Pre GE2025 Tundu Lissu arejea nchini, asema atagombea urais 2025 kuitikia wito wa Watanzania

Pre GE2025 Tundu Lissu arejea nchini, asema atagombea urais 2025 kuitikia wito wa Watanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Amesema "ana nia" yakugombea Urais kupitia Chadema 2025, akiwa na maana endapo kama atapitishwa na vikao vya chama chake.

Hiyo ni tofauti na kusema atagombea Urais kupitia Chadema, hata kama bado vikao vya chama chake kumpitisha mgombea havijakaa.
Tatizo lako nini?
 
Makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Antipas Lisu amesema hana Mpango wa kugombea Uenyekiti wa Chadema

Lisu amesema yeye na Mbowe hawana tofauti zozote ni Waandishi wa Habari wazushi tu ndio wanavumisha Uwongo huu

Baadae Mlale Unono 😀😀
Inaonyesha CCM wanakuwa na kiherehere kingi wakisubiri mtafaruku utokee CHADEMA

Wanayo hofu kubwa sana juu ya Tundu Lissu.
 
Alikwisha toa maono yake kuhusu Katiba Mpya. All in all Samia apewe mauwa yake kwa kuongoza nchi vizuri kwa kuitumia Katiba hii ambayo Magufuli aliisigina.
Sa100 na huyo mwingine uliyemtaja wote ni CCM so mpaka hapo shida iko palepale. Tunahitaji mabadiliko ya hiyari au ya "lazima"

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Wewe una uraia wa ubelgiji , watoto wako raia wa Marekani alafu unakuja kugombea urais Tanzania?

Alafu eti watanzania wakuchague? Watanzania siyo wajinga

Huenda risasi za Mbowe ziliacha uchizi kichwani mwake.
Kwani Mkoa wa Njombe uko Ubelgiji? Maana mimi ni mzaliwa wa Lugarawa wilaya ya Ludewa
 
Wewe una uraia wa ubelgiji , watoto wako raia wa Marekani alafu unakuja kugombea urais Tanzania?

Alafu eti watanzania wakuchague? Watanzania siyo wajinga

Huenda risasi za Mbowe ziliacha uchizi kichwani mwake.
Wewe ndo chizi!
 
..Mama Abduli alizuia Katiba Mpya ili upinzani wasusie, apite bila kupingwa.
Hiyo pekee ni ajenda tosha ya kumshtaki huyo 'Chura Kiziwi' kwa wananchi waone hadaa zilizo wazi toka kwake.. Siku zote utawala wake umekuwa ni kupindisha pindisha tu mambo; hakuna analofanya likiwa kwenye taratibu za kueleweka!
Chukulia mfano mwingine wa DP World na Bandari jinsi Bunge lilivyo vungavunga mambo!
Nchi haiwezi kwenda namna hii.
 
Tundu Lisu ni mpinzani wa kipekee Kabisa hapa Duniani

Hanaga Undumilakuwili
Linalo nishangaza na wewe na kunichanganya juu yako; mara moja moja hujitokeza na kuonyesha dalili za msimamo.
Hapo juu ninakubaliana nawe moja kwa moja.

Uliwahi kumsikia Edward Sokoine, au Mwalimu Nyerere akichanganya changanya mambo kupima upepo? Tundu Lissu yumo kwenye kundi hilo.
 
Hamna kitu hapo, apambanie afya yake kwanza, ila angalau amekulamo, kaenda kuzitunza ubeleji
 
Sasa.. hata kama yeye Huyo tundu la wapi sijui hagombei ndio amwache Huyo Mwenyekiti WA milele kwani hakuna wengine?
 
Angalau na yeye kapata hela, ameacha kelele, wenzake walimruka, mupe-muruke, sasa hivi roho yake kwatu
 
Wewe una uraia wa ubelgiji , watoto wako raia wa Marekani alafu unakuja kugombea urais Tanzania?

Alafu eti watanzania wakuchague?

Huenda risasi za Mbowe ziliacha uchizi kichwani mwake.
Mbowe ana nguvu sana nchi hii, kumbe alimpiga risasi Lissu na akawazuia poliis kufanya uchunguzi!?

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Ila siasa bhana 😂
Uchaguzi dhidi ya JPM alikimbia nchi akisema anatishiwa maisha yake afu akarudi tena kwa ajili ya uchaguzi halafu akaondoka tena ety anatishiwa maisha yake.

Game is on 😎
 
Tangu lini hawa jamaa wakawa na demokrasia wao Huyo ndio mgombea wao WA milele kama ilivyokua kwa Mwenyekiti wao WA milele.
Uchaguzi ujao chama chetu pendwa cha kijani kitachapisha form ngapi vile za Urais ili kudhihirisha namna demokrasia ilivyoshamiri ndani ya chama?

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom