Uchaguzi 2020 Tundu Lissu anajitutumua kuitumia Corona kisiasa lakini wapi!

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu anajitutumua kuitumia Corona kisiasa lakini wapi!

Amezungumzia historia ya utendaji wa Magufuli katika miaka yake mitano, hajazungumzia korona tu.

Kazungumzia:

1.kauli za Magufuli kipindi cha tetemeko Kagera
2. kauli za Magufuli kipindi cha ukame wa njaa
3. kauli za Magufuli kipindi cha Korona
4. Kauli za Magufuli wananchi wanapomdai nyongeza za mishahara

Yote haya ameyazungumza kuwaonyesha na kuwakumbusha Watanzania aina ya kiongozi tuliye naye na umuhimu wa kumbadilisha ili tuweke mwingine atakayewasaidia wananchi kipindi cha majanga na atakayekuwa na kauli za staha na heshima kwa wananchi!
Kwa hiyo wewe kwa hakili yako unaona nani anafaaa baada ya sisi wananchi kuhacha kumpigia magufuri kula?
 
Sikuwai jua ilijamaa lileta uzi ni linafiki kwa kiwango hiki.
wakati Lissu akiwa hajaonyesha mpango wa kurudi nyumbani, alikuwa anavunga yupo neutral, lakini sasa amejivika ngozi yake halisi.
*kweli maafrika ndivyo yalivyo*
 
Mimi uncle wangu juzi kafariki singida kwa Corona yaani anazikwa juma nne. Wajinga wachache wanasababisha ndugu zetu kufa kwa ushabiki wa Siasa. Ngoja upoteze mtu ndiyo utajua Corona ipo
Kama hawa wajinga wachache wanaficha wewe umepata wapi kipimo cha kukuonyesha kuwa kafa na Corona wakati hao wajinga wachache ndo wana vipimo?
 
Kuna wengi wanakufa kijana mwingine wa Arusha tulisoma naye Ilboru naye kafariki wiki mbili sasa. Kwasababu alikuwa na kisukari Corona ilimpeleka haraka sana. Uliza kwenye watu walio group za Ilboru kama si kweli ndugu yetu Elisante kafariki kwa Corona
Iliboru huwa mnasoma masomo ya sayansi? Unajuaje Kama alikufa kwa Corona?
 
"Tusikubali kuletewa barakoa,tengenezeni zenu,kwanza barakoa inafanana na sidiria zenu,kateni sidiria ziwe barakoa "...

Kwa kweli mh alitudhalilisha sana,

Kuwa nguo tunayovaa ndani ndo tuvae hadharani,udhalilishaji kwa wanawake,bora angesema wavae singilend au boxa
Je wewe unauhakika haujidhalilishi?,wadada wangapi wanatembea nazo adharani kama ni za ndani?,kiko wapi cha aibu hapo unachokiona wakati watoto wa kike ndo watembea uchi
 
Sasa kuna haja gani kurejea yaliyopita kama yashaonekana hayana lolote?

Wewe upo ‘rockdown’? Unavaa barakoa?
Ngabu, mpambano wa hoja upo katika mtizamo wa kigezo cha yale yaliyokwisha kufanyika na kuainisha madhaifu yake. Hizo ndizo "grounds" za upinzani. Hoja kinzani ipo ktk mtizamo hasi ili kuweka muonekano wa kimbadala wa jinsi ya mambo yanavyopaswa kuwa ama kuendeshwa.

Sasa sijui wewe kama msomi unasimamia wapi. Hivi kweli unategemea upinzani kuwa sehemu ya timu ya kusifu na kuabudu kama vile ambavyo wanafiki wengi wa CCM wanavyofanya.
 
Kama hawa wajinga wachache wanaficha wewe umepata wapi kipimo cha kukuonyesha kuwa kafa na Corona wakati hao wajinga wachache ndo wana vipimo?

