THE BIG SHOW
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 18,873
- 15,267
Mbowe aliibadilisha KATIBA ya mwenyekiti kuhudumu VIPINDI VIWILI TU....leo ana miaka 17 madarakani....umri wa mtoto kumaliza KIDATO CHA 4 🤣🤣🤣🤣
Msimamo wa lissu ni upi?"Kama msimamo wa Samia Suluhu Hassan ndio huu aliousema juzi, maana yake ni kwamba tujiandae kwa mapambano makali na magumu mbeleni. Huyu mama ni Magufuli wa kike, kwa hii kauli yake kuhusiana na haki za vyama vya siasa na katiba mpya ni anataka kuendeleza Umagufuli bila Magufuli mwenyewe kuwepo, anataka kuendeleza Magufulism without magufuli. Tujiandae na mapambano makali na magumu mbeleni"- Tundu Antipas Lissu
Pia soma > Lissu: Samia Suluhu Hassan has finally revealed her true colors
CCM haiwezi kuondoka madarakani bila ya watu kuchinjana..that's for sure..yaani ni lazima watu wakichafue mbaya mbovu.
Shida ni kuwa upinzani nao umepoteza dira..upoupo tu,wanadandia hili wanaliacha wanaenda na lingine bila lolote kukamilika.
Mfano,ishu ya wale wabunge 18 inatosha kuonyesha ni kwa kiasi gani wapinzani wanafeli.
"Vyama vya Saccos hivyo"Umeona sasa,af then akuja kuhubir demokrasia na utawala wa haki na kufuata katiba,yeye mwenyewe mbona haonesh mfano??
Waganga Njaa tuh hawa wapinzan
Mimi huwa nashangaa sana watu wanaomtuhumu Lissu kuwa ni mwanasheria nguli, siyo kweli, wewe angalia kesi nyingi alizosimamia alishindwa hata ile ya ubunge wake na kuzuia uchaguzi usifanyike. Mwanasheria nguli alikuwa ni Dr Masumbuko Lamwai bwana. Hao CHADEMA nao ni Kenge kweli, sasa Lissu alikwashakimbia nchi kwa sababu za kijinga na bado wanamkumbatia.TL inawezekana anaijua sana sheria kama taaluma yake lakini kwenye kitu kinachoitwa uzoefu wa mambo na uongozi sifuri kabisa....anaonekana ana uelewa mdogo sana wa mambo nje ya taaluma aliyosomea ndio maana kwenye kampeni alikuwa anaongea matango pori mengi sana, alikuwa akimeza mazima mazima kifupi hana tofauti sana na Dr Slaa japo Dr kamzidi kidogo uelewa.....
Naamini huyu hakuwa mgombea chagua la Mbowe na naamini bado Mbowe hamkubali TL hata kidogo ndio vile tu naye anaogopa siasa za oyaoya...
Kuongea tuh ni jambo rahis Sana,
Wangekuwa hao chadema wangefanya hivyo?
Urais ni Taasisi,hawez kufanya maamuz SAMIA pekeyake bila kuhusisha baraka za chama chake,mnataka awe dikteta??
Mbowe mwenyew ana miaka 17 hapo hatak kuachia kiti Cha uenyekiti, angekuwa kwenye power hiyo hata yeye asingeweza fanya hivyo tusiongopeane hapa,
Suala la katiba ni mchakato,hatuwez liendea kwa pressure za chadema
Tumeshawasilisha mihoja uchwara unazotaka wewe kusikia hadi tumechoka. Sasa tumesema baas liwalo na liwe. Mama tutamsamehe.Hanaga staha huyu....
Magufuli wa kike!! Haijakaa vizuri, kulikuwa na njia nyingi za kuwasilisha hoja.
Mimi huwa nashangaa sana watu wanaomtuhumu Lissu kuwa ni mwanasheria nguli, siyo kweli, wewe angalia kesi nyingi alizosimamia alishindwa hata ile ya ubunge wake na kuzuia uchaguzi usifanyike. Mwanasheria nguli alikuwa ni Dr Masumbuko Lamwai bwana.....
Hiyo ya katiba mbona hata JK hakulimaliza? katiba hiyo ni nzuri kwa kila mwenye nafasi ya kuwa mtawala. Raisi wa sasa ataweka nia ya kuibadili iwapo tu hatakuwa na nia ya kugombea uraisi, vinginevyo haiwezekani!!! Hata wewe ukiwa rais kwa bahati mbaya huwezi kubadili tuwe wa-kweli!!!!..kama ni uongo basi Rais Samia Suluhu atuonyeshe kwa VITENDO.
