Tundu Lissu aondoka nchini kuelekea Ubelgiji. Asema anakwenda uwanja mpya wa kudai haki, demokrasia na utu wetu kwa nchi yetu

Tundu Lissu aondoka nchini kuelekea Ubelgiji. Asema anakwenda uwanja mpya wa kudai haki, demokrasia na utu wetu kwa nchi yetu

Uzoefu unaonyesha kuwa hata Oscer Kambona na Abdulahmani Babu waliporejea nchini kutoka uhamishoni waligombea uongozi wa nchi na walipofeli hawakuondoka kurudi Uingereza.
Kwani kasema atarudi lini? Pia kasema anaenda kufanya nini?
 
Aende tu na hana kheri na sisi nchi hii.

Alitaka kuifanya kama Libya mwenyezi Mungu katunusuru. Tunamuomba atunusuru tena na tena na nia ovu.
Chadema saccos
 
Aende tu na hana kheri na sisi nchi hii
alitaka kuifanya kama libya mwemyezimungu katunusuru.tunamuomba atunusuru tena na tena na nia ovu.
Chadema saccos
Alitaka kuifanya hii nchi kama Libya. Aiseee sentensi yako na what happened ni vitu viwili tofauti.
 
Katika hatua nyingine, mke wa Lissu, Alicia Magabe, ameondoka Tanzania kuelekea nchini Ubelgiji. Magabe aliondoka nchini, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mke alimtanguliza. Ila yeye akaamua kukimbilia ubalozi
Makamanda wamesimamisha mishipa ya shingo wakati mwenzao, familia ipo nje.
 
Pamoja na mengine, mtu huwezi toka nje ya nchi kuja kugombea urais tu na kuondoka, hakuna mtu atakuchagua na hakuna mtu atakukabidhi nchi.
Unafahamu Rais wa Congo hapo, alikuwa anaishi wapi na kwa muda gani kabla ya kurejea Congo na kugombea na kushinda kiti hicho?.
 
Panya ukimuona nyumbani ukimkimbiza angalia shimo anakokimbilia huko ndio Kwao Lema na Lissu wamekimbizwa Tanzania wamekimbilia mashimo ya Kenya na Kutaka kwenda USA kwa Lema ukimbizi kwa Lema na Lissu katimukia ubalozi wa ugermani na ubelgiji huko ndiko shimo lake alikotokokea...

Walitaka nchi eti
 
The fact that you had the audacity to come back inspite of the attempt on your life goes to show that you are a true patriot of this country. You have my respect. Farewell Lissu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inatia haosra majizi kuhalalisha kuwa uliopita ulikuwa ni uchanguzi. Kampuni ya afrika kusini ili print ballot paper halali. jamana wakaprint za wizi. mnadhani hatujui. mimi nipo Jamana Printers
So what! Mbona mkaombwa muingie barabarani kumuondoa mwizi wa kura mkagoma?
 
Mkuu unaishi mwezini, taratibu hapa ni uchaguzi ukiisha hakuna mikutano ya hadhara,hakuna kufanya siasa labda kwenye jimbo lako kama umefanikiwa kuupata ubunge.

Vinginevyo ni mpaka baada ya miaka mitano.
Mbona walisema wataingia barabarani?
 
Yuko wapi Tundu Lissu ambaye alituhamasisha wananchama wa CHADEMA kuandamana nchi nzima kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu, hayupo nchini ameondoka kwenda Ubelgiji huku akisindikizwa na maafisa wa Ubalozi wa Ujerumani mpaka uwanja wa ndege!!!

Hapa ndipo tunapogundua kuwa Tundu Lissu hakuwa pamoja nasi bali alikuwa anatudanganya kwa kutushawishi tuingie barabarani kuandamana na kufanya vurugu ilhali akijua kwa upande wake haitamletea matatizo kwa kuwa alishaandaliwa mpango na Mataifa ya Magharibi kuondolewa nchini baada ya kusababisha vurugu na machafuko nchini.

Sasa tunajiuliza endapo tungeingia barabarani kuandamana tungekuwa katika hali gani? Maana aliyekuwa anahamasisha maandamano angekuwa katika mazingira salama na kutuacha sisi tukiwa katika hali mbaya baada ya kusababisha vurugu nchini, tungekosa mahali pa kwenda, kwani wote walikuwa wanaunga mkono maandamano wameshapata mahali pa kujihifadhi, Tundu Lissu nchini Ubelgiji, Godbless Lema nchini Kenya, na Evarist Chahali nchini Scotland.

Hata hawa wengine akina Freeman Mbowe, Zitto Kabwe, Maria Sarungi na wengineo wana mahali pa kwenda kwani watapewa hifadhi na mabeberu ambao wanawalipa fedha nyingi kwa kuwatumikisha katika masuala kisiasa kwa maslahi ya nchi zao.

Tulikuwa tukisikia tu kuwa Tundu Lissu ni kibaraka wa mabeberu, lakini jana tumeshuhudia kwa macho yetu kuwa kweli ni kibaraka, kwani amesindikizwa na maafisa wa Ubalozi wa Ujerumani mpaka uwanja wa ndege kwa ajili ya safari yake ya kwenda nchini Ubelgiji, kwa taarifa tulizipata ni kwamba amepewa fedha nyingi na kuahidiwa kuwa watamlea hadi atakapokufa.

Tunasosoneka baada ya kugundua kuwa Tundu Lissu pamoja na viongozi wengine wa chama walikuwa wanatudanganya kwa kujifanya wako pamoja nasi kumbe tayari walikuwa wametengenezewa mazingira ya kupata hifadhi katika mataifa ya nje baada ya kushindwa kutimiza azma yao ya kusababisha machafuko nchini.

Tulipumbazwa na maneno ya Lissu na Viongozi wetu wa chama na hata tuliposikia maneno ya watu wakituambia kuwa Tundu Lissu anahamasisha tuandamane kwa sababu anajua baada ya uchaguzi ataondoka nchini na ana tiketi ya ndege ya kuondoka tulikataa na kujidanganya wenyewe kuwa atakwenda tu kwenye matibabu na kurudi, sasa tunapata wakati mgumu kuamini kuwa yaliyokuwa yakisemwa ni ya kweli.

Hata hivyo, tunamshukuru Mungu kwa kuwa hatukuingia barabarani kaundamana kwani tungekuwa tumeingia katika machafuko na kukosa mahali pa kwenda huku viongozi wetu wakiwa katika mazingira salama pamoja na familia zao.

Akili za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Back
Top Bottom