Kwani hujui Chadema wakati wakikataa kupokea ruzuku hapakuwepo na maridhiano? wanafiki mnaotaka maridhiano yaguse pote isipokuwa kwenye ruzuku.
Nyie kufanya yale mliyofanya Zanzibar, hakiwezi kuwa kipimo cha nini Chadema wafanye, hamja-set standard yoyote, kwanza hiyo quality hamna, wao watafanya yao, kwa wakati ambao watauona ni sahihi kwao.
Kwangu ni heri Chadema walioonesha kutokubaliana na yale matokeo, wakaukataa ule uchaguzi, kuliko nyie mliokimbilia kujiunga SUK huku mkijua fika, kuna wanachama wenu wengi walioumizwa kule Pemba kwa kufanyiwa matendo haramu, lakini hamkuwahi kuwasemea popote.
Baada ya CCM kuwazoea, sasa wameshawaona wakawaida, juzi mligoma kuteuliwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kule Zanzibar, mkadai mnakuja bara kuwasemea kwa wananchi, ajabu, waumizwe wa visiwani, mkawaulize wa bara!, mpaka leo mpo kimya, hamkuwasemea au ilikuwaje? badala yake bado mpo tu SUK!
Nakwambia ukweli, nyie hamuwezi kujilinganisha na Chadema, badala ya kusema mna vision, na fikra yakinifu, fikra zipi yakinifu wakati mnakaa kimya hamtuambii matokeo ya kile mlichokipeleka kwa wananchi na nini mlijibiwa?
Listen, unatakiwa useme nyie ACT mna viherehere, viherehere hivyo ndivyo viliwapeleka kujiunga na SUK licha ya maumivu waliyopewa wanachama wenu Pemba, na mnaendeleza viherehere hivyo kwa kutoa taarifa rasmi isiyowahusu kwa niaba ya Chadema, mkijua fika mnatafuta political gain, wala hamkumbuki kama hayo ni matokeo ya maridhiano.
Mnafanya siasa za kishamba za kuviziana, claiming mna vision! taarifa ambayo Chadema walijipanga kuitoa kwa wakati wao, nyie mkaidandia haraka, nendeni field mkatafute kuungwa mkono na watanzania, hiki mnachokifanya sasa ni kama fisi anayemsindikiza mwanadamu akitegemea iko siku mkono wa mwanadamu utadondoka, mnajidanganya.