Wapi kweny hivyo vitabu wamesema hivo?
Nitakupa referencw ndogo ndogo visa vifuatavyo.
Kitabu cha Samwel wakwanza na wa pili
Daudi akiwa kijana mdogo alikuwa mpinzani wa Utawala wa Mfaulme Saul.
Saul alijua ktk utawala wake kuna mtoto mtukutu na siku z usoni atakuja kuchukua kiti chake.
Daudi alikuwa kijana mkakamavu, asiye na woga hata mbele ya jeshi la Saul na Wafilisti.
Watu wengi walimshangaa sana Daud ule ujasiri kiasi cha kutokuogopa kufa.
Siku moja Saul akapanga njama za kumuua Daudi. Mtoto wake Saul aitwaje Jonathan akiqa ikulu akazinyaka zile taarifa za Intelijensia akamtonya Daud.
Jonathan alimweleza unapaswa kuondoka Nchini kwani Baba yangu ametangaza kukumaliza na vikosi viko tayari kwa kazi hiyo.
Kwa kuwa ilikuwa usiku akaanza safari akaenda kujificha porini. Jonathan akawa anampelekea chakula kwa kificho.
Hatimaye Daud akafanikiwa kuokoa uhai wake.
Na baadae akawa Mfalme wa Dola ya Israel.
Soma kisa cha Mfalme Yeroboam alivyoakimbilia Misri kujificha baada ya kutaka kuuliwa na Mfalme Suleiman baada ya Suleiman kutambua kuwa Yeroboam anakubalika kwenye tawala yake na anaweza kuchukua ufalme. Ukumbuke Yeroboam alikuwa mtumishi mwenye akili na maarifa mengi akiwa chini ya Suleiman. Suleiman hakufanikiwa hatimaye Unabii wa Abia ukatimia kuwa Yeroboam atakuwa mfalme.
Kisa cha Nabii Daniel kwenye ufalme wa Umedi na uajem wa Mfalme Dario(Darius) na Ashatasta baadae.