Tundu Lissu, kabla ya kufuta Idara ya Maelezo, futa Idara ya Habari na Uenezi ya CHADEMA

Tundu Lissu, kabla ya kufuta Idara ya Maelezo, futa Idara ya Habari na Uenezi ya CHADEMA

Hili tatizo limelalamikiwa sana but tujiulize vyema

Unafikir wanapenda haya?? No rahisi sana kuongea ukiwa nje ila humo ndani hali ni tofauti sana.
No democracy in chama cha demokrasia na maendeleo.
 
Kwakweli ,ngoja mpaka kesho jion km alivyosema mkuu Lissu.

Baada ya hapo hii idara haipaswi kuwepo kama hawatafanya mabadiliko.

Haiwezekani chama kichanga km ACT Kiwe makini kihabari kushinda CDM.
Wanawalaumu tu bure kama kitengo hakipewi resilimali fedha unategemea miujiza ya nini
 
Sina shaka kuwa Mbowe kakipambania sana hiki chama, ila kwa sasa kafika mwisho. Na hiyo ni hali ya kawaida kuwa binadamu hufikia mwisho. Wakati ukuta.
Tatizo kawa mwenyekiti wa kudumu. Ame expire sasa.
Chadema mnataka viongozi wanaojua kupayuka na siyo kujenga hoja kwa utulivu.
Mbowe kwa sasa amekomaa kifikra, anajenga hoja badala ya kupayuka ndo maana mnamwona kama hafai. Bila mbowe chadema itakufa kesho asubuhi. Jaribuni muone. Wajumbe wamewauza wanachama. Lisu hafai kubeba maono ya chama. Nyalandu ndiye aliefaa.
 
Kichwa cha habari chahusika.

Idara ya habari ya CHADEMA ina matatizo mengi, nikianza kuyataja yote tutajaza ukurasa huu.

Kuna tatizo la kutotoa habari kwa wakati.

Pia wanatoa habari zikiwa zimekatwa-katwa.

Zaidi hawamuandai mgombea kwa maswali anayoulizwa na waandishi wa habari.

In short, these people need to wake up. Wanakiangusha chama na wanamuangusha mgombea Urais.

Hapo sio kufuta bali kuboresha ,habari maelezo ya serikali inaminya waTZ kupata habari kwa mizania sawa.
 
Makene ana kinyongo baada ya kupata habari za kutafuniwa
Wekeni majungu na mizaha pembeni. Huu siyo wakati wala sehemu yake. Hoja hapa nikuimarisha chama. Siyo vema kurushiana madongo wala lawama kwa wakati huu.

Chadema ni mali ya Wanachama wote na si ya Viongozi. Hivyo basi mshikamano na Viongozi wetu ni muhimu sana kipindi kuliko wakati mwingine wowote. Kila mmoja wetu ajaribu kufikiri ni nini atakifanyia chama chetu kutoka hapa tulipo na si kukisubiri chama kimfanyie nn.

Suala la Habari ni muhimu sana kupatikana kwa wakati lkn siyo kila kitu ni habari vingine ni tetesi tu.

Kuhusu Viongozi wetu kuwa kimya mimi binafsi sina uhakika hasa kuna nn lkn kila mmoja wetu anafahamu hali ya siasa ilivyo Nchini mwetu. Wasipokuwa makini hasa kipindi hiki watajikuta wana kesi za UCHOCHEZI. Au kukusanyika bila vibali.

Mimi niwashauri Wanachadema wenzangu safari bado ni ndefu. Tuwapende Tuwaheshimu na Kuwaombea Dua Viongozi wetu tufike huko tunakoelekea tukiwa wamoja na wenye afya njema.
 
Sina shaka kuwa Mbowe kakipambania sana hiki chama, ila kwa sasa kafika mwisho. Na hiyo ni hali ya kawaida kuwa binadamu hufikia mwisho. Wakati ukuta.
Hili jambo linahitaji twende taratibu tutagawanyika, hapa tu ziko dalili za mgawanyiko ndani yetu
 
Ukiiangalia chadema ya baada ya 2015 unagundua kuna kitu Slaa aliondoka nacho.. Jishusheni mtafuteni awashauri
 
JokaKuu Nyani Ngabu tindo

Kwa miaka 2 nimekuwa 'adui' wa wanachadema kwasababu ya kuwaambia ukweli.
1. Nilisema kuhusu Mwenyekiti kuchoka na walipaswa kufanya mabadiliko. Tukaona kundi la Mwamba tuvushe

2. Hawa Mwamba tuvushe ni watu wa 'mbinu local'' I mean ndani ya Chadema na si zaidi ya hapo

3. Nilizungumzia uzembe wa media na mawasiliano duni sana

4. Nilizungumzia kuhusu maandalizi ya uchaguzi. Kwamba lazima wawe na wanasheria kila mkoa kuhakikisha hakuna hujuma za Wakurugenzi kwa namna yoyote. Leo uchaguzi wa 5 Mbowe akiwa na chama bado watu wanaenguliwa.

Kwangu kila kinachotokea ni kutimia tu kwa kile nilichowahi kusema tena kwa gharama !
 
Kichwa cha habari chahusika.

