Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aongea na Wahariri wa Vyombo vya Habari - Sept 9, 2020, ataenda Mahakamani kwenye kesi zake Kampeni zikiisha

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aongea na Wahariri wa Vyombo vya Habari - Sept 9, 2020, ataenda Mahakamani kwenye kesi zake Kampeni zikiisha

Hana jipya. Mguu haukunji so what?
Wewe jipya kwako ni lipi? Punguza shobo za kujifanya mswahili ilihali umetoka porini ulikokuwa unalala chumba kimoja na ndama! Halafu, badilisha hiyo avatar kwani unamharibia mamvi mwenye jina lake!
 
Maneno ya Lisu ni magumu na mazito mno kuyasikiliza!!Yanatia uchungu sana!!!!NAWAAHIDI MIMI NA FAMILIA YANGU NITAMPIGIA KURA!!!LAKINI BARABARANI SITOINGIA !!KAZI KWAKE KULINDA ASIIBIWE!!!!NAWASHAURI ASHIRIKIANE NA DIASPORA WAUNDE JESHI LA MSITUNI ILI WAJE NA OPERATION "OKOA DEMOKRASIA YETU" WAPAMBANE ILI WATANGAZWE WASHINDI!!!!!
Naunga mkono hoja 👋 👏
 
Shida ya Lissu hasemi yeye kama yeye atafanya mambo gani makubwa, tushajua magu hafai. Sasa yeye aache kila siku kumzungumzia magu badala yake aseme yeye kama yeye atafanya yapi
Alishayasema na CCM wakacopy baadhi na kuyahodhi japo hayapo kwenye ilani yao!
 
Walizoea siasa za personal attacks enzi za Kikwete sasa watanzania wamekomaa politically wanataka sera sio umbeya wa kuongelea mtu...
Kama hujasikia sera za Chadema mpaka leo basi wewe unamtindio wa akili,sababu mpaka mgombea wako anajichanganya kujibu,kuambiwa tutaongeza mishahara kwa wafanyakazi mara kajitafunatafuna mara tuliongeza kupitia kodi mara na sisi tutaongeza
 
Magu hafai kwa lipo?. Yeye anafaa kwa lipi?. Kazi kulalama tu, huyu jamaa hafai kuwa Rais.
Magu hafai kwa kufanya nchi kama nyumba yake,anatisha watu,anaminya uhuru na haki za watu hafai hata kwa ukatibu kata
 
Lisu tatizo alidanganywa na social media kudhani Magufuli hakubaliki. Sasa ameingia kwa field anaanza kulia lia, aendelee asiwandae kwanini aanze kuwandaa kisakolojia kushindwa yani siku 15 za kampeni?
Kumbe wewe juha,hivi kama ingekuwa Kuna fursa sawa nani angelalamika,vyombo vya habari vina lalamika,tume sio huru,polisi ndio ccm namba mbili
 
Aliyewafukuza TBC ndiye yuleyule analilia TBC warudi? Kweli vituko havina jina

Kiwango cha chini sana cha fikra. Hivi ukikataa kudhulumu mtu pesa, maana yake ndio hupendi pesa???

Ukirusha matangazo “live” unakosa nafasi ya kufanya “editing”. Ndicho Chadema hawakutaka. TBC akienda kilirusha matangazo live, asifanye hila. Umeshaona matangazo yanakatika kwa CCM?

Ujinga wa namna hii mnautoa wapi??
 
Shida ya Lissu hasemi yeye kama yeye atafanya mambo gani makubwa, tushajua magu hafai. Sasa yeye aache kila siku kumzungumzia magu badala yake aseme yeye kama yeye atafanya yapi
Dah....mkuu hujaelewa wapi? Mbona kasema wazi kabisa....atarudisha mahusiano na mabeberu ambayo Magufuli kayaharibu....na kuhakikisha kila mtanzania anajua kuongea kiingereza [emoji2960]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lisu anagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Urais wa Tanganyika??

Maana yeye sio muumini wa Muungano.
Matunda ya Miaka 43 ya Utawala wa CCM Maradhi, Ujinga na Umaskini wa kutupwa. Walau wakati wa TANU hawajamaa walikuwa wanakondeana... tangu CCM ifanye Azimio la Zanzibar 1992, kasi ya unono na ukibonge inaongezea maradufu!
 
Back
Top Bottom