CCM wenyewe na hasa wanaomzunguka pamoja na TBC na TISS ndio walomharibia Jiwe. Walimtoa kwenye mazingira ya kupambana na hoja pinzani, kukutana na changamoto mbali mbali za wanaharakati na waanahabari wakamvalisha utukufu. Utukufu wa kutokosolewa, kutopingwa, kutoambiwa, kutoshauriwa, naye akapokea joho Hilo la utukufu kwa moyo mkunjufu. Akakubali kuimbiwa mapambio, kutukuzwa, kusifiwa, kuabudiwa, kuombwa, kunyenyekewa, kuona walinzi wa design mbalimbali, helcopta juu ya msafara, ujue hata Sasa anatembea kwenye kampeni hakuna cha helcopta Wala Nini lakini yuko salama, Wala hakuna anayefikiria kutenda madhara kwake. Magu akabweteka, hakujihangaisha kujua wananchi wanataka Nini, wanahoja gani,naamini angetoa mwanya wa kusikiliza mengine yangeisha jibiwa kitambo!
Sasa ona, wakati umefika, hoja zinaibuka, watu wanapinga, wanalaumu, wanashutumu, wanalalamika, Ni kipindi Cha kampeni Hali so shwari
Magu ataweza kweli kupiga kampeni yake kwa kunadi ilani ya chama, kusikiliza wapinzani wanahoja gani, kusikiliza mahitaji ya wananchi, kuandaa majibu ya hoja za wapinzani kwa wakati uleule?