Uchaguzi 2020 Tundu Lissu (CHADEMA), aomba mdahalo na Dkt. Pombe Magufuli (CCM)

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu (CHADEMA), aomba mdahalo na Dkt. Pombe Magufuli (CCM)

Kuna tofauti kubwa kati mdahalo wa urais na mipasho..... Kama alikua hajui Magufuli ni mtu wa kazi zaidi ya maneno na sasa anafanya kampeni ya kisayansi

Wewe utakuwa ni mwenye ile hotel pale Mwenge.. Si bure.
 
Sisi tunataka kusikia sera na sio mashindano ya midahalo. Kwanza anatakiwa ajue Magufuli anafanya mambo mawili makubwa kwa wakati mmoja kuendesha nchi kama rais na kuendelea na kampeni na mambo yote kaweza kuyamudu vizuri sana. Chadema mwambieni mgombea wenu asimpotezee muda jemedari
 
Sasa kama ni kujinadi kuzunguka si kwatosha?

Na kama ni sera mgombea wa CCM ameishaziongelea?

Na Tundu Lissu nae si bado azunguka?

Sasa midahalo ya ni?

Kwani kinachohofiwa kwenye mdahalo ni nini? Mbona mnahangaika hivi? Mnaelewa hapo kuwa mtu wenu hamuwezi Lissu kwa hoja, sasa mnajaribu kufunikafunika.
 
Huyu mgombea wetu hana adabu kabisa sijui kalelewa na mzazi mmoja? Wanachadema wenzangu nisaidieni kunielewesha juu ya mgombea wetu lissu, kwani mdahalo ndo utampa kura? Akafanye midahalo na Robert Amsterdam,
Mbona mnamficha magufuli kama msukule?
Mwacheni apambane na wanaume wenzie.
Kuongoza nchi sio mashindano ya urembo wala vijembe.
Amepata mshindani kwani alitamba sana miaka mitano akifokafoka na kutukana.
Mleteni hadharani apambane
 
Anatapatapa sasa ameshindwa kuwa win watz! Hatuhitajj mdahalo sisi bali tunataka utuambie umefanya nini na utafanya nini tukikupa kura zetu! Hatuko kwenye mashindano ya mdahalo!

Amefanya nini Kwani amewahi kuwa Rais, ni vema kuwepo na mdahalo ili kuhojiwa namna wanavokusudia kuiongoza hii nchi aliyekuwepo madarakani pia atwambie kama anakusufia kuendeleza ukandamizaji wa haki na uhuru wa wananchi kwa kuendelea kutunga sheria za kutubana au tutegemee nini na huyo a,baye hajawahi kutawala atwambie anataka kufanya kipi tofauti na aliyetawala na mkakati wake ni upi. Mdahalo ndo njia pekee ya kuelewa maono ya kila mgombea.
 


Akiwa mkoani Iringa leo tarehe 13 Septemba, Lissu amesema "Natoa rai kwa Mgombea Urais wa CCM na vyombo vyetu vya habari, kufanikisha mdahalo kuhusu mustakabali wa Taifa letu la Tanzania"

=====

LISSU IRINGA: MDAHALO NA MAGUFULI, MIKOPO ELIMU YA JUU NA HIFADHI YA JAMII KWA WOTE

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mhe. Tundu Lissu ametoa wito kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Mhe. John Magufuli, kuwa tayari kushiriki mdahalo utakaowakutanisha wagombea hao wawili ili waeleze na kuhojiwa kuhusu maono na mipango yao ya namna ya kutekeleza agenda zinazohusu Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watanzania, ikiwa ni sehemu ya wapiga kura kuwapima na kuwajua vyema washindani hao wakubwa katika nafasi ya juu ya uongozi wa nchi.

Mhe. Lissu amesema kuwa ushiriki wa midahalo kwa wagombea urais ni mojawapo ya kipimo muhimu kinachotumika kimataifa kujua uwezo wa wagombea urais na kwa hapa nchini, takriban wiki mbili tangu kuanza kwa mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu, Agosti 26, mwaka huu, haina shaka yoyote kuwa ushindani katika nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uko kati ya Mgombea wa Chadema na Mgombea wa CCM, ambapo amesisitiza wito huo kwa kuviomba vyombo vya habari vikubwa hususan vituo vya luninga, kuandaa mdahalo huo.

