Magufuli alijiamini sana kuwa mwaka 2020 atapata mserereko, tulimuonya kuwa tunapanga jeshi huko porini na siku likiingia field patatawanyika. Tukawaambia wafuasi wa CCM kuwa mwenendo wanaoenda nao kwa awamu hii ndiyo mwenendo mbaya zaidi kuwahi kuwepo Tanzania tangia enzi ya ukoloni ila wakatuita mapingapinga.
Ghafla bi vuu tunashuhudia vituko vya kila aina vya wanaccm kuombea kura, mambo yanakuwa si mambo tena. Na bado tutashuhudia maajabu ya aina yake.
Tundu Lissu kila siku kila saa anaporomosha imani ya wafuasi wa Magufuli, anamhenyesha kweli kweli Magufuli. Napenda sana na navutiwa sana na siasa za mwaka huu kwa Mgombea wa Chadema na niseme kuwa siasa za mwaka huu zinanivutia tangia kuzaliwa.
Kila siku Lissu anavyozidi kusonga mbele ndipo anapozidi kupata ushawishi tena mara dufu! Hatari hii!
Hii ni tofauti kabisa na mzee wetu wa mapanga-shaaa ambaye kila siku anaongeza wasanii mara dufu. Upo uwezekano kuwa siku za mwisho pakatokea plan B kwa Lissu ila si mnamjua? Yule ni manusura wa full magazine ya AK 47! Labda mje na ICBM za kiduku! Lissu kaza mwendo baba!
Tunaambiwa kuwa JK rasmi anaingia field kupambana. Karibu mzee wa msoga ila uzuri Lissu unamjua.
Tukutane Dodoma baadaye tutandike jukwaa.