Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,270
- 2,822
Kwenye majukwaa ya siasa za ujenzi na kuimarisha chama, hotuba za maandishi ni sumu ambayo itaboa audience yote na hutapata wasikilizaji unless uwe umewabeba kwa malori na kuwapa posho kama wafanyavyo CCM maana hao watakuwa watumwa wako hata kama unamwaga uharo, watakuvumilia tu kukusikiliza hadi mwisho hata kama watakuwa wanasinzia...Ndomana ni kheri kwake kama angeichapa hotuba Kwa maandishi aende na kuusoma kupitia kipaza sauti.
Hotuba za kuandika huwa ni za wale waliokariri kilometa za barabara, vyumba vya madaraka, madaraja na matundu ya vyoo ili kuepuka kusahau
Kwenye majukwaa za uimarishaji chama kama wanavyofanya CHADEMA sasa, unakwenda na kuzungumza na wananchi juu matatizo ya Kila siku na mengine hutoka hapohapo Kwa njia ya maswali au kusema wao kuwa tuna shida hii au ile. Na kazi yako ni kui - address changamoto ipasavyo..
Tundu Lissu namkubali sana huyu jamaa. He's an expert kwenye hili. He's a very good public speaker. Anajua kuteka akili na mawazo ya hadhira. Hakuna mtu aweza kuondoka asipende kuendelea kumsikiliza hatua kwa hatua..
Fuatilia mikutano yake inayoendelea Kanda ya ziwa utathibitisha hili nisemalo..
NOTE: Fuatilia mkutano wa Chato YouTube channels siku mbili tatu zilizopita. The guy was at his best na Kila mwa- Chato aliyefika na kusikiliza nondo za jamaa siku hiyo ali - appreciate kuliko kawaida...
The same happened at Misungwi - Mwanza today. Again, Tundu Lissu delivered and he was at his best..!!