Wajinga ndiyo wanaoamini hakuna Corona. Madaktari wanajua wagojwa wa Corona na tofauti na mwezi wa nne vipimo vipo mfano kwenda Kenya huingii bila kupimwa? kuna watu wanapimwa kila siku hospital hizo Pia zina vipimo huwezi kasema havipo? tofauti no kwamba sio bure tena. Huo ni uongo kwamba serikali tu ndiyo ina vipimo hospital vipo! Tatizo lako unaamini serikali hiyo hiyo ambayo haisemi ukweli. Kuna tofauti ya madaktari na wanasisa. Ndugu wanajua na serikali wanajua kuna wagojwa ni wajinga tu ndiyo hawajui😂. Sitaendelea kujibu maswali ya kijinga kama unaamini Corona inaishia namanga kwasababu Mungu anatupenda sisi Watanzania kuliko Wakenya endelea kuamini hivyo maana Mungu ndiye aliweka mipaka ya nchi yetu😂. Tuombee Mungu chanjo ije haraka kutoka kwa mabeberu. Hivi unajua Marekani pekee imetisaidia kwenye budget ya Afya zaidi ya $600M ambayo in zaidi ya Tsh 1.2trillion lakini wanasiasa wanawaita mabeberu na kuficha Mwamba pesa ya Afya karibu yote ya chanjo za watoto na dawa ni pesa za hao wanaowaita mabeberu. Lakini wajinga au mnaojifanya wajinga hamuoni hili kwasababu ya ushabiki wa kisisa🙆. Imekuwa sifa siku hizi kujifanya mjinga
 
Leo akiwa huko Muheza ‘kwenye kampeni zake za urais’, Tundu Lissu kazungumzia tena suala la Corona.

Japo kalizungumzia kidogo tu, lakini kaligusia kwa kumkosoa tena Rais Magufuli na jinsi alivyoamua kukabiliana nayo.

Kamkosoa Magufuli kwa kuwaambia watu wasivae barakoa, ‘kwanza zinafanana na sidiria za wanawake’.

Sijui ni lini na wapi Rais alisema hivyo. Mnaojua mtanifahamisha.

Ila kwa Tundu Lissu kusimama mbele ya watu ambao hawana ‘time’ na Corona, ambao wamesimama kwa kurundikana bila kuacha nafasi, na ambao wala hawajavaa barakoa, akiwemo yeye mwenyewe, ni unafiki wa daraja la kwanza.

Kila siasa huwa ni za mahali pake. Kwa Tanzania hii, suala la Corona si hoja yenye mashiko, na kwa mtaji huo, si hoja ya ushindi.

Mbaya zaidi ni kutokitenda kile ambacho unakihubiri.

Huyo Tundu Lissu yeye anachukua tahadhari gani dhidi ya Corona tokea aje?

Ile barakoa yake aliyoivaa kwa dakika chache ile siku aliporudi, iko wapi?

Huyu jamaa ni kama vile yuko nje ya mguso na mambo ambayo Watanzania wanayajali.

Hebu mtazame hapa kuanzia dakika ya 6:30.....

Corona ni porojo tu ndio maana yeye mwenyewe hajavaa barakoa wala hao aliowakusanya hawajavaa. Yeye anahangaika kutafuta makosa ambayo hayapo ila ni tofauti ya namna ya kuona jambo lilelile kati ya wanasiasa.

Hivi yeye Lissu haoni mambo yote mazuri aliyoyafanya Rais Magufuli? Chuki imempofusha.

Wagombea urais wako 16 lakini 15 kati yao wanatafuta wadhamini kwa staha bila mbwembwe wala kukashifu wengine isipokuwa yeye tu.

Aachwe tu tusubiri hukumu tarehe 28 Oktoba ndipo atawajua vizuri watanzania.
 
Huna hoja wewe! Umeng'ang'ania ya Lissu utadhani ni mtalaka wako?
Kwamba kakuacha huku unampenda!
Mwambie Lisu aachane na suala la corona linamvua nguo,! Anaonesha jinsi gani alivyo mbumbumbu
 
Wajinga ndiyo wanaoamini hakuna Corona. Madaktari wanajua wagojwa wa Corona na tofauti na mwezi wa nne vipimo vipo mfano kwenda Kenya huingii bila kupimwa? kuna watu wanapimwa kila siku hospital hizo Pia zina vipimo huwezi kasema havipo? tofauti no kwamba sio bure tena. Huo ni uongo kwamba serikali tu ndiyo ina vipimo hospital vipo! Tatizo lako unaamini serikali hiyo hiyo ambayo haisemi ukweli. Kuna tofauti ya madaktari na wanasisa. Ndugu wanajua na serikali wanajua kuna wagojwa ni wajinga tu ndiyo hawajui😂. Sitaendelea kujibu maswali ya kijinga kama unaamini Corona inaishia namanga kwasababu Mungu anatupenda sisi Watanzania kuliko Wakenya endelea kuamini hivyo maana Mungu ndiye aliweka mipaka ya nchi yetu😂. Tuombee Mungu chanjo ije haraka kutoka kwa mabeberu. Hivi unajua Marekani pekee imetisaidia kwenye budget ya Afya zaidi ya $600M ambayo in zaidi ya Tsh 1.2trillion lakini wanasiasa wanawaita mabeberu na kuficha Mwamba pesa ya Afya karibu yote ya chanjo za watoto na dawa ni pesa za hao wanaowaita mabeberu. Lakini wajinga au mnaojifanya wajinga hamuoni hili kwasababu ya ushabiki wa kisisa🙆. Imekuwa sifa siku hizi kujifanya mjinga
Inaposemwa ugonjwa haupo sii maana ni kwa asilimia 100 kama mnavyopotosha.

