Tundu Lissu: CHADEMA tumeanza kupokea Ruzuku

Tundu Lissu: CHADEMA tumeanza kupokea Ruzuku

Wenzako wanapokea ruzuku za akina Halima Mdee 😂
Maelekezo ya donors kwamba CDM kama chama kikuu cha upinzani nchini kiwezeshwe nchini vinginevyo mtaendelea kukopa Uchina kupitia Exim kama alivyokuwa anafanya mwendazake. EU alikuwa hasubutu kukanyagi.
 
njaa haina baunsa
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Screenshot_20230306-053007.jpg
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Si nilikuwa nakwambia hapa kila siku ukawa unakomaza shingo?

Kiko wapi sasa?

Utakuta sasa kuna mipumbavu inasubiri kina Halima watimuliwe bungeni

Suala la ofisi nisiburi ww uniambie wakati mimi kuna post zaidi ya moja kabla ya 2015, na kuendelea nilisema kuhusu umuhimu wa ofisi yenye hadhi ya CDM?
 
Makamu Mwenyekiti Mh Tundu Lissu akiwa ktk mtandao wa Club house ameweka wazi kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeanza kupokea Ruzuku Mwezi huu uliopita.

Makamu huyo nguli wa sheria na siasa bora Tanzania ametumia nafasi hiyo kuwapongeza watanzania waliokiunga mkono chama hicho kikiwa katika hali ngumu ya kifedha.

"Wanachama wetu na wafuasi waliendelea kufanya kazi za chama bure kabisa bila malipo, na hii inaonesha kuwa Chama chetu ni chama cha watu."

===


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeanza kupokea ruzuku waliogoma kuichukua baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.

Uthibitisho huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu leo Jumapili, Machi 05, 2023 wakati akijibu maswali kwenye hadhara iliyofanyika kwenye mtandao wa Clubhouse.

“Chama (Chadema) kimeanza kupokea ruzuku mwezi huu (Machi) ambayo hatukuichukua tangu ulipofanyika uchaguzi mkuu wa 2020

“Tumepokea sehemu tu ya pesa hizo na kiasi kilichosalia tutapewa siku za usoni. Tumeamua kuichukua kwasababu ya ahadi ya maridhiano yanayoendelea,” alisema Lissu

Hata hivyo mwanasiasa huyo alisema hivi karibuni Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika au Mwenyekiti, Freeman Mbowe atatoa taarifa rasmi.

Chadema iligoma kuchukua ruzuku hiyo inayokadiriwa kuwa ni zaidi ya sh. Milioni 110 baada ya kukataa matokeo ya uchaguzi waliyodai haukuwa uchaguzi bali ulikuwa ni uchafuzi.

Kwenye kauli za chama hicho walisikika wakisema kuwa wanaukataa uchaguzi na mazao yake.

Ikumbukwe chama hicho pia kilikataa kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni kwa sababu ya kutoutambua uchaguzi huo.

Hii ni hatua nyingine ya matunda ya maridhiano yanayoendelea baina ya chama hicho na Serikali.
Chadema njaa imezidi. Sasa walijidai nini kukataa.
 
kadhibitisha kupitia wewe huko club house hahaaaaa uvccm bongolala kabisa 2025 si mtataga kama mapema hivi mmechanganyikiwa.
===
Ni makosa kudhani utaushinda ukuta wa zege la 1:1.5:3(cement:mchanga:kokoto) kwa Ngumi za chembe!
 
Sasa jomba we unazungumzia chama gani..kwa sababu Chadema Wana Mbunge mmoja tu..wale wengine Covid 19 wametemwa zamani ingawa ruzuku yao inaendelea kuchukuliwa... Hahahah..sijaelewa hapa wajameni
Hawa jamaa ni wazee wa kuhalarisha haramu kuwa halali,
Uchaguzi haukuwa halali lakini kwa sasa wanautambua kuwa ni halali.
Usicheze na asali.
 
"Lissu kadhibitisha club house Jana" voicer
Kathibitisha badala kadhibitisha, sasa umefurahi! Pesa zile serikali ilikuwa inataka wazichukue ili watimize lengo lao batili ila Chadema walizikataa, kama sasa wamezichukua hii inatokana na maridhiano na maridhiano si dhambi kwa waungwana na si utashi wa upande mmoja, baada ya maridhiano yaliyopita yamepita huwa hayarejewi.
 
Kwa hiyo uchaguzi wa 2020 ulikuwa halali na wale wabunge wenye kesi nao ni halali.

Sometimes ukitaka kiwaelewa wapinzani inabidi ujitoe ufahamu.
 
Kwa hiyo kwa kukubali kupokea ruzuku wamehalalisha uchafuzi mkuu wa 2020 kuwa uchaguzi mkuu wa 2020?
 
Kwa hiyo uchaguzi wa 2020 ulikuwa halali na wale wabunge wenye kesi nao ni halali.

Sometimes ukitaka kiwaelewa wapinzani inabidi ujitoe ufahamu.
Soma vizuri usijifanye huelewi.

Rais Samia amefuta kesi zote za kubambikiza ambazo 90% zilisababishwa na uchafuzi ule.

Unataka kusema Rais ni mjinga aliyezifuta? Anajua kilichofanyika 2020.

Sasa mtu mzima tena Rais mwenye mamlaka ya juu amelitambua hilo kwa kuweka watanzania pamoja utakuwa ni mpumbavu ukiendelea kugome vitu vidogo tena hela.
 
Hawa jamaa ni wazee wa kuhalarisha haramu kuwa halali,
Uchaguzi haukuwa halali lakini kwa sasa wanautambua kuwa ni halali.
Usicheze na asali.
Sukuma gang tena mtalala na viatu
 
Mbowe mwenyewe akiona hizi coment zako atakucheka kwa dharau sana
Mlidhani tutawaachia pesa??

Kesi zimefutwa na tume haki jinai imeundwa. Mikutano ya siasa inaendelea.

Mtanuna hadi mpasuke.
 
Hapa vijana wa chadema tumesalitiwa sana,, kwanini wakubali kupokea ruzuku wakati hawatambui ubunge wa covid 19?.. 🤔
We chadema tangu lini? Ccm kupokea ruzuku mbona mnaumia sana?
 
Back
Top Bottom