Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amuunga mkono Maalim Seif Urais Zanzibar

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amuunga mkono Maalim Seif Urais Zanzibar

CHADEMA wameanza kukiri udhaifu Sasa,

Hata hapa bara pia nako watabwaga manyanga.
Hawakujipanga,sijui Lissu kwanini anasaidia watu wasiomsaidia.Kama Membe hajiondoi,basi Lissu amesaidia CCM.
 
Hawakujipanga,sijui Lissu kwanini anasaidia watu wasiomsaidia.Kama Membe hajiondoi,basi Lissu amesaidia CCM.
Ccm jueni tu kuwa ile divide and rule program yenu imeshafeli kabla haijaanza mwaka huu!!
 
Pumba kabisa.. nani kakwambia wananchi wanahitaji ofisi ya chama??
Ala, kumbe? Je, hayo mabilioni ya kodi yangu na wanannchi wengine, akiwemo wewe, hao viongozi wamefanyia nini ili nisiulize? Kama hao viongozi nao wawe na uhalali wa kuhoji kodi kutumika kwa maendeleo ya vitu. Je, wakipewa madaraka kutakuwa na usalama wa hazina na msliasili za nchi?
 
Maamuzi yote mazito ya chama huamuliwa na vikao vizito vya chama..

CHADEMA kupitia vikao vyake Halali vya kamati kuu, baraza kuu na mkutano mkuu waliteua mgombea urais wa Zanzibar

Lissu kasema kura za Zanzibar apewe Maalim Seif wa ACT wazalendo kajitamkia bila ridhaa ya kamati kuu, baraza kuu wala mkutano kuu.

CHADEMA Hayo maamuzi aliyotamka Lissu mlikaa kikao gani kuyaamua?

Mgombea wenu anavunja katiba ya CHADEMA mchana kweupe.

Sasa huyo mgombea mliyemwidhinisha kuwa agombee urais Zanzibar mbona mnatapeli mchana kweupe.
Mwaka huu mtatafuta kura kwa tochi. Siyo bara wala visiwani.
 
Wajiondoe zanzibar sasa huyo mgombea wao yeye atamnadi T Lisu au atakuwa na kazi gani?
Mmeshikwa pabaya subiri bara Membe atoe neno mtajua mpango wa Mungu ulivyo toka kifo hadi Ufalme mtapata tabu sana wasaliti
 
Lissu ni mwanasheria anayeheshimika, lakini kwahili la jana nimepata mashaka kidogo kalifanya kienyeji mno.

Chadema ni taasisi iliyosajiliwa na inaendesha mambo yake kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu, sasa hili la kuachiana ugombea na ACT mlikubaliana lini? MoU iko wapi? Lissu kama mwanasheria wa chama hebu tuambie ni kikao gani kilichokaa mkakubaliana kumwachia maalimu saif Zanziber?

Na kama kweli umeamua kumuunga mkono maalim Saif basi panda nae jukwaani umnadi na muombee kura

Kwa kauli yako ya jana Membe atapata wakati mgumu sana kufanya kampeni kwani ataonekana kinganganizi. Kesho Zitto anazindua kampeni Kigoma ni ya Kumnadi Lissu au Membe?
 
Sasa kuna hoja kubwa kwenye uchaguzi huu zaidi ya hii??? Hakuna katiba mpya ya warioba bila CCM kutoka madarakani??? Hakuna uhuru wa Zanzibar bila CCM kutoka madarakani, Hakuna Uhuru, haki na maendeleo bila CCM kutoka madarakani!!!

Mnalo mwaka huu mataga [emoji23][emoji23][emoji3]
Hapo umenena kuliko huyo anayeomba WaTz wamwamini kumkabidhi nchi ati kwa nia ya kuiondoa CCM madarakani.

Hoja zako (Katiba na Uhuru wa Zanzibar) zinajadilika na kuhitaji ridhaa ya WaTz, CCM iwe madarakani au la na si kwa kiongozi kuamua.
 
Nmeshangaa mlkivyo wajinga na hamkujipanga!

Unajua kabisa chadema na act wana itikadi tofauti sasa unategemea mkishinda mtaingozaje?

Yani Lisu akivusha 20%ya kura nipigwe ban ya maisha hapa jf
Ban utapigwa tu, maana hakuna namna nyingine, tatizo kwa hizi tabu unazopata kila siku, usije kwenda peponi na lichama lako la mboga mboga!
 
Chadema ni wajinga sana!

Sasa hiyo ni nini?

Sasa hii nchi mtaitawala vipi?

Yani kule act huku chadema, nchi moja itikadi 2.

Hakuna system ya kijinga kugawa mchi vipande namna hii.
Ona ng'ombe hii! Sasa kwanini kuna tume mbili za uchaguzi? ZEC na NEC kwa pamoja zinafanya kazi lakini independently sasa unategemea nini?
Yaani akili za maccm za ajabu sana
 
Hapo umenena kuliko huyo anayeomba WaTz wamwamini kumkabidhi nchi ati kwa nia ya kuiondoa CCM madarakani.

Hoja zako (Katiba na Uhuru wa Zanzibar) zinajadilika na kuhitaji ridhaa ya WaTz, CCM iwe madarakani au la na si kwa kiongozi kuamua.
Sasa nilichokisema mimi ndo anachokimaanisha huyu kiongozi mbeba maono Tundu Antiphas Lissu
 
Ona ng'ombe hii! Sasa kwanini kuna tume mbili za uchaguzi? ZEC na NEC kwa pamoja zinafanya kazi lakini independently sasa unategemea nini?
Yaani akili za maccm za ajabu sana
NEC siyo itikadi za vyama we kidagaa wa hapo ufipa
 
Back
Top Bottom