Hili liwe fundisho kwa mamlaka, wanapoleta maigizo yao, waangalie wanamuigizia nani, sio kujikurupukia tu, huwezi kumtisha mwanasheria, kwenye jambo linalohusu sheria, kienyeji.
Lissu itakuwa baada ya kupokea ile barua akajiuliza hivi naenda pale kufanya nini? kwani sheria inasemaje? akaona ujinga huu, siendi popote.
Walishaambiwa kuna watu wakuwatisha, lakini kwa Lissu aliyeonja mpaka ladha ya risasi zao zaidi ya kumi na sita, huyu kucheza nae kunahitaji akili ya ziada, wala sio hayo maigizo yao waliyoyazoea kila wakati. Kingai aibu kwake.