Tundu Lissu hebu tueleze vizuri tukio la kupigwa risasi lilivyotokea haya uliyotoa yanaacha maswali mengi sana

Serikali ina nafasi ya kuyajibu maswali hayo yote, tena kwa vitendo, kwa sababu walitenda uovu huu wanafahamika wazi.

Sasa kama hayo yanajulikana tatizo lipo wapi?

Where is the Disconnect? Kukosa Dhamira?

Nani anayesema Ukweli? Mh. Tundu Lissu au Serikali?
Tumechanganyikiwa Wananchi.


...Je haya yaliyozuliwa katika mada...

'...tueleze vizuri tukio la kupigwa risasi lilivyotokea haya uliyotoa yanaacha maswali mengi sana'

Tufunge mjadala, kwakuwa majibu yapo ila Serikali haina Dhamira?

Unafikiri Tundu Lissu anaafiki na hayo?
 
Utuambie wewe je ?yakuwa maigizo kama unawasiwasi na alicho ongea ipigie kelele serikali iweke uchunguzi huru ili maswali yako yapate ufumbuzi.
Katika suala la lissu inatakiwa ukweli uwekwe huru ili tuyafichue maovu
Mhusika mkuu na shahidi wake wahataki- nani ana hasara- ila hawajali kwa sababu wanapta fursa za kutukana na kuchafua watu
 
Na Wewe unaamini walioshindwa kumuua?
Basi tufuate ujinga wako. Wauaji walifanikiwa kumwua Lisu.

Lakini wenye akili timamu wanafahamu kuwa jaribio la kumwua Lisu lilishindwa, na Lisu bado yupo hai. Lisu alinusurika kifo kwa kudra za mwenyezi Mungu, kwa kuwafanya wauaji kutotambua position ambayo Lisu alikuwepo ndani ya gari. Mkono wa Mungu kwa kupitia dereva aliyemwondoa Lisu eneo alilokuwa amekaa, ulitenda kazi iliyomshangaza muuaji kiasi cha muuaji mwenyewe kifo chake kushuhudiwa na Lisu.

Mumgu hadhihakiwi. Muuaji, washirika wake, na watetezi wa muuaji, wote ni sehemu ya wauaji. Wote watalipwa na Mungu kwa wakati na namna iwafaayo, kwa hekima na mapenzi ya Mungu, sawasawa na ushiriki wao. Na wengine, huenda wamekwushapokea adhabu zao. Wewe na mimi hatuwezi kujua maana utambuzi wetu una kikomo.

Watu wa Mungu, hata kama tuwadhambi, tukakosa ukamilifu mbele za Mungu, kuna mambo kamwe hatustahili kuyagusa, nayo ni DHULUMA, usidhulumu uhai wa mtu, usidhulumu mali ya mtu.

You shall pursue justice, and only justice, so that you may live and take possession of the land which the Lord your God is giving you.”
 

Ndugu SYLLOGIST! hoja yako ni nini hasa?

Nimekusoma mwanzo mwisho sijakuelewa zaidi ya kuona maandishi yanayounda sentensi zilizokusanyika ktk mpangilio usio na mantiki ili mtu asome na kuelewa..

Sana sana nimeambulia neno "NITAKUBUTUA", yaani wewe SYLLOGIST! unibutue mimi Uzima Tele!!!

USHAURI KWAKO: Acha vitisho vya kijuha. Hunijui na wala sikujui. Tujadiliane kilicho kwenye jukwaa. Ukichoka au ukiona unakereka, unatambaa taratibu kuendelea na mambo yako!
 
Yaani kabisa unaamini Wasiojulikana walishindwa kumuua Tundu asiye na Ulinzi wowote

Waulize Watu wa Nyororo au wale akina Kombe!

Usileweshwe Siasa
 
Swala la 4 Ungeuliza wale walinzi pale getini walipotelea wapi siku huyo watu waovu wakaingia na kutoka bila ukaguzi au purukushani yoyote
Unauhakika hawakuwepo? Wameulizwa?
 
Kwa mantiki hiyo, mada inasimama? Ikiwa ina maana na ye Tundu Lissu ana maswali ambayo hajibiwi? kama vile kwanini hawafikishwi mahakamani au wanyongwe hadharani n.k n.k?

Au haisimami...?

Mkuu huoni kwamba mleta mada anamsaidia Mh. Tundu Lissu kupata majibu? au Tukubali tu Hayati alitoa maagizo, makonda akayachukua na kuyafanyia kazi na ushahidi ukapotezwa. Wananchi wakubali hivyo?

Binafsi ninayo maswali mengi tu na moja lapo kuu, ni nani ambae angefaidika na Lissu kufa..? Ila tunajua ameponywa, yaani ni miujiza kapigwa Risasi 16 kapona!

....kabla hujajibu Bamzi tafadhali rejea Post zangu zote katika mada hii Tutaelewana vizuri tu.
 
Watz hatuna desturi ya kuchunguza Mambo but Mimi naamini ukikaa na wakulungwa vizuri watakueleza kila kilichotokea by my side naamini uchunguzi ulishafanywa na wahusika wote wanajulikana ila viko makabatini kulinda maslai
 
we
we unaota au umeandika nini. Awatambue kwani kuna gwaride la utambulisho lililoitwa? Maswali ya hovyo unauliza! Maelezo ya Lissu yalikuwa clear na yaliyojitosheleza usitake kujifanya una akili unahoji upupu. Wana wa Mungu wa mbinguni tunachoshukuru ni kuwa Mungu yupo wakati wote na yuko kazini. Lissu yuko hai ndiyo furaha yetu nyie wachawai, mashetani mtaendelea kuaibika.
 
Utakuwa unaumwa
 
Nani angefaidika na kufa Lisu?

Swali zuri!
 
Mimi nadhani msukumo mkubwa uwe ni kuitaka Serikali ya sasa ichukue hatua. Ile Serikali ya mwanzo isingeweza kwa sababu kimantiki, ni yenyewe ndiyo iliyohusika katika uovu ule.

Kama hii Serikali ya sasa inachukia uovu, basi ichukue hatua. Mpaka sasa haijachukua hatua yoyote. Japo kwa kiasi kikubwa nina imani huenda Serikali hii ya sasa, wakati fulani itachukua hatua. Imani hiyo inajengekea katika uhalisia wa baadhi ya mambo yanayoendelea. Leo Biswalo tayari anatajwa kwa uwazi jinsi alivyoshiriki kupora pesa. Hapo mwanzo, japo ilikuwa inafahamika, haikuwahi hata kutamkwa hadharani. Hivyo, naamini na hili kuna siku kutaagizwa kuanza kwa uchunguzi.
 
Ukweli utakuja kujulikana siku moja. Wangekuja wale wazee wa Forensic Files mara moja tu wangeshachambua mbivu na mbichi - hata kama ni Uchachawangwe ingekuwa ishajulikana.
 
Kwani Serikali ya sasa ni ya Chama gani?
 
Tujadiliane kilicho kwenye jukwaa.
We chagua unayoyaona na kuelewa, ni shauri lako. Wacha na mie nichague yale yanayoletwa kwenye Jukwaa.

Umeniparamia. Ati simwelewi Joka Kuu? Kivipi? Kutokubaliana na hoja zake ni kutomwelewa?



Unataka nikubali kila alisemalo ili iwe vipi. Umekereka wewe unataka kunigeuzia kibao, majibu yako kwangu, yamenidhihirishia umekereka. Katambae mwenyewe kwa kuchutama. Ati Uzima tele.

Usiniletee za Kuleta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…