..Lissu amefanya mahojiano na watu wengi sana.
..amewahi kuhojiwa na watu wanaomuunga mkono, na wasiomuunga mkono.
..nimewahi kumsikiliza Lissu akihojiwa na vijana wa Ccm ambao kwa ujumla walikuwa wakimuuliza maswali ya kumkejeli na kumcheka.
..Lissu anatakiwa ahojiwe mambo ya kisomi kuhusu future ya Tanzania na sio kuhusu mambo yetu ya kila siku ambayo tayari tuna majibu na misimamo yetu kwa mfano kupigwa risasi, ripoti ya cag, kuachiwa Ole Sabaya, etc
..Kuna Watanzania wachache sana wenye uelewa wa historia, katiba, sheria, na harakati za kutafuta haki, kama Tundu Lissu. Ukimhoji Lissu kuhusu masuala hayo unaweza kupata mambo mapya yenye msaada kwa watakaokufuatilia.