Idara ya habari ya CHADEMA ina matatizo mengi, nikianza kuyataja yote tutajaza ukurasa huu.

Kuna tatizo la kutotoa habari kwa wakati.

Pia wanatoa habari zikiwa zimekatwa-katwa.

Zaidi hawamuandai mgombea kwa maswali anayoulizwa na waandishi wa habari.

In short, these people need to wake up. Wanakiangusha chama na wanamuangusha mgombea Urais.
vipi idara ya habari za TBC na LUMUMBA ambayo hata kutoa habari hawatoi? wao si waambie si watanzania kabisa?
 
Tatizo kawa mwenyekiti wa kudumu. Ame expire sasa.
Chadema mnataka viongozi wanaojua kupayuka na siyo kujenga hoja kwa utulivu.
Mbowe kwa sasa amekomaa kifikra, anajenga hoja badala ya kupayuka ndo maana mnamwona kama hafai. Bila mbowe chadema itakufa kesho asubuhi. Jaribuni muone. Wajumbe wamewauza wanachama. Lisu hafai kubeba maono ya chama. Nyalandu ndiye aliefaa.

Nyalandu sio mwanacdm bali ni ccm.
 
Kwa kweli, Mwenyekiti Mbowe amepoa sana, Katibu Mkuu ndio amelala kabisa usingizi, Idara ya Habari Kimnya na habari wanazotoa ni vipande vipande tu kama tetesi hazina maelezo na way forward. Yaani wanaripoti kama uzishi tu wala hakuna muelekeo wanachukua hatua gani.
Kwa kiasi fulani unachosema ni sahihi. Media ya chama kikuu cha upinzani ni lazima ioneshe weledi wa juu kuanzia kukusanya habari, uchambuzi, reporting na hata kuwaandaa watu wake ku-deliver special remarks
 
Kichwa cha habari chahusika.

Idara ya habari ya CHADEMA ina matatizo mengi, nikianza kuyataja yote tutajaza ukurasa huu.

Kuna tatizo la kutotoa habari kwa wakati.

Pia wanatoa habari zikiwa zimekatwa-katwa.

Zaidi hawamuandai mgombea kwa maswali anayoulizwa na waandishi wa habari.

In short, these people need to wake up. Wanakiangusha chama na wanamuangusha mgombea Urais.
Concur with you.
Hiyo idara ni hopeless kabisa. Hivi nani kiongozi wake?
Wakati vyombo vingine vya habari, hasa main stream media vikiwa vimeufyata na kulamba miguu ya wanalumumba, ilikuwa fursa ya dhahabu kwa chombo cha chadema kutupa habari za upande wa pili.
 
Tutahakikisha idara ya habari inang'olewa yote , ni wapuuzi sana na wako kama konokono , hatutaki ujinga kabisa , mleta uzi ni kama amechokoza nyuki , na kwa kweli kama kuanzia kesho hawajang''olewa patachimbika , sasa baaaasi !

Baadhi wananifahamu lakini Liwalo na liwe , hatutafuga ujinga
......Naunga Mkono Hoja Mkuu kuna hili bango nimelitengeza sijuwi wameliona
1598441730848.jpeg
 
..kwa maoni yangu Tumaini Makene siyo mtu wa media.

..anatakiwa apewe msaidizi mwenye weledi ktk masuala ya media/ public relations.

..Tumaini abakie kuwa Chief of Staff pale makao makuu.

..huu sio muda wa kufukuzana, kuna miezi 2 tu ya kufanya kampeni.
 
Honestly tbc wanatangaZa wanakuja kuwafanyia coverage mlitarajia fairplay? yaani Lissu aelezee jinsi jamaa alivyoagiza apigwe risasi kwamba ni msaliti anawasiliana nma Mwanyika ambaye naye ni mgombea ubunge huko CCM ingawa naye inasemekana ni kibaraka wa mabeberu?

TBC wametumia picha za asubuhi saa 5 tena za drone wakapost kwamba ndio mafuriko na ndio zinatumika mitandaoni,for the first time leo CHADEMA inahangaika kujitetea kuhusu crowd unadhani TBC hawajui kwamba kulikuwa na crowd kubwa?

Jamani nyie CHADEMA MEDIA hivi makene analipwa mshahara? Kuna social media team?

Mbowe, Lissu ana maumivu ya kutisha na mzigio mkubwa mabegani kwake unashindwa ku-organise hata team ya kueleweka ya social media?
Wewe kweli uli recruit katambi na Mashinji ?

Leo msaidie basi hata Lissu kumtafutia drone ya kupiga picha juuu basi kama umekosa drone ya milioni 2 basi tafuta wapiga picha watakaonenda kuomba vibaraza vya watu na kupanda juu ya miti,sijui kama umenielewa?

Walioenda juzi TCRA kuhusu drone,msawali ilkuwa unatumia drone kwa ajili gani? Sema unachotaka wewe usiseme mkutano hupewi kibali ndiyo maana TBC leo wametupia picha ya juu inawadhalilisha, mkoje lakini jamani?

Kuanzia mkutano ujao mikutano yenu yote pigeni picha na drone leo mtajitetea na mapicha hadi itakuwa ujinga next time so on iwe drone pics na updates za kufa mtu acheni ujinga
 
Back
Top Bottom