Tundu Lissu hana tofauti na Magufuli, anatumia propaganda za serikali ya Magufuli kumchonganisha Samia na wananchi

Kwa akili yako unaamini Mbowe na Zito ni wapinzani?

Na unaamini wakipata madaraka wataondoa uozo uliopo?

Pole sana.

Tatizo lako unaongelea personalities na sio Upinzani Kama movement. Upinzani ulikuwepo tangu enzi za chama kimoja. Tatizo lako unadhani upinzani ni watu akina Lissu au Mbowe unasahau upinzani ni movement.
 
Umenikumbusha wimbo wa CCM ni ileile
 
Lissu hana hoja yoyote zaidi ya porojo,Lissu anafikiri anaweza kuharibu nchi kwa maneno ya ajabu,Ngoja Sultan amgeuke ndio atajua.
 
Usipomtaja mwamba JPM unaona mchango wako wa mawazo hautosomwa au ni kichaa tu kinakusumbua kumuwaza siku zote?

Mpaka ipite karne nzima nyie wezi hamtamsahau JPM aliwang'oa ubishi wenu bila ganzi
 
Haaa haaa bisha kama Samia sio Mzanzibar. Weka ushahidi

kwanini munakwepa hoja? Tatizo sio kuwa ni mzanzibari, tatizo ni kuaminisha matatizo ya serikali yanatokana na sababu ya kuwa yeye ni mzanzibari, Wanatengeneza chuki kubwa kwa wananchi, hivo sio vitu vya kushabikia kabisa. Nchi nyengine ambazo leo zimejaa vita vilianza na chochoko za dizain kama hizi.
 
Wewe ndio mbumbumbu wa mwisho, kuwa kuchagua upinzani ndio guarantee ya kuwa na maisha bora? Maisha bora utayapata kwa kutumia nguvu na akili zako

Kuna watu wangapi Wana akili na nguvu na Wana maisha magumu. Punguza dharau sera na sheria za uwezeshaji ndio zinahitajika. Upinzani unaweza kuleta transformation kwenye mambo mengi. Kenya ya KANU ni tofauti na Kenya upinzani afterwards. Usikariri kuwa CCM ndio wenye Hali mmiliki na nchi.
 
Ulimsikiliza Lissu? Au umelishwa maneno na Nape. Lissu akiongea katika context ya bandari na kumfukuza wamasai.
 
Tatizo lako unadhani upinzani ni watu akina Lissu au Mbowe unasahau upinzani ni movement.
Mkuu una hoja ya msingi kwa context ya nje ya Tanzania...

Upinzani katika nchi yetu ni watu, ndio maana hata nyinyi Chadema mnatamani Mbowe aendelee kuwepo

ACT pale ni Zito kabwe, amejiweka pembeni ila ana nguvu ya kufanya chechote bila kupingwa na yeyote...

Pale Zanzibar kulikuwa na CUF ya Maalim Seif Shalif Hamad, alipohama unajua kilichotokea...

Kwahiyo tukizungumzia upinzani kwa Tanzania hatukwepi kuzungumza watu.
 
Nimeelewa hoja yako. Ila kwa Tanzania bado upinzani ni movement. Sio Mbowe au Zitto. Hata baada ya uhuru upinzani ulikuwepo na umeendelea kuwepo. Shida ni kwamba mfumo wetu wa kiuchumi na uchaguzi umefanya wananchi wasijikite kwenye siasa Sana.
 
Kwani kosa la Lissu liko wapi kama Samia mwenyewe hujitambulisha kwa fahari kabisa kwamba yeye ni Mzanzibari?
 
Wewe ndio mbumbumbu kiwango cha sgr, unashindwa kuelewa serikali inapokua na sera nzuri kwa wananchi wake basi maendeleo yanakuwepo,utaendelea kufanya kazi kwa nguvu na akili hutasonga mbele sababu ya sera mbovu ya serikali famba wewe🚮
Wewe Zezeta unafikiri hawa akina Mdude na Lissu ndio watakutoa? Wangapi wanetoboa kwenye mazingira haya haya unayosema ni mabovu?
 
Kuitambua Tanzania bara ila kukataa kuipatia serikali yake.
Kwahiyo mnataka kuongezeke Idadi ya Serikali na sio kupunguza..gharama za uendeshaji wa Serikali tatu mnazo, mnataka muongezewe Kodi zaidi ili Serikali ziweze kufanya kazi, mpo tayari???...manake msilete ushabiki tu bila kujua athari zake..tafakari
Nadhan. Tunaelekea kwenye Serikali moja ili tuwe tumeunganika zaidi sasa
 
na hiyo ndio ticket ya ushindi kwa chadema, hicho ndicho wananchi walitamani kukisikia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…