Ye (mama) anafikiri Magu alikuwa mkaksi kwa sababu ya haiba binafsi ya Magufuli, no, nchi hii na watu wake walimlazimisha awe mkaksi. Mtu karithi nchi ambayo watu wake wapo busy kubuni namna gani ya uhakika zaidi ya kuitafuna serikali, wawe wa sekta ya umma au sekta binafsi, wawe wapinzani au wa chama tawala. Mtu kaingia kaipanga upya ( hata kama kwa shida sana na si kwa ukamilifu), afu mtu anakuja kuvuruga na kuua yote yaliyojengwa tena kwa gharama ya uhai wa rais wa nchi. Hapana kwa kweli, na hiyo kitu itamtesa sana mama.
Sisi tupo tu hapa tuna popcorn zetu kucheki hili gemu linakwendaje. Soon or later muda utaamua. Mwisho wa yote mama ana option mbili: aidha akubali kufuata model ya JPM ya Tanzania kwanza Ulimwengu baadaye, au akubali kuwafuata mabeberu na vibaraka wao akina Lissu. Mwisho wa siku haitakuwa rahisi kuvuruga yote aliyoyajenga JPM na 2025 tutarudi hapa kuzungumza mengine.