Tundu Lissu: Kama msimamo wa Rais Samia ndio huu, tujiandae kwa mapambano makali na magumu mbeleni

Tundu Lissu: Kama msimamo wa Rais Samia ndio huu, tujiandae kwa mapambano makali na magumu mbeleni

Mwacheni mama yetu,ww lisu kua na lugha za staha kwa amiri jeshi mkuu,
 
Nguvu ya umma ikiamua, hamna cha kufanya! Mtakuwa wa kwanza kuikimbia nchi kama yule kunguru mwenzenu wa Eswatini, aliyewekeza kwenye kudinya tu wanawake, huku wananchi wake walio wengi wakiendelea kuishi katika dimbwi la umaskini na maradhi!
Unaposema nguvu ya umma na kuelewa na nakuunga mkono. Lakini, nguvu ya Chadema? Tutawapiga hadi Ubeleji lipojificha Lissu na Canada anapodemkia Lema. Mark my word!!!!!!!!!!?
 
Unaweza kuwa na hoja nzuri, ila lugha unayotumia ikakuongusha sana kuufikisha ujumbe wako.....hata kama hukubalini na mtu kimtazamo, ni vema kutumia busara
 
Tanzania hii tukitaka tusonge mbele kiuchumi na kidemokrasia dawa ni kuiondoshea mbali ccm. Ikishindikana kwenye ballot box basi hata kwa mtutu.
Hadithi za kwenye mitandao mtanzania gani aache kutafuta pesa aje kuandamana kwa ajili ya watu wenye makazi nje ya Nchi?
 
Katiba ya nchi hupewi..unaidai...vivaaa CDM kuwaonyesha mwanga watanzania njia ilipo ya kudai Katiba mpya for better Tanzania 🇹🇿
 
Huu ni ujinga tuu , mtu yupo mile 7500 away anawahutubia watu na wao bila kufkri wanapiga makofi , what a nonsense , si arudi tukichafue pamoja , kama anahofia maisha yake vip hawa waliopo wao hawapaswi kuhofia maisha Yao? Hata hvyo ni mda sasa wa kuifanya Tanzania iwe nchi tano
Mkuu unasema muda sasa wa kuifanya Tanzania "IWE NCHI TANO" hapo sijaelewa, UFUNGUKA.
 
CCM haiwezi kuondoka madarakani bila ya watu kuchinjana..that's for sure..yaani ni lazima watu wakichafue mbaya mbovu.

Shida ni kuwa upinzani nao umepoteza dira..upoupo tu,wanadandia hili wanaliacha wanaenda na lingine bila lolote kukamilika.

Mfano,ishu ya wale wabunge 18 inatosha kuonyesha ni kwa kiasi gani wapinzani wanafeli.
Huo utata nani wa kuuleta sasa? Hamna mtanzania timamu kiakili mwenye jeuri hio
 
Tundu Lisu, ninachomsifu ni daima kuwa mkweli wa nafsi yake. Huwezi kumvuta au kumdanganya kiurahisi.

Mama Samia anayoyafanya mpaka sasa ni kupiga plasta nyumba iliyojengwa kwa miti na kukandikwa udongo, na sote tunafurahia kwa sababu tunaona inapendeza, bila ya kujua kuwa cement haishikamani na tope, wakati wowote itabanduka.

Tunataka Mama Samia afanye mambo ya msingi, na siyo kuweka plasta kwenye nyumba dhaifu. Anatakiwa asimamie upatikanaji mpya wa katiba inayojenga Taifa imara. Taifa lisilo na misingi ya haki ni Taifa dhaifu kwa sababu Taifa lisilo na mshikamano wa watu, kamwe haliwezi kuwa Taifa lenye nguvu.

Tunataka KATIBA MPYA inayolinda misingi bora ya utawala wa haki, umoja, demokrasia na usawa.
 
unafikiri siku risasi zikilia ndio zitanyamaza? shukuru Mungu na huo ugali unaokula hapo, kuna wenzio wanaomba amani kila kukicha hawaioni....Ukishaanza kuliza risasi na hiyo CCM ikatoka usifikiri amani itarudi kirahisi tena....tena Tanzania magenge ya kimafia wanaitamani sana siku mpigane ili waigeuze DRC nyingine ya Africa maana kuna kila aina ya resources wanazozitaka....
Watanzania tumejazwa ujinga. Sizungumzii masuala ya vita ila kujidanganya kuwa Tanzania tuna natural resources nyingi sana, wakati hayuiingii hata to 20 ya Dunia.
 
Tanzania hii tukitaka tusonge mbele kiuchumi na kidemokrasia dawa ni kuiondoshea mbali ccm. Ikishindikana kwenye ballot box basi hata kwa mtutu.
Ccm haiwezi kuondoka kwa kusaini petition ya kumtoa Diamond kwenye tuzo za BET
 
..kama ni uongo basi Rais Samia Suluhu atuonyeshe kwa VITENDO.

1. Aivunje tume ya uchaguzi na kuanza mchakato wa kuunda tume mpya na huru.

2. Sheria ya vyama vya siasa iandikwe upya ili itoe haki sawa kwa vyama vyote.

3. Vyama vya siasa viruhusiwe kufanya shughuli zao bila kuingiliwa na kubugudhiwa na dola.

..Rais Samia akirekebisha hayo basi atakuwa amethibitisha kwamba yeye siyo " magufuli wa kike. "
Afanye hayo Ili wanasiasa mpate madaraka siyo 🤣
 
Huyu bwana siku hizi anajiona Yuko juu Sana,amekuwa msemaji na mtoa kauli za ajabu ajabu ,sishangai maana anafaili pale mirembe.

Lakini wafuasi wake wajiulize Mapambano gani huyu lisu anasema ikiwa wakati wa uchaguzi alituahidi kuwa asipokuwa rais nchi hii haitakalika na kinyume chake yeye ndo hakuikalia nchi mpaka leo Yuko kwa mabwana zake ,wafuasi wake mpuuzeni huyu Jonas savimbi.

Hivi huyu aliyesalitiwa na watanzania wa enzi za Magufuli anaamini kabisa watanzania wa Samia watamuunga mkono.?

Kama anataka Mapambano aje kwa motherland apambane nasio kutoa kauli za kijinga akidhani kuwa watanzania ni wapuuzi Kama alivyo yeye.
mpumbavu Nani Kati yake na wewe halafu unamchukulia Jonas savimbi na vitu vya ajabu jamaa alipigana Sana enzi hizo wa kina dos Santos wakawalisha watu propaganda Kali kua jamaa Hana Nia nzuri na taifa,Leo hii angalia Dos Santos yule mpuuzi alivyoigeuza nchi Mali ya familia na kupiga matrilion ya Dola Leo yupo ukimbizini wakati enzi hizo alijiita mkombozi wa wanyonge na mapambio Kama ya Mungu wenu jiwe kujiita mzalendo kumbe lijizi likubwa
Leo hii watu wa Angola ndio wanaamini maneno ya savimbi yalikua ya kweli!
 
Back
Top Bottom