Tundu Lissu apuuza wito wa DCI Kingai, asema hatoenda ofisini kwake

Si wamkamate kwani amekataa kukamatwa? yeye anataka ajulishe kosa kama sheria inavyotaka ndiyo aende polisi
kwanini wamkamate? huenda polisi wanzo taarifa za kiintelijensia wanataka kumjulisha na kumtahadharisha kuwa maisha yake yako hatarini awe makini na wanaoumzunguka wanaweza kumdhuru kwani hawana nia njema nae. Kwani hiyo ni mbaya? au unabisha tu kwasababu una hulka ya kubisha
 
Atajulishwa na malaika wa bwana na siyo polisi, Lissu hana imani na polisi alishawahi kutoa taarifa kuwa anafuatiliwa matokeo yake polisi wanaolinda makazi ya viongozi waliondolewa akapigwa risasi kwenye makazi ya viongozi na ulinzi full. Analindwa na MUNGU na ndiye aliyemuokoa na risasi 37
 
Yaani kwa jinsi CCM inavyowanyanyasa Wapinzani ni sawa na akina Madela walivyonyanyaswa na Makaburu!! Tofauti ni kipindi, rangi na nchi....!!
 
Your browser is not able to display this video.

Polisi wa Tanzania ni changamoto au sababu ya entry qualifications zao kuwa ni za chini?

Kwenye ile kesi ya kubumba ya Mbowe tuliona jinsi gani ambavyo polisi hawajui Police Force General Orders (PGO).

Katika video hii ya mwaka 2017 jionee hapo Lissu anavyompa "shule" polisi kilaza asiyejua Criminal Procedure Act (CPA) kwa kutaka kumshikilia mtu bila ya anayeshikiliwa kujua kosa lake .

Nchi ina safari ndefu kwa jinsi polisi inavyotumika kuserve interests za CCM.
 
mambo ya ajabu sana. Yaani wakili tena anajiita msomi anapambana na polisi tu wa kawaida mwenye wajibu tu wakukamata mtuhumiwa eti hadi anampa document aonyeshe ni sheria ipi inampa nguvu ya kukamata. Wakili anaejielewa hababaiki na polisi anenda kumtetea mteja wake mbele ya mwansheria mwenzake au wakili mahakamani. vinjinevyo anataka tu ajulikane au askike kua anajua kubisha na kuongea.
 
Kwahiyo leo hii polisi akija kukukamata hata saa hizi hutomuuliza sababu ya kukukamata?
 
wenyewe wanasema Zipompa-pompa.
 
Binafsi nashukuru zaidi kwa vile hili ni "FUNDISHO" muhimu sana kwa wananchi.

Haya mavitisho mengi wanayotoa hawa polisi na wengine yanalenga hasa kuwatisha raia.
Sasa inapotokea hivi, nasi ambao hatuna ufahamu wa sheria zinasemaje, taratibu tunaanza kujifunza haki zetu, na kuzilinda.
 
Mama endelea kuwachekea hawa uone kama nchi itatawalika. Unaitwa na mamlaka unaleta dharau hiiiiiii.
 
Umeandika TAKATAKA.

Kwamba Dola isifuate sheria?

Dola si ni kikundi cha watu tu tumepitiamo Depo.

Uchawa umekujaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…