Kwakweli kama mtu akishinda ana haki ya kudai ushindi! Nawasihi CHADEMA na wapinzani wengine wote kujipanga kwa umakini mkubwa katika kuhakikisha wanapata idadi kamili ya kura walizopewa na wananchi! Itakumbukwa mwaka 2015, timu ya vijana wa waliokuwa pale mlimani City wakipokea na kujmlisha kura za Lowassa toka mikoani walitengenezewa zengwe wakavamiwa na kukamatwa eti wanajihusisha na biashara ya kusafirisha binadamu! Wakatupwa ndani mpaka uchaguzi ukapita na mshindi target akatangazwa, haijulikani mpaka leo kesi iliishia wapi! So nashauri CDM wawe makini na jambo hili ikiwezekana kituo hicho kiwekwe pasipojulikana na kifanye kazi kwa siri kubwa mpaka matokeo yote yatumwe toka nchi nzima!