“Natoa rai kwa mgombea mwenzangu wa CCM, tukutane kwenye mdahalo. Ufanyike kwa lugha yoyote ile na uendeshwe na wataalam tutakaokubaliana. Ili tuwaeleze na tuhojiwe hadharani na kujibu hadharani mipango na maono yetu. Naamini mwenzagu ambaye ameshakuwa Rais kwa miaka mitano hatakuwa na hofu ya kushindana na mimi ambaye sijawahi kuwa Rais. Tukutane pamoja. Tuache haya mambo ya kuogopana na kuchengana. Nina imani hatakimbia mdahalo. Akiogopa tutahoji majigambo ya usomi wake,” amesema Mhe. Lissu.

Aidha, Mhe. Lissu amesema Serikali atakayoiunda chini ya chama Chadema, itaondoa mara moja masharti ya kibaguzi na utaratibu mbovu wa kisheria unaotumika katika mfumo wa sasa wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ambao umegeuka kuwa adha kubwa kwa wanafunzi na wazazi na badala yake, kanuni pekee itakayosimamia upatikanaji wa mikopo hiyo ni uhitaji wa mhusika.

Akisisitiza hoja hiyo, Mhe. Lissu amesema kuwa mfumo wa urejeshaji riba ya mikopo hiyo unaotumika sasa nao pia uko kinyume na utaratibu wa kisheria uliokuwa mwongozo kwa wanafunzi na wazazi kuingia makubaliano ya kukopeshwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB), ambapo Serikali imeingiza utaratibu mwingine kuwataka wanufaika kulipa riba ya asilimia 15 badala ya asilimia 3 ya awali, akiahidi kuwa Serikali ya Chadema itaufutilia mbali kwa sababu unawafilisi kiuchumi wanufaikaji wa mikopo hiyo.

Akihutubia mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Mji wa Iringa na viunga vyake, uliofanyika leo katika Uwanja wa Mwembetogwa, Mhe. Lissu amesema mfumo unaotumika sasa umewekewa utaratibu ambao unawaumiza na kuwabagua wanafunzi na wazazzi hata wenye uhitaji wa mikopo hiyo ili waweze kujielimisha elimu ya juu kwa kadri ya uwezo wao.

Aidha, Mhe. Lissu akizungumzia umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa watu wote bila kubagua hali wala hadhi ya mtu, amesema kuwa kila mmoja katika wakati usiotarajiwa anaweza kuhitaji msaada wa kuhifadhiwa iwe kwa matibabu, ulemavu usiotarajiwa, umri wa uzeeni, kupoteza ajira au uhitaji wowote ule, hivyo Serikali atakayoiunda, akichaguliwa Oktoba 28, mwaka huu, itaweka utaratibu utakaohakikisha kila Mtanzania anapata hifadhi kadri ya ya mahitaji, ikiwemo bima ya afya, badala ya sasa wanaohudumiwa walioko kwenye ajira rasmi pekee.

“Iringa ni mahali sahihi kabisa kuzungumzia agenda ya hali ya elimu yetu na hususan elimu ya juu. Kuna tatizo katika mfumo wetu wa utoaji elimu nchini. Mtakumbuka wakati ule nilipokuja wakati wa kutafuta udhamini nilizungumza hili. Tunapaswa kuubadili ili uweze kuwapatia watoto wetu maarifa na uwezo wa kufikiria kutatua matatizo yao na kuajiriwa mahali popote duniani. Kwa sababu hilo nililisema wakati ule na mlinielewa, leo nataka nizungumzie hili la elimu ya juu na hususan elimu ya juu, chuo kikuu. Wale wa makamo yangu wanajua kuwa wakati wetu elimu tuliyosoma ililipwa na umma wa Watanzania. Katika zama za CCM wanaita ya kisasa, ili motto wako asome Chuo Kikuu lazima umlipie au akopeshwe na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, mikopo hiyo na utaratibu wa utoaji wake na urejeshaji wake, imegeuka kuwa adha kubwa mno kwa wazazi na wanafunzi wenyewe.

