Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kama Serikali ya CCM inapinga kweli ushoga basi ikafute kipengele cha Katiba kinachoinyima Serikali kuingilia faragha ya mtu

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kama Serikali ya CCM inapinga kweli ushoga basi ikafute kipengele cha Katiba kinachoinyima Serikali kuingilia faragha ya mtu

dikteta2020

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2018
Posts
595
Reaction score
3,991
Tundu Lissu akiwa Arusha leo asubuhi imeibuliwa tena hoja ya ushoga na huu ndiyo msimamo alioutoa

"Wanaleta vihoja kuwa naunga mkono ushoga, katiba ya JMT inasema kila mmoja ana haki ya kulindiwa faragha yake, naunga mkono msimamo huo wa Katiba, siyo kazi ya Serikali kuchungulia kwenye vyumba vya watu, kama kweli wanapiga vita ushoga wafute hayo maneno."

Ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kama wataanza kuingilia mambo ya vyumbani kwa watu itafikia kipindi mtu ataulizwa "Wewe mbona hufanyi sawasawa"

MY TAKE: WANA CCM IFIKIE HATUA MUACHE SIASA ZA KIPUUZI
Rais yeyote anayechaguliwa anaapa kuilinda katiba. Na isitoshe ni lazima uelewe kuwa kila kinachoandikwa kwenye katiba lazima kifuatwe na Rais mteule na ndiyo maana anaapa.

Kwenye katiba nchi yetu haijauzungumzia ushoga kwa kuwa hawana kipimo cha kumjua shoga ili waliweke kuwa ni kosa. Mfano hao kina James hakuna mahali unaweza ku prove kuwa ni shoga. Na hata hukumu yao iliegemea kwenye sheria ya makosa ya mtandao.

Isipokuwa sheria imewekwa kuzuia usambazaji wa video na picha chafu ikiwemo za ngono na hiyo sheria waliipitisha kina Lissu bungeni.

Hilo la ushoga na usagaji linabakia kama maadili ya mtu binafsi na Mungu wake. Sasa huwezi kumtuhumu Lissu kwa mapenzi ya jinsia moja wakati ndoa yake aliyofunga imehusisha jinsia mbili tofauti. Pia ana watoto na hajawahi popote kutamka hata mzaha tu kuhusu ushoga. Na katiba inachotambua ni ndoa kati ya watu wawili wa jinsia tofauti. Hakuna mahali Lissu amesema kuwa atabadili katiba ili mashoga na wasagaji waruhusiwe kuoana!

Nikupe mfano. Hivi Magufuli alipokuwa Dodoma kisha akamjibu yule baba kuwa aliyedai kuwa anamuota akamuuliza "Unaniota tukiwa kitandani au? Angekuwa amesema hivyo Lissu hata kwa mzaha tu nyie muda huu si mngekuwa mnamnyea kabisa! Emb acheni kujadili ujinga.

Au leo Magufuli alipomuomba Sugu amsugue ingekuwa kasema hivyo Lissu si mngepeleka hadi malalamiko NEC? Mbona wao Chadema wala hata hawana ishu na hayo aliyosema Magufuli?

Ifikie mahali nyie CCM muache hizi siasa za kipumbavu!
 
Katiba ni msumari wa 6"

Ukimkuta mtu anaejua kuisoma, kuielewa na kuitafsiri kiukweli mtasumbuana.

Huyu