa hiyo inahitaji akili ya ziada kucrash sehemu kubwa ya approach ya Magufuli katika mapambano dhidi ya Korona
Ni kweli.. kwa issue ya korona amuunge mkono jiwe tuu
 
Yaani mie huyu simuelewi kabisa, hivi wapiga kula wake wako kenya?, Watanzania wangapi wana access na hizo radio za kenya!
Citizen inasikika Tanzania. Waache platform maana vyombo vya habari vya Tanzania hawataki kumpa muda wa kuongea tutasikiliza nyie mumetupa kama mfupa wapo wanaokota
 
Huyu anataka kuongoza hii nchi.. huku akikimbilia kutuonyesha hataki kutumia.. vyombo vya habari vya nchini.. huyu angeuza nchi yetu kama angebahatika kuchaguliwa kuwa Rais..

Anaonyesha yupo radhi.. media za nchi za nje ziendelee.. kuliko za nchini.. mpenda mabeberu.. hajali uchumi wa nchi yetu.. wala kusaidia kutengeneza ajira.. kwa sababu kawaona bora Kenyans waendelee.. poleni washabiki wake wafwu..

Magufuli 💯 Mzalendo
Propaganda za kichina zimepitwa na wakati. Hutudanganyiki munakataaa asihojiwe na vyombo vya serikali vya chama chenu na binafsi wacha atumie vya jirani tutamsikiliza
 
Lissu na Membe wao wanapiga kampeini za hasira binafsi dhidi ya Magufuli; hilo linajulikana kabisa; siyo kuwa wanashindana na sera za CCM. Sasa awe makini atakapokuwa anatumia vyombo vya nje kumtukana Magufuli kama alivyokuwa anafanya alipokuwa Ulaya. Watangazaji wa Kenya wanaweza kabisa kumwuliza maswali yanayoelekea huko, na akishindwa kuwa makini atajikuta anatoa matusi tena, jambo litakalokuwa inakiuka kanuni za uchaguzi.
Kama kanuni za uchaguzi zinazuia kutukanana .......... Mbona Lowassa alitukanwa sana 2015 na hatukusikia mtu alilalamika kuwa kanuni zinavunjwa!!
 
Go Go Lissu Go Go......Sisi tutakusikiliza kwa njia yoyote unayotaka kuongea na watz na dunia ww
 
Ukweli ni kuwa hii ni aibu kubwa kwa vyombo vya habari vya hapa nyumbani,
Hivi inawezekanaje akili zao wote zikashikiwa sehemu moja?
 
Hivi Lisu anataka urais wa tz au Kenya?

Maana ukiangalia hata katika hotuba zake zote hakuna inayoisha bila kutaja Kenya
 
Back
Top Bottom