Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amewahoji wafanyabiashara wanavyolipa kodi TRA kama nani?

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amewahoji wafanyabiashara wanavyolipa kodi TRA kama nani?

Suala la kulipa kodi tusilichukulie kirahisi na tusilichukulie kisiasa.
Wafanyabiashara wanatakiwa kulipa kodi stahiki. Ili biashara ziendelee kuwepo. Na si vinginevyo
CCM wametengeneza kodi ambazo si rafiki kiasi kwamba wengi hawalipi kodi hukwepa na kufanya biashara kienyeji, Lisu ataifanya kodi kuwa rafiki kiasi kwamba hakuna Mtanzania ataiona ni mzigo kwake watailipa bila shinikizo lolote.
 
Amewahoji kama Lissu binadamu, kama Lissu mgombea urais, kama Lissu makamu mwenyekiti CDM, kama Lissu rais mtarajiwa, kama Lissu mnusurika wa shambulizi lile lililoasisiwa na kina nanihii nk.

Lissu ni yule yule, hajabadilika na hatabadilika hadhi wala nafsi kwa kumhoji yeyote hata kama ni mwuuzaji kariakoo, achilia mbali nia ovu za akina jiwe, DKt. Manoti au ma lb7 wote kumwelekea yeye.
 
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA ambaye ndio mgombea urais wa JMT wa chama hicho mh Tundu Lissu amewahoji wafanyabiashara wa pembejeo sokoni kariakoo namna wanavyolipa kodi zao TRA.

Lissu alitaka pia kujua kama wafanyabiashara wana uelewa wa usahihi wa kodi wanayolipa.

Chanzo: ITV habari.

My take; Tundu Lisu amewahoji wafanyabiashara akiwa kama nani?

Maendeleo hayana vyama!
Amstadarm Aliyechangamka!
 
ITV wanaweza kuingia kikaangoni
 
kama mwanasheria,wakili msomi na raisi mtarajiwa. Vip kwani unateseka
 
kesi zake wamesema ztaskilizwa mfululizo, kwahio ajiandae kisaikolojia
ndani ya moyo wako,unajua lipi jema na lipi baya! ndani ya moyo wako unajua kama ao unaowatetea wanatenda haki mbele ya Mungu au wanatesa na kuua wasio na Hatia,ndani ya moyo wako unajua adhabu ya wauaji na wanaomwaga damu zisizo na hatia,ndani ya moyo wako unajua kama haya unayotetea ndivyo anavyotaka Mungu unaemwabudu au la.So sina cha kusema zaidi!! Mwenyezi Mungu akujalie wewe na wote wenye akili tope kama wewe lahaana ya milele
 
Lisu akiwa Rais hakuna atayelipa kodi na wote tutajua kingereza.
Nasikia Kagame alisema akipewa bandari tu ataweza kutulisha sijui alitumia kikokotoo gani kuwezajua atapata net profit kiasi gani cha kufanikisha hilo
 
Kuhoji kwamba kwanini WAKULIMA wa KOROSHO huko kusini walioporwa KOROSHO zao kifashist unatakiwa uwe na cheo? Kwamba tumeongezewa tozo/makato ya mikopo ya elimu ya juu toka 8- 15% bila hata kushirikishwa lazima uwe naa

Mpumbavu wewe
Hisia yangu ni kwamba tumejifanya kuyabeba matatizo ya wanasiasa bila wao kuyabeba ya kwetu. Eti tunakwazika sana tukisikia Lissu kapigwa risasi kuliko tukisikia mfuasi wa CHADEMA kapigwa risasi morogoro, au Mawazo wa CHADEMA kauwawa Geita.

Tumewapa wanasiasa thamani sana kuliko thamani yetu. Wengine tunaamini wanatupigania. Wengine wanavyoandika humu ndani ni kama Lissu ni ndugu yao au labda baba yao. Wanamsemea badala ya kujadiliana wengine.
 
Tunataka kizazi Cha kuhoji. Tundu Lissu kaonyesha njia.
MAGUFULI anataka kutuziba mdomo, anunue ndege Kama karanga tusiulize kwanini Hilo Jambo halikupitia bungeni.
Mnataka tuwe MAZEZETA Kama mlivyo wa CHAMA CHA MAZEZETA?
Nawe ni zezeta sana! Nini cha maana kilichowahi pitia bungeni ambacho unaweza kukionesha? Bunge lipi? Hilo la akina Mbowe na akina Zitto na Kibajaji, n.k. Utaratibu huo uliusikia mwaka gani kwamba serikali ikitaka kununua kitu inapitisha bungeni? Tatizo tunafuata yanayosemwa ana kina Lissu. Wengine wakasema tenda haikutangazwa, wengine wakasema vioo vya ndege vinaonesha zimetumika. Yooote umbumbumbu tu!
 
Tunataka kizazi Cha kuhoji. Tundu Lissu kaonyesha njia.
MAGUFULI anataka kutuziba mdomo, anunue ndege Kama karanga tusiulize kwanini Hilo Jambo halikupitia bungeni.
Mnataka tuwe MAZEZETA Kama mlivyo wa CHAMA CHA MAZEZETA?
Huyo mgombea wenu tarehe 30 aanze kutafuta flemu hapo kariakoo anze biashara, kisha atapata elimu ya mlipa kodi huko.
Kila siku TRA wanaitisha wafanyabiashara kwenda kuwapa elimu ya mlipa kodi sasa endapo hutaenda si kosa la TRA bali ni kosa la mtu binafsi.
Tundu lisu anadhani siku angepata madaraka je angeanza kwanza kuwafundisha watu haki zao ndo aanze mambo ya maendeleo?
Yeye kama anapenda Mambo ya mabishani basi atengeneze taasisi yake ya ubishi.
 
Kuhoji kwa aina ile inaonesha ni mtu anayejifunza kwa taabu. Huyu na wengine wako kundi la majivuno ya kijinga. Kila wakati, kila siku anaamini ufahamu ni vifungu vya sheria tu. Iweje miaka yote hiyo bungeni asijue wananchi wake wanalipaje kodi, hadi siku ya kugombea urais? Alichojifunza kwa miaka yopte hiyo ni nini?
Kuna watu kutozwa zaidi ya kawaida, lakini usidanganyinike, Lissu hakuuliza yale kwa nia ya kujifunza au kwa kuwa eti kwamba hajui! Lissu alikua kwenye kampeni zake, hata kama NEC wamemzuia!
 
Back
Top Bottom