“Kumekuwa na masharti ya kibaguzi katika utoaji wa mikopo ya hiyo. Wanafunzi waliosoma shule za binafsi wamekuwa wakiambiwa hawastahili kupata mikopo. Wanafunzi wengine wengi wameshindwa kuendelea na masomo yao. Serikali ya Chadema, nitakayoiunda mkinichagua Oktoba 28, mwaka huu, itaweka utaratibu unaohakikisha kila mtoto anastahili kupata mkopo bila kujali alisoma wapi. Kanuni pekee itakayotuongoza ni, je anahitaji mkopo? Tutahakikisha pia wanufaikaji wote wanatendewa haki kwa kurejea kwenye sheria ya mwanzo iliyokuwa inaelekeza makato ya riba ya asilimia 3 badala ya sasa ambapo imefanywa kuwa asilimia 15 hali inayowafilisi kiuchumi,” amesema Mhe. Lissu.

Akitumia mkutano huo pia kuomba kura zake na kuwaombea kura wagombea ubunge na udiwani kwa tiketi ya Chadema katika Mkoa wa Iringa, Mhe. Lissu amezungumzia umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa watu wote, ambapo amesema kuwa mfumo uliopo sasa pamoja na kuwatenga watu wengine wasiokuwa kwenye ajira rasmi, pia umeshindwa kuwahudumia hata wahusika baada ya kutumiwa vibaya kwa matumizi yasiyokuwa na tija kwa wachangiaji, ambapo amesema fedha nyingi zimefujwa kiasi cha mifuko hiyo kushindwa kujiendesha na hatimae kufilisika.

Ameongeza kuwa tatizo la hifadhi ya jamii si uwingi au uchache wake, bali ni matumizi mabaya ya rasilimali zake, hivyo ameahidi kuwa Serikali atakayoiunda baada ya kuchaguliwa mwezi Oktoba, itahakikisha utaratibu mpya wa hifadhi ya jamii unawahusisha watu wote kwa ajili ya maendeleo yao na kuhakikisha inaendeshwa katika namna inayozingatia matumizi sahihi yenye tija kwa wahusika ambao watakuwa na uhuru wa kuamua.

“Tunazungumzia mfumo wa hifadhi ya jamii utakaoweza kuwahudumia watu wote, wastaafu wetu, wazee, wasiojiweza, bima ya afya. Tutahakikisha kila asiyejiweza anatunzwa na hifadhi ya jamii. Sisi wote hapa tutazeeka, tunaweza kuwa walemavu, tunaweza kupoteza ajira, tutaugua, tutahitaji kuhifadhiwa. Shida hapa kwetu si wingi wa mifuko, bali mifuko hiyo imefujwa. Walipoifilisi wakaleta masuala ya fao la kujitoa na ile kanuni mpya ya kikotoo, maana mifuko hiyo haina fedha tena,” amesema Mhe. Lissu.

Mhe. Lissu amesema kuwa utekelezaji wa mipango hiyo utahitaji vyanzo vya uhakika vya fedha, ambapo ametaja mapato yatakayotokana na uuzaji wa gesi asilia, ambayo uendelezaji wake ulianza wakati wa Serikali ya awamu ya nne, ulioibainisha Tanzania kuwa mojawapo ya nchi zenye utajiri mkubwa wa rasilimali hiyo, kabla haujatelekezwa katika awamu ya tano, itakuwa ni mojawapo ya vyanzo vya fedha ili kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata elimu ya uhakika na Watanzania wote wanapewa haki ya hifadhi ya jamii.

Mhe. Lissu ametumia mikutano yake mitatu katika maeneo ya Migoli (Isimani), Ifunda (Kalenga) na Iringa mjini, kunadi agenda mbalimbali zilizomo katika Ilani ya Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, inayozungumzia masuala yote katika muktadha wa Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu.

Imetolewa leo, Jumapili, Septemba 13, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano

Naunga mkono mdahalo huu, na kwa nyongeza naomba uendeshwe kwa lugha ya kiingereza ili dunia nzima ielewe.!!!
 
Lengo la mdahalo ni nini?
Kama ni utendaji wote tunajua kwa sasa JPM hana mpinzan

Sisi hatutaki kuchagua Rais wa nchi yetu kwa mazoea tunataka mdahalo tuweze kujuwa tofauti ya maono yao hatutaki kuwa na kiongozi ambaye hatujuwe atatupeleka wapi hii miaka 5 ijayo
 
Mimi ninaongea na kuandika kiingereza vizuri sana kuliko Lissu na Magufuli; ni matokeao ya nature ya kazi yangu ambapo nimekuwa mwalimu Marekani kwa takriban miaka 25 sasa. Je mimi ndiye ninafaa zaidi kuwa rais wa Tanzania? Nimemsikiliza Lissu anpoongea kiingereza jinsi anavyokosea na anatumia tabia ya kuweka pause kwa muda mrefu ili kurekebisha makosa hayo, na nimesikia Magufuli pia anapoongea kiingereza yeye anaongea kwa haraka katika lafudhi ya kisukuma na hivyo kufanya makosa ya matamashi fulani. Kati yao hakuna bingwa.

Binafsi nafikiri Lissu ni mzuri. Ila nafikiri wewe unataka kuwajaza watu ujinga ili waamini Lissu na Magufuli wote hawajui Kiingereza.
 
Hahaha Mdahalo tena? Leo hata Mseven alijua alitoa hotuba kwa lugha tatu, Kizinza, Kiswahili na kiingereza. Nakila alipoongea Kiingereza alisisitiza kutafsiri.
 
Unadhani Urais ni midahalo??

Wenzetu wanafanya midahalo huo urais wa kupewa kificho kwa watu wasio nasifa sasa basi tunaanza na mdahalo wa urahisi halafu na wengine wote watakuwa wanafanyiwa interview katika nafasi kubwa tena zinakuwa wazi kama wanavofanya kenya tusiendelee kuongozwa na watu wasikuwa na uwezo hata wakujieleza matokeo yake kuogopa kwenda kukutana na marais wenzako kwa kisingizio cha kubana matumizi
 
Mimi na wewe ni watu wa kawaida sana.

Hata Tundu Lissu ni mtu wa kawaida sana ukiondoa sifa yake ya ugombea uraisi.

Uchaguzi ukiisha atateremka atatulia.

Tundu Lissu ana kitu chaitwa "personal hatred" kwa JPM na hiyo iko wazi.
Waswahili tunsema kikulacho ki-nguoni mwako. Jamaa hajafungua akili kuangalia kwa kina kujua ni nani aliyetaka kumuua. Yeye anaamini kuwa ni Magufuli tu ndiye aliyetaka kumuua bila kujua kuwa Magufuli kwa position yake kama rais alikuwa na njia nyingi sana za kumhandle. Kibaya ni kwamba, ile kurupuka ya kulaumu serikali ilivuruga sana nguvu za serikali kufuatilia jambo hilo. Tunasahau kuwa miaka ya nyuma kidogo Dr. Mwakyembe naye alikumbana na kadhia ya kufuatiliwa na baadaye kulishwa sumu.
 
Binafsi nafikiri Lissu ni mzuri. Ila nafikiri wewe unataka kuwajaza watu ujinga ili waamini Lissu na Magufuli wote hawajui Kiingereza.
Inawezekana na wewe hujui kiingereza; unaweza kujua kuasiliana kwa kiingereza bila kukijua vizuri kama Lissu na Magufuli walivyo.
 
Waswahili tunsema kikulacho ki-nguoni mwako. Jamaa hajafungua akili kuangalia kwa kina kujua ni nani aliyetka kumuua. Yeye anaamini kuwa ni Magufuli tu ndiye aliyertta kumuua bila kujua kuwa Magufuli kwa position yake kama rais alikuwa na njia nyingi sana za kumhandle. Kibaya ni kwamba, ile kurupuka ya kulaumu serikali ilivuruga sana nguvu za serikali kufuatilia jambo hilo. Tunasahahukuwa miaka ya nyuma kidogo Dr. Mwakyembe naye alikumbana na kadhia ya kufuatiliwa na baadaye kulishwa sumu.
Ikishakuwa serikali ya majungu hayo ndiyo matokeo yake.

Kuna sheria kanuni na taratibu zilizotungwa kutoka kwenye katiba.

Sio kufanya kazi kwa hisia. Hata kama hupendi jambo lakini unabanwa kisheria ni wajibu wako kutekeleza.

Huu upuuzi ndiyo tunausikia eti mkichagua upinzani hampelekewi maendeleo.

Sasa sijui ukishachagua upinzani unakuwa nchi nyingine.
 
Jamani mtasababisha mtu apatwe stroku hivi wewe mtu hawezi kuongea hata sentesi mbili za Kiingereza leo ndio umpe mdahalo ? .
 
Back
Top Bottom