1. Aivunje tume ya uchaguzi na kuanza mchakato wa kuunda tume mpya na huru.
2. Sheria ya vyama vya siasa iandikwe upya ili itoe haki sawa kwa vyama vyote.
3. Vyama vya siasa viruhusiwe kufanya shughuli zao bila kuingiliwa na kubugudhiwa na dola.
..Rais Samia akirekebisha hayo basi atakuwa amethibitisha kwamba yeye siyo " magufuli wa kike. "
YU wapi sasa? aje tujenge kwa pamoja,..ameshindwa kesi baada ya mahakama kuvamiwa na genge la magufuli.
..wakati mahakama ikiwa huru alikuwa anashinda kesi nyingi zikiwemo za wachimbaji wadogo-wadogo wa tarime.
..Lissu aliwatoa gerezani na mahabusu wachimbaji wadogo zaidi ya 300 waliokuwa na tuhuma, kesi, na hukumu mbalimbali.
..Na kesi zote hizo ni kesi chafu-chafu ambazo mawakili wanaopenda mapesa hawataki kuzitetea.
..Lissu ndiye wakili wa wanyonge wa nchi hii. Mtetezi wa wasio na sauti nchi hii.
..Uko sahihi 100% kuwa katiba mpya ni mchakato.
..Lakini kwa sasa hivi lazima watu, wanaharakati, vyama vya siasa, viseme-seme ktk makongamano, na mikutano ya hadhara, ili wananchi wawe na uelewa.
..Lakini pia kuna mambo kama kuunda TUME HURU YA UCHAGUZI ambayo yanaweza kufanyika bila kuchelewa.
..Uko sahihi 100% kuwa katiba mpya ni mchakato.
..Lakini kwa sasa hivi lazima watu, wanaharakati, vyama vya siasa, viseme-seme ktk makongamano, na mikutano ya hadhara, ili wananchi wawe na uelewa.
..Lakini pia kuna mambo kama kuunda TUME HURU YA UCHAGUZI ambayo yanaweza kufanyika bila kuchelewa.
Huyo madawa yamemchanganya kichwa msamehe bure.Hanaga staha huyu....
Magufuli wa kike!! Haijakaa vizuri, kulikuwa na njia nyingi za kuwasilisha hoja.
Unaujua mtutu wewe?Tanzania hii tukitaka tusonge mbele kiuchumi na kidemokrasia dawa ni kuiondoshea mbali ccm. Ikishindikana kwenye ballot box basi hata kwa mtutu.
Kimenuka !! Tulionya tukapuuzwa ."Kama msimamo wa Samia Suluhu Hassan ndio huu aliousema juzi, maana yake ni kwamba tujiandae kwa mapambano makali na magumu mbeleni. Huyu mama ni Magufuli wa kike, kwa hii kauli yake kuhusiana na haki za vyama vya siasa na katiba mpya ni anataka kuendeleza Umagufuli bila Magufuli mwenyewe kuwepo, anataka kuendeleza Magufulism without magufuli. Tujiandae na mapambano makali na magumu mbeleni"- Tundu Antipas Lissu
Pia soma > Lissu: Samia Suluhu Hassan has finally revealed her true colors
Hiyo ya katiba mbona hata JK hakulimaliza? katiba hiyo ni nzuri kwa kila mwenye nafasi ya kuwa mtawala. Raisi wa sasa ataweka nia ya kuibadili iwapo tu hatakuwa na nia ya kugombea uraisi, vinginevyo haiwezekani!!! Hata wewe ukiwa rais kwa bahati mbaya huwezi kubadili tuwe wa-kweli!!!!
Jukumu la kuunda tume huru ya uchaguz ni la mama samia??
Mbowe angekuwa kwenye position kama ya mama SAMIA angeweza kuunda tume huru ya uchaguz??
Na angeweza vip Ili hali hata hiyo nafas ya uenyekiti wa chama chake kakomaa nayo miaka zaid ya 17 kwa sasa??
Tatizo haish maneno anayoyasema,kitu ambacho kinatuaminisha sisi kuwa hawa ni political entrepreneurs tuh...