Kama upinzani wakitaka mwamko wa maandamano nchi nzima, hapo katoro ndio sehemu ya kuanzia mji mdogo lakini unaamsha sana... Mji uliojaa matukio ya kila namna.
===
Hawa watu sio waongeaji sana japo wanavitendo hatari nakumbuka miaka ya nyuma walishawahi kubomoa kituo cha polisi.. Yaani wanaume wanabomoa na kuchoma magari yale yanayokamatagwa na askari wakati huo askari wanarusha mabomu ya machozi, cha ajabu wanawake walikuwa wanawaletea wanaume maji ya kunawa ili waendelee na uharibifu..chanzo cha vurugu hizi ni kwamba polisi wamemshikilia mama mmoja aliyekuwa anadaiwa mchawi.
=
=
.
Tukumbuke miaka ya nyuma sakata la waislamu na wakirsto kuchinjana kisa walalamikiana suala la kuchinja mifugo machinjioni lilianzia hapo.
Waislamu walichoma bible na wakristo walichoma Quran hadharani.. Tukio lilipelekea mchungaji kuchinjwa na waislamu huku wakristo wakimalizia hasira zao kwa kubomoa maduka ya waislamu.
.
Hapo ni mpakani mwa wilaya ya chato na geita vijijini hapo nyuma ikiwa mpakani mwa kagera na mwanza..
.
Kiufupi katoro ni mji wa kuogopa sana tena sana tu.
.
Way back kwa Mara ya kwanza nilihudhuria mkutano wa chadema 2009 uchaguzi wa marudio Hapo katoro jimboni busanda. ndio Mara ya kwanza nilimuona Tundu Lissu alikuwa kavaa t.shirt ya chadema na kofia zile za miti huku kashika tablet Mkononi.Nakumbuka Finiasi magesa mgombea wa Chadema alishinda lakini akamuuzia ubunge bi Lolensia bukwimba wa CCM.
=
.
Siku moja nitarudi huko.
Msalimie lissu mleta mada mwambie finiasi magesa alitulaza nje kisa kufuatilia matokeo yake.
..
Hongera katoro hongera Lissu.