Tundu Lissu hebu tueleze vizuri tukio la kupigwa risasi lilivyotokea haya uliyotoa yanaacha maswali mengi sana

Tundu Lissu hebu tueleze vizuri tukio la kupigwa risasi lilivyotokea haya uliyotoa yanaacha maswali mengi sana

Kwa wanaoijua CHADEMA inawezekana kabisa ni inside job!
  1. CHADEMA mabingwa wa mapichapicha, walijitahidi kuhakikisha picha za tukio hilonhazisambai kinyume na utamaduni wao!
  2. Risasi kutoboa upande moja wa gari na yeye kuumizwa upande mwingine. Risasi zitoboe kushoto na muathirika aumie mguu wa kulia!
  3. Dereva aliyeko kulia risasi isimpate hata moja!
  4. Zipigwe risasi 38 na atoke kama alivyotoka!
  5. Dereva kuingia mitini na mpkumficha kwa nguvu zote!
Simkubali lissu ila je unataka kuniambia risasi alijipiga mwenyewe? Na kama alijipiga mwenyewe kwanini kamera ziling'olewa si wangeacha tu ili lissu aumbuke? Serikali ilihusika kwenye hili
 
Maelezo ya Lissu alipohojiwa na CLOUDS
Nafasi za parking zimechukuliwa imebaki moja kwa sababu niko mbele nikaingia kwenye hiyo parking. Wakaingia upande wa kushoto wanatafuta eneo la kupaki kuna magari, kulia kuna magari wakageuza gari kuelekea walipotokea dereva akaniambia nisishuke, wakasubiri na wao

Mmoja akatoka siti ya nyuma akaamia mbele upande wa abiria wakazungumza akarudi ndani akafunga mlango ghafla akafungua yeye, akafungua mwingine wanamashine hapo wakaachia" - Lissu

MASWALI
1. Je risasi zilipigwa kutoka nyuma yake?

2. Mbona gari lake lilionekana kuwa risasi zilikuwazimepigwa ubavuni. Kama niko sahihi hii iliwezekana vipi wakati hakukuwa na nafasi ya wao kuegesha gari hapo?

Maana yake ni kuwa nafasi kati ya gari na gari kwenye maegesho isIngeweza kumfanya mpigaji atumie bunduki kwa usahihi mpaka asogee karibu sana na hii ingemfanya amtambue aliyemshambulia.

3. Kwa nini dreva wake kama mtu aliyekuwa kwenye tukio anamzuia asitoe maelezo yake?
Hawa wajinga nilishaacha kufuatilia taarifa zao.

Hakuna kitu cha kipuuzi kukifuatilia kama maisha ya wanasiasa.
 
Kipindi kile kuvaa tshirt za pray for Lissu haikutakiwa. Tukio la ajabu lile. Jambo gani baya lingeipata nchi kwa watu kumuombea TL?
 
Mleta mada ni wazi wewe sio mtaalamu wa kupeleleza jambo hili na maswali unayouliza yanaweza hata yasiulizwe na mtaalamu wa uchunguzi. Jaribu kushughulika na mambo uliyo na uwezo nayo!!

Vijana wa nchi hii tutadharauliwa kwa ujumla wetu kumbe dharau ilipaswa kuelekezwa kwako tu.
vijana mmefundishwa kujadili hoja au kumjadili mtoa hoja?
mbona alichouliza ni cha kawaida kabisa? si ujibu tu kwamba risasi zilipigwa kwa nyuma zikakata kona
 
16538044797770.jpg
 
Je tunaweza kutamka hapa jamvini kwa Uhakika kuwa hayo hayajafuatiliwa na Vyombo husika?

DPP, Wizara ya Sheria,Wizara ya mambo ya Nje n.k can we ascertain that? Where is the Disconnect? nani mkaidi?

Ikiwa na maana hata kuomba akamatwe! sasa tukirudi juu na kuuliza nani mkaidi hapa? Serikali yetu, Polisi wetu, Serikali ya Ubeligiji au Polisi wao. Protokali imevunjika wapi na Kwanini?

