SYLLOGIST!
JF-Expert Member
- Dec 28, 2007
- 8,189
- 7,853
Nimekupata.Mimi nadhani msukumo mkubwa uwe ni kuitaka Serikali ya sasa ichukue hatua. Ile Serikali ya mwanzo isingeweza kwa sababu kimantiki, ni yenyewe ndiyo iliyohusika katika uovu ule.
Kama hii Serikali ya sasa inachukia uovu, basi ichukue hatua. Mpaka sasa haijachukua hatua yoyote. Japo kwa kiasi kikubwa nina imani huenda Serikali hii ya sasa, wakati fulani itachukua hatua. Imani hiyo inajengekea katika uhalisia wa baadhi ya mambo yanayoendelea. Leo Biswalo tayari anatajwa kwa uwazi jinsi alivyoshiriki kupora pesa. Hapo mwanzo, japo ilikuwa inafahamika, haikuwahi hata kutamkwa hadharani. Hivyo, naamini na hili kuna siku kutaagizwa kuanza kwa uchunguzi.
Niseme tu, Sitakubaliana na uanzishwaji wa Tume. Sidhani kama nitapenda kuona hadaa nyingine....ni maoni yangu.
Inaonekana una taarifa nyingi na Nyeti, au kwa lugha nyingine ni kuwa Ushahidi wa kutosha upo. Kwanini Mh. Tundu Lissu asiwafungulie Polisi au Serikali kesi na kudai amenyimwa haki...au hilo nalo linahitaji Katiba mpya?