Uchaguzi 2020 Tundu Lissu, huku ni kutafuta wadhamini au ni kampeni?

Tundu Lissu ni mwanasheria na ameshaichambua hio sentesi ya kusema ni kampeni. Kampeni bado hazijaanza unawewaje kusema ni kusema ni kampeni? Labda hawajui tofauti ya Kampeni na kutafuta wadhamini.
Wadhamini wanatafutwa kwenye mikutano ya hadhara tena yenye ahadi kem kem za muomba kugombea?

Akikatwa msijilaumu. Najiandaa kumuwekea pingamizi.
 
Embu tuambie kampeni ni nini? Alafu tupime kama CCM hamjafanya kampeni kwa miaka yote mitano na bado hamjiamini.
Mimi nashauri tu kwamba huyu jamaa hata kama amefanya makosa kuanza kampeni kable ya muda aachwe tu ataleta matatizo tu kwanza akilizake hazijaenea mara aseme yeye ana damu ya kenya mara ya Ubelgiji basi tu yupo yupo tu.
 
Acha kututia aibu CCM wewe.. Sisi hatumuogopi huyo Tundu Lissu. Na hatakatwa ili tumuabishe siku ya uchaguzi. Hakuna kitu kinaitwa kampeni kabla ya muda. Mikutano ya hadhara sio kampeni.
 
Daaah pamoja na nyinyiemu kufanya kampeni kwa miaka mitano peke yakeee bado mnalalamika duuuh.
 
Hujui sheria wewe.Ataonekana amekiuka sheria pale ambapo NEC imemtangaza rasmi kuwa mgombea wa kiti cha Uraisi na yeye akaaza on the spot kupiga kampeni bila idhini ya NEC na hilo liendane sambamba na yeye binafsi kurudisha ile form NEC na kutangazwa kuwa ana sifa.Kwasasa kila mgombea ni ruksa kukusanya watu na kuwaomba udhamini huku akiwa convince wamdhamini bila kuvunja sheria.Hapa tuna angalia sheria siyo hisia zako binafsi ! upo hapo nyonyo wa Lumumba
 
Tena afadhali yeye anatoa elimu ya uraia kwa wananchi. Elimu ambayo imeachwa kutolewa si katika masomo ya shule za msingi na sekondari tu, bali pia hata vyuo vikuu vimegeuzwa kuwa viwanda vya kuzalisha makondoo, yaani vijana wasiofikiri kuhoji au kujenga fikira mbadala za kutatua matatizo ya kijamii. Wanaimbishwa wimbo wa hapa kazi tu. Baada ya miaka mitano ya hapa kazi tu tuna madege ya ATCL (ambayo huwezi kuambiwa faida yake) wakati shule za msingi na sekondari hapo Mkuranga (km 50 kutoka Dar) watoto wa 'wanyonge wa magufuli' wanakalia mawe na ndoo darasani!. Acha atoe elimu ya uraia, hata akikatwa atakuwa ametoa mchango mkubwa kuelekea ukombozi wa taifa hili.
 
kwa sehemu kubwa ni reflection ya lack of self-confidence; kwa hiyo anaona ngoja aanze mapema kujitambulisha kwa sababu wenzie wakianza kishindo chao hatakuwa na ubavu wa kukabiliana nao.
 
Go work on your prepositions, idiot. Andika kwa lugha unayoielewa vizuri.
 
Lissu sasa ameanza kuona thamani ya polisi wetu, anaona jinsi wanamlinda..!! Nategemea ataonyesha hiyo heshima na kuendelea.. Kudos to our Police Officers
 
Hapo hakuna kampeni yoyote iliyofanyika maana huwezi kufanya kampeni kabla hujapitishwa n Nec.
 
KwahiyoJiwe amefanya kampeni miaka 5? Jibu hili kwanza then tuendelee
 
Mie sisikilizi media za bongo saivi. Wote saivi ni kuwapigia kampeni CCM tu wakati kuna vyombo vya Habari vimefungiwa, waandishi wananyanyaswa, watu kutekwa hovyo, kupigwa risasi na kubambikiwa makesi
 
Lissu sasa ameanza kuona thamani ya polisi wetu, anaona jinsi wanamlinda..!! Nategemea ataonyesha hiyo heshima na kuendelea.. Kudos to our Police Officers
Hakuna siyejua thamani ya polisi, ila kwa siasa za Jiwe polisi force/service imekengeuka! TRA hakuna asiyejua thamani yake, ila kwa siasa za Jiwe, TRA imekengeuka , hakuna siyejua thamani ya mahakama, ila kwa siasa za Jiwe, Mahakama imekengeuka, hakuna siyejua thamani ya Bunge, ila kwa siasa za Jiwe, Bunge limekengeuka etc etc etc
 
Ubarikiwe sana
 
Hapo sawa

Kejuu,
Hapo sawa, hajamtukana Magufuli Wala hajasema maneno ya uongo, hajabeba marungu na Bondo kutumia jeshi la Police ndivyo tunataka.
Tatizo la ccm siku hizi sio wale vichwa wa zamani waliokuwa wanajibu hoja. ccm ya siku hizi ni propaganda na kutokujiamini tu. wanakimbia kimbia tu bila mipangilio na mwaka huu huyu jamaa anayeitwa Lissu kawanasa kweli kweli kitanzini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…