Where is the Disconnect?

Ni nani haswa wenye ukaidi. Je katika kabrasha za kuomba viza huko walidai wamekimbia nchi kwa nini? Je ushahidi wa "tulirushiwa risasi" zinatosha kuwapatia visa huko?

Mkuu naelewa fika huna majibu yote, lakini ukweli unabakia pale kwenye Mada. Kuna maswali mengi ambayo yeye TL na Serikali au watu anaowatuhumu/washutumu ndio wenye majibu.

Nafikiri tunaweza afikiana kila pande zinataka majibu/muafaka ile Nchi iendelee, Jamii ziendelee, Familia ziendelee. Hatuwezi kuendelea kwenye chaka la kutupiana vijembe kwa kudai Udhalimu au Makosa yametokea upande mmoja, na cha kusikitisha "yamefanywa na mtu mmoja"....

Mazingira yalijengwa pande zote. Sababu za utetezi kuhusu kwanini mazingira hayo yalitokea in the first place and or....they are open to Speculate...kwa kweli Kuna Ulazimu wa kuyafunika. Ulazimu huo ni Ukweli kupatikana kabla ya 2025 hatuwezi kuwachagua watu ambao bado wana vinyongo na usasi.
Serikali ina nafasi ya kuyajibu maswali hayo yote, tena kwa vitendo, kwa sababu walitenda uovu huu wanafahamika wazi.

Bashite, aliyesimamia zoezi la shambulizi akiwa pale Dodoma hotel, yupo.

Zero aliyetoa maelekezo ya walinzi waondolewe na gari ya washambuliaji ipewe njia ya kutoka kwa kusimamisha magari na bodaboda zote, yupo.

Kalemni, aliyemwelekeza mke wake kuwa awaruhusu watu waliotumwa kuondoa camera, yupo.

Tatizo siyo kuwatambua wahalifu waliohusika kwenye shambulio lile, tatizo Serikali haina dhamira ya kuchukua hatua dhidi ya waovu.
 
Watu wengine mna roho za ajabu sana. Yaani unaona sawa kuchagua muuaji Lakini sio victims wa hao wauaji?

Si waunde Tume yenye watalaam wa nje na ndani na kuchunguza hii issue?
Wauaji, wasimamizi na wapangaji wote wa shambulio lile wanafahamika.

The only problem, the government is not ready to act. Siyo kwamba hawawajui washambuliaji. Kigugumizi chao kipo kwa sababu ya hofu ya yale yatakayoibuka kesi itakapofika mahakamani.
 
Wewe inaonekana hata masikio hayafanyi kazi. Habari hii iliongelewa kwa kirefu, na aliyetoa maelezo marefu zaidi alikuwa ni dereva. Sasa wewe labda una tatizo la kutosikia, au una tatizo la kutokuwa na kumbukumbu, au una tatuzo la unafiki.

Dereva alieleza wazi namna alivyojitahidi kumwokoa Lisu. Alimvuta Lisu toka upande wa kushoto mpaka kwenye upande wa dereva, akamshusha chini ambako huwa inakaa miguu ya dereva, ni sehemu ile ambayo ipo brake na accelerator. Dereva alishuka na kutambaa mpaka chini, akaingia kwenye uvungu wa gari bovu lililokuwepo hapo. Halafu wewe bado unaleta maswali yasiyo na vichwa wala miguu.

Yawezekana uovu unakufanya uwehuke.
Sasa kwanini huyo dereva amejificha?

Au yeye ndiye asiyejulikana?
 
..Lissu amesema risasi zilipigwa " AT AN ANGLE " kuelekea upande wake.

..Hakukuwa na nafasi ya kuegesha gari lakini haimaanishi hakukuwa na nafasi ya washambulia kulenga alipokuwa amekaa Lissu.

..Haiwezekani kumtambua mtu anayekutupia marisasi. Kitendo cha kwanza kitakuwa ni kuepa au kujikinga na risasi hizo.