Generally Tanzania hakuna corona na maisha (status quo) yanaendelea kama ilivyokuwa kabla na hakuna wimbi la vifo zaidi ya natural death rates kama zilivyokuwa. Nyinyi mnaoamini corona ipo vaeni barakoa au mjikarantini jinsi mnavyopenda lakini serikali na wananchi tunaendelea na maisha kama kawaida. Shule kuanzia chekechea hadi vyuo vikuu wanafunzi wanasoma, shughuli za kiuchumi zinarndelea kama kawaida mbanano katika vyombo vya usafiri, matamasha na mikusanyiko kama ile ya mgombea wenu inaendelea na bila athari zozote.

Serikali iko well informed kuliko nyinyi mnaojifanya kujua baada ya kutumia fursa mbalimbali zilizotolewa na serikali.

Mgombea wenu alipaswa aeleze namna atakavyoraise pesa tena kwa figures za kutekeleza mambo mbalimbali badala ya hadithi za alinacha.
 
Hahahaha kinacho muuma zaidi Lissu ni kutojibiwa hilo linamtesa sana!

Angekuwa timamu au nagekuwa sawa kisaikolojia angeachana na swala la corona maana sidhani kama kuna mtanzania au mwanachadema yeyote anaweza kumuelewa kabisa!

Na hili la Corona ndilo linazidi kumfanya watanzania wasithubutu kumpigia kura kwani wengi wameshaogopa kuwekwa karantini!
Lisu ni mbumbumbu ambae anaendeshwa na mizuka ya washabiki wake!

Hivi haoni kabisa kama suala la corona ndio liliosababisha hadi Mbowe kwenda kulewa na kuvunjika mguu baada ya kiki yake ya kujiweka karantine na kusababisha kutimuana na wabunge wake
 
Inaposemwa ugonjwa haupo sii maana ni kwa asilimia 100 kama mnavyopotosha.

Generally Tanzania hakuna corona na maisha (status quo) yanaendelea kama ilivyokuwa kabla na hakuna wimbi la vifo zaidi ya natural death rates kama zilivyokuwa. Nyinyi mnaoamini corona ipo vaeni barakoa au mjikarantini jinsi mnavyopenda lakini serikali na wananchi tunaendelea na maisha kama kawaida. Shule kuanzia chekechea hadi vyuo vikuu wanafunzi wanasoma, shughuli za kiuchumi zinarndelea kama kawaida mbanano katika vyombo vya usafiri, matamasha na mikusanyiko kama ile ya mgombea wenu inaendelea na bila athari zozote.

Serikali iko well informed kuliko nyinyi mnaojifanya kujua baada ya kutumia fursa mbalimbali zilizotolewa na serikali.

Mgombea wenu alipaswa aeleze namna atakavyoraise pesa tena kwa figures za kutekeleza mambo mbalimbali badala ya hadithi za alinacha.

Serikali ipo kweli well informed lakini inadanganya. Ukienda Kenya unahitaji certificate ya vipimo. Unavyosema wewe asilimia 100% Ya vipimo ni negative😂. Inabidi ukapime akili kama unaamini hivyo kabla ya kutoa hoja
 
Wewr ndiyo unapaswa kupimwa akili maana hata kusoma tu kilichoandikwa na kuelewa huwezi. Pole sii kila jambo lazima uchangie wakati IQ yako ni ndogo mno.
 
Kila siasa huwa ni za mahali pake. Kwa Tanzania hii, suala la Corona si hoja yenye mashiko, na kwa mtaji huo, si hoja ya ushindi.
Mie sijafika Tanzania tokea kuanza changamoto hii ya corona. Lakini tuache masihara hii changamoto imeondosha watu wala tusiichukulie kirahisi. Tundu anaweza kuwa anaifahamu vizuri maana alipotoka yeye Belgium kwa matibabu imepiga vibaya vibaya.
 
Back
Top Bottom