Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu, amesema kuwa chama hicho hakitaruhusu kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 endapo hakutakuwa na mabadiliko ya matukio yatakayolenga kuhakikisha chaguzi huru na za haki nchini.
==
"Kuanzia 2015 hakuna ushindani, hawataki uchaguzi na ukweli wa Mungu ni kwamba sisi (CHADEMA) hatujashindwa uchaguzi na CCM tumeshindwa uchaguzi na Jeshi la Polisi, tumeshinda uchaguzi na Idara ya Usalama wa Taifa, tumeshindwa uchaguzi na mfumo mzima wa Tawala za Mikoa (TAMISEMI), Wakuu wa mikoa, Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi na watumishi wao wote sio CCM"
"Sasa maana yake ni kwamba tatizo letu la msingi ni mfumo wa uchaguzi, huu unaofanya Polisi, Usalama wa Taifa, JWTZ, watumishi wa umma badala ya kusmamia uchaguzi na kutenda haki wanakuwa wao ndio wapambanaji wa uchaguzi huo, na vilevile wanaamua nani anashinda, na tukisema tunaenda hivihivi itatokea tena mwaka ujao (2025), na itatokea tena kwenye uchaguzi wowote utakaofanyika"
"Ni tatizo la mfumo, na jibu la tatizo la mfumo ni 'No Reforms, No Election' (bila mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, hakuna uchaguzi), sio kususia ni kuzuia uchaguzi hiyo ndiyo njia"