Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa Tundu Lissu akizungumza wakati wa mkutano kati ya CHADEMA na Jukwaa la Wahariri (TEF) unaofanyika siku ya Jumapili Machi 2, 2025 Makao Makuu ya CHADEMA, Dar es Salaam
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Sasa shida iko wapi? Kwanini kila tume inayoteuliwa (Ikiwamo Tume ya Jaji Warioba) inasema tufanye mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi? Huu mfumo wa uchaguzi una shida gani hasa? Na hii shida hii ndiyo inayoelezea sababu ya bila mabadiliko hakuna uchaguzi."
"Hiyo shida ndiyo tunayosema isipotatuliwa hakutakuwa na uchaguzi. Mheshimiwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, lugha yangu ilikuwa bayana kabisa, tumesema siyo hatutasusia uchaguzi, tutazuia uchaguzi, lugha siyo kususia uchaguzi lugha ni kuzuia uchaguzi, na tumesema tutazuia uchaguzi kwa nguvu ya umma, tutawaalika Watanzania wahakikishe uchaguzi huu haufanyiki."
"Bila mabadiliko hakuna uchaguzi na siyo bila mabadiliko hatutashiriki uchaguzi, hiyo siyo lugha yetu, lugha yetu ni bila mabadiliko uchaguzi hautafanyika, ndiyo lengo letu. Sasa ni kwanini, hii lugha mbona kali sana, ni kwanini? Mfumo wetu wa uchaguzi una shida gani? na kwanini wazee waliopendekeza ubadilishwe kwanini walipendekeza hivyo? Una shida gani? Shida ya kwanza kabisa, mfumo wetu wa uchaguzi ni mfumo wa Rais, ambao unadhibitiwa kutoka juu mpaka chini ya Rais na mnafahamu Rais wa nchi hii ni Mwenyekiti wa CCM, na Marais wa CCM wametumia udhibiti wao wa mfumo wa uchaguzi kuhakikisha kwamba CCM inabaki madarakani kwa njia zozote, nyingi haramu"