Uchaguzi 2020 Tundu Lissu anaporomosha wafuasi wa Magufuli kila saa kila siku kwa kasi ya ajabu, JK anaingia rasmi ulingoni kupambania jahazi

Wewe unaota ndoto ya mchana kweupe.
 
Mimi akikubali katiba mpya nampa kura yangu hayo mengine Sasa hivi hata akisema watu hawamuamini, Mimi naona na msimamo wake Ila aongeze katiba mpya na ndo limebeba kura nyingi.
Mwaka 2015 alisema hivyo ila alipoingia ikulu akakana mchana kweupeeee. Yani amekana mengi aliyozungumza kwenye kampeni. Haaminiki hata kidogo!
 
Nivizuri pia utuambie kwann wasipatikane je nikwakura au kwakutowatangaza
Chama hakina wagombea makini wa ubunge
Mgombea wa urais hana uwezo wa kuutengeneza wabunge kimkakati
Chama hakina pesa

Kampeni za Lisu ni za kurukaruka, Dar, Arusha, Mwanza, Shinyanga, leo Dodoma! Na kite huko anapita kwa kuhutubia mikutano mmojammoja!
Siasa ni sayansi bro!
 
Wanaojitikeza kwenye kampeni ni 20%ya wananchi walio wengi watakaopiga kura jidanganye,sema magu mwaka huu hana mzuka kama 2015 amechoka kwa Nazi tofauti na huyo chiriku lissu lakini yakusema ni mengi mno sana.
 
CCM wenyewe na hasa wanaomzunguka pamoja na TBC na TISS ndio walomharibia Jiwe. Walimtoa kwenye mazingira ya kupambana na hoja pinzani, kukutana na changamoto mbali mbali za wanaharakati na waanahabari wakamvalisha utukufu. Utukufu wa kutokosolewa, kutopingwa, kutoambiwa, kutoshauriwa, naye akapokea joho Hilo la utukufu kwa moyo mkunjufu. Akakubali kuimbiwa mapambio, kutukuzwa, kusifiwa, kuabudiwa, kuombwa, kunyenyekewa, kuona walinzi wa design mbalimbali, helcopta juu ya msafara, ujue hata Sasa anatembea kwenye kampeni hakuna cha helcopta Wala Nini lakini yuko salama, Wala hakuna anayefikiria kutenda madhara kwake. Magu akabweteka, hakujihangaisha kujua wananchi wanataka Nini, wanahoja gani,naamini angetoa mwanya wa kusikiliza mengine yangeisha jibiwa kitambo!
Sasa ona, wakati umefika, hoja zinaibuka, watu wanapinga, wanalaumu, wanashutumu, wanalalamika, Ni kipindi Cha kampeni Hali so shwari
Magu ataweza kweli kupiga kampeni yake kwa kunadi ilani ya chama, kusikiliza wapinzani wanahoja gani, kusikiliza mahitaji ya wananchi, kuandaa majibu ya hoja za wapinzani kwa wakati uleule?
 
Hiyo ratiba. Ya Nec.
 
Upinzani ulishakufa tangu 2015, JPM kwasasa anafanya kampeni ili kutimiza matakwa ya Chama chake.

Hii kauli ya upinzani kufa aliitoa Wasira kilichofuata Mzee wa watu anajua mwenyewe.
 
Lissu ameshatuhakikishia KUINGIA BARABARANI iwapo Tume ya Magufuli itachezea kura zetu, yeye si kama Mzee Lowassa aliyeamua kumuachia Mungu tu.

alimuachia mungu au alikua tayaru ni kada wa ccm mbn alirudi yule alikua anatuchezea akili tu na breach lake la kikongo lizee nafki sana lile
 
Jamaa amepiga kampeni hadi kavimba uso na bado hatumuelewi kabisa!!!Mi nadhani angeomba Poo ccm warudi Chimwaga wakafanye mchakato upya!!!Kuhusu JK bora asisogelee mzoga unanuka sana!!Jk angerudi tu Chimwaga mchakato ukaanze upya!!Kwanza JK katusaliti kutuletea muuaji ikulu hatuna hamu naye kabisa!!!
 
LAKINI HAYO NI MAWAZO YAKO TU MKUU JPM YUKO IMARA KULIKO HAPO AWALI
 
Hv kwa tume ipi ya uchaguzi? hii hii au nyingine.Ok tusubiri wakati utakapofika
Tume yanini tukimaliza kupiga kura tunaweka kambi kwenye vituo karibia vyote Tanzania tunataka matokeo tunajumlisha na kumpata Rais muda wa kufika saa 1 jioni tunaanza maadamano nchi nzima kushinikiza aapishwe mapema

Mwaka huu Ni jino kwa jino sijuwi polisi watakuwa katika Hali gani kutudhibiti

Hawatatuweza maana tutakesha na kushinda nje mpaka pale atakapotangazwa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…