Hakuna cha ajabu. Huo ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ambao hata watangulizi wake walifanya. Hata aliyepo anafanya japo Magufuli aliwadanganya kuwa yeye akitoka madarakani hakina mtu mwingine atajenga mabarabara na madaraja.
Mungu akaona isiwe tabu. Kamsepesha 2021 na Tanzania inakwenda kwa kasi sana. Acha kuabudu marehemu
Nilisha amua niachane nawe kwenye hili, lakini naona ninazidi kuvutwa tu kila ninapokusoma.
Mimi ni kati ya walio chukizwa sana na tabia mbovu za huyo jamaa Magufuli. Nilidiriki kumpa jina la "shetani katika kiwiliwili cha binaadam" kwa matendo yake ya hovyo; na hili nitaendelea kuliamini hivyo kwa kiongozi huyo.
Kwa upande anaosifiwa Magufuli, hata kama katika baadhi ya mambo aliyofanya kulikuwemo na makosa.
Huwezi kamwe kusema Magufuli hakufanya mambo kwa nia ya kuleta faida kwa Tanzania na watu wake kiujumla.
Kama ni swala la mipango ya maendeleo iliyomo kwenye ilani,; lile Bwawa la Mwalimu Nyerere kwa hakika lilihitaji uthubutu kuliweka mbele katika mipango ya utekelezaji. Hili lililkuwa katika mipango hiyo kwa muda mrefu sana, na kila kiongozi aliliona, lakini hakuchukuwa hatua ya kulitekeleza.
Hata maswala ya mali za taifa hili, kama madini, pamoja na kasoro zilizojitokeza katika utekelezaji, lakini uthubutu huo ulihitahi ujasiri wa uongozi na kujiamini.
Sitaki kupitia katika 'laundry list' ya kila kitu; lakini 'theme' nzima ya uongozi wa huyo Magufuli ilikuwa ni kuliwezesha taifa hili, kuwawezesha waTanzania kuwa wanufaika na wahusika wa mali zao za kitaifa.
Tanzania inahitaji zaidi kiongozi anayeweza kuwatia moyo wananchi wake kuhusu uwezo wao wa kujiletea maendeleo kwa kutumia raslimali walizo jaaliwa na Mwenyezi Mungu; watu wanaoamini kuwa ni jukumu lao la kuleta maendeleo yao, na siyo kutegemea maendeleo yaletwe toka nje.
WaTanzania ni lazima wawe ni watu wa kujiamini wanao uwezo; kama hawana watautafuta, kwa sababu raslimali watu tunayo ya kutosha kabisa.
Hatuhitaji kwenda kutafuta watu wa kuja kupanda miti hapa, ili tuwe na misitu ya kutosha; na hatuhitaji watu kuja ku-manage' mapori tuliyo nayo hapa, kazi hiyo haihitaji 'rocket science' kuimudu. Kama hatuna wataalam kwa sasa, hata kukodi 'cosultant' tu waje hapa kwa muda kutufundisha hatuwezi?
Bandarini kuna jambo gani la ajabu sana kwamba hatuwezi kuendesha bandari zetu?Tunanadisha miaka 30, pengine zaidi, kwamba katika muda wote huo, sisi tutakuwa hatuwezi kujifunza kazi hiyo na kuifanya kwa ufanisi?
Unapoona kila kitu tunategemea kuja kufanyiwa, tena kwa gharama kubwa, ubovu unaanzia huko juuu kabisa kwenye ngazi ya urais.
Imenibidi niandike yote haya kukuonyesha mahali ambapo tunapishana sana katika maswala ya uongozi wa nchi hii.
Kwa uongozi wa 'Chra Kiziwi', Tanzania itakuwa ni nchi tegemezi milele. Linganisha hali hiyo na nchi kama Korea Kusini.