..Nafasi ya kuwatambua ingekuwa kabla ya kumshambulia, au kama watu hao wangekwenda na kuzungumza na Lissu kabla ya kumshambulia.

..Dereva ameshawahi kuhojiwa na vyombo vya habari. Polisi wanaweza kumhoji wakishirikiana na Polisi wa Ubelgiji.
Hili shambulizi lina Utata kama ajali ya Chacha Wangwe
 
Serikali ina nafasi ya kuyajibu maswali hayo yote, tena kwa vitendo, kwa sababu walitenda uovu huu wanafahamika wazi.

Bashite, aliyesimamia zoezi la shambulizi akiwa pale Dodoma hotel, yupo.

Zero aliyetoa maelekezo ya walinzi waondolewe na gari ya washambuliaji ipewe njia ya kutoka kwa kusimamisha magari na bodaboda zote, yupo.

Kalemni, aliyemwelekeza mke wake kuwa awaruhusu watu waliotumwa kuondoa camera, yupo.

Tatizo siyo kuwatambua wahalifu waliohusika kwenye shambulio lile, tatizo Serikali haina dhamira ya kuchukua hatua dhidi ya waovu.
Serikali gani unayoizungumzia?
 
Kwa kifupi unadai. Case Closed!

Nafikiri utakuwa haumtendei haki T.L ambaye anawezekana ana taarifa nyingi zaidi.Temeke alisema huwa anatembea na kabrasha zenye Taarifa nyingi tu.

Atueleze, let him volunteer the information to the Police.

...na sasa ukimsikia vizuri, toka Temeke na kwingine anapoongea anajikomba kwao!

Ipo siku, tutajua, its just not soon enough!
TL aeleze wapi? Aeleze kwenye vyombo vya habari? Kwa upande wa Serikali, kwa sababu wanajua kila kitu, hawana haja ya kuelezwa kwa sababu wanafahamu kila kitu.

Uliwahi kusikia Serikali kwa kupitia vyombo vyake waliwahi kumhoji Lisu au mtu mwingine yeyote yule kuhusiana na shambulio lile?

Fikiria kuna matukio yanatokea kwenye mazingira magumu ya kuwatambua wahusika, lakini lazima kuna watu kadhaa huwa wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo. Unadhani ni kwa nini kitu kama hicho hakijawahi kufanyika kwa tukio la Lisu? Kwa namna fulani inaleta sense, Serikali imeamua isiwe mnafiki. Inajua waliohusika, inajua tukio lilivyotendeka, na hivyo wanaona hawana haja ya kuuhadaa umma kuwa wanachunguza.
 
..hoja ya kwanini mguu wa kulia umeumia kuliko wa kushoto tumeishaelewana? Is it closed and off the table?

..Kuna taarifa kwamba familia ya Lissu iliandika barua kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kumtaka aombe msaada wa vyombo vya nje visaidie ktk uchunguzi wa tukio la Lissu lakini inasemekana serikali ilikataa.

..Natamani waandishi makini wamuombe Lissu atolee ufafanuzi suala hilo.

..Kuhusu suala la dereva na Lissu kuhojiwa mimi nadhani tatizo liko kwa serikali na jeshi la Polisi.

..Hivi inaingia akilini kwamba blogger JOHN MARWA, na kipindi cha CLOUDS 360, wameweza kumhoji Lissu kwa masaa kadhaa, lakini POLISI wanaodai wanamtafuta kwa miaka 5 sasa hawajaweza kumhoji? Does that make any sense to you?

..Mimi kwa mtizamo wangu Polisi wetu wameonyesha uzembe wa hali ya juu kuhusu tukio hilo. Naweza kusema wameonyesha KUTOKUJALI.

..Naungana na wewe kwamba ni lazima ukweli ujulikane haraka iwezekanavyo, na hususan kabla ya 2025.

..Umesema tusichague watu wenye vinyongo na visasi, mimi nadhani tusichague watu wenye roho za kikatili na wanaoshabikia Watanzania kuumizwa.
Kisasi Ndio Ukatili wenyewe
 
Kwa kifupi unadai. Case Closed!

Nafikiri utakuwa haumtendei haki T.L ambaye anawezekana ana taarifa nyingi zaidi.Temeke alisema huwa anatembea na kabrasha zenye Taarifa nyingi tu.

Atueleze, let him volunteer the information to the Police.

...na sasa ukimsikia vizuri, toka Temeke na kwingine anapoongea anajikomba kwao!

Ipo siku, tutajua, its just not soon enough!
Lazima ajikombe amerudi kufata mafao
 
TL aeleze wapi? Aeleze kwenye vyombo vya habari? Kwa upande wa Serikali, kwa sababu wanajua kila kitu, hawana haja ya kuelezwa kwa sababu wanafahamu kila kitu.

Uliwahi kusikia Serikali kwa kupitia vyombo vyake waliwahi kumhoji Lisu au mtu mwingine yeyote yule kuhusiana na shambulio lile?

Fikiria kuna matukio yanatokea kwenye mazingira magumu ya kuwatambua wahusika, lakini lazima kuna watu kadhaa huwa wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo. Unadhani ni kwa nini kitu kama hicho hakijawahi kufanyika kwa tukio la Lisu? Kwa namna fulani inaleta sense, Serikali imeamua isiwe mnafiki. Inajua waliohusika, inajua tukio lilivyotendeka, na hivyo wanaona hawana haja ya kuuhadaa umma kuwa wanachunguza.
Utachunguzaje bila mashahidi?
 
Maswali yako yote jibu lake ni moja na rahisi sana;

Kwamba, whether it's inside or out of CHADEMA's job, jibu lake ni INTENSIVE INVESTIGATION by Tanzania police force!!

Na wewe kama ni muungwana na ni mtenda haki kweli, hebu majibu maswali haya matatu tu;

1. Unadhani ni kwanini polisi mpaka sasa hawajafanya uchunguzi wa tukio hili?

2. Je, kwa kuwa unadhani ni "CHADEMA's inside job", basi polisi wanagwaya kuichunguza CHADEMA?

3. Na hivi ni kweli kabisa Kwa akili yako ndogo hiyo unaamini CHADEMA wamemficha dereva na Kwa hiyo wanazuia uchunguzi!!??

Kama unaamini hivi, KAPIMWE AKILI ZAKO HIZO!!!
Kwahiyo Dereva kajificha mwenyewe?
 
Maelezo ya Lissu alipohojiwa na CLOUDS
Nafasi za parking zimechukuliwa imebaki moja kwa sababu niko mbele nikaingia kwenye hiyo parking. Wakaingia upande wa kushoto wanatafuta eneo la kupaki kuna magari, kulia kuna magari wakageuza gari kuelekea walipotokea dereva akaniambia nisishuke, wakasubiri na wao

Mmoja akatoka siti ya nyuma akaamia mbele upande wa abiria wakazungumza akarudi ndani akafunga mlango ghafla akafungua yeye, akafungua mwingine wanamashine hapo wakaachia" - Lissu

MASWALI
1. Je risasi zilipigwa kutoka nyuma yake?

2. Mbona gari lake lilionekana kuwa risasi zilikuwazimepigwa ubavuni. Kama niko sahihi hii iliwezekana vipi wakati hakukuwa na nafasi ya wao kuegesha gari hapo?

Maana yake ni kuwa nafasi kati ya gari na gari kwenye maegesho isIngeweza kumfanya mpigaji atumie bunduki kwa usahihi mpaka asogee karibu sana na hii ingemfanya amtambue aliyemshambulia.

3. Kwa nini dreva wake kama mtu aliyekuwa kwenye tukio anamzuia asitoe maelezo yake?
Eti tufanye alijipiga....au ametunga....story hahagah saw watu wabaya
 
Back
Top Bottom