Kama hujakaa nchi za nje bila kazi ya maana hutaelewa! Lissu ni wakusikitikia sana - na ni mjumuishe pia na Lema, hawa watu ni wakuwasikitikia sana. Imagine! Mtu ulikuwa unaitwa mheshimiwa, ukiwa class ya juu nchini mwako, na mshahara mnono na marupurupu mengi, sasa unaitwa mkimbizi (refugee status) Unapewa hela kidogo ya kujikimu ambayo ni kidogo au sawasawa na kiwango cha kima cha chini cha ulipo kimbilia! Hao si watu wa kuwasikitikia! Na Unapopita njiani, hutambuliki na kuheshimiwa na yeyote unatukanwa kwa sababu ya ngozi yako! Hauko sawasawa na wenyeji - ila huzodolewi waziwazi kwa kuogopa sheria lakini jamii inayokuzunguka haikupendi! Je! Bado huwaonei huruma? Na matumizi yao sasa ni ya kima cha chini, siyo watu wa bata tena! Hawawezi kumudu vitu vya anasa kama walivyokuwa navyo! Mfano.: hawezi akamudu mfanyakazi wa ndani, dereva, etc. Hawezi, kwa sababu huko waliko mishahara ya hao wafanyakazi ni mikubwa! - ukitaka kujua ubaya wa kuhama nchi yako, waulize makaburu waliohamia Australia mara Mandela alipo tawazwa South Africa - waliacha wafanyakazi wa nyumbani kama Sita hivi Afica ya Kusini, huko Australia wao wakawa ndio vibarua!
Wasipokuwa makini utasikia Lema ni dreva wa Ubba au ana bodaboda kusambaza KFC! Na Lissu yupo anavuna nyanya Green house au strawberry! Yasiwafike ya kuuza madawa nawaombea hilo Mungu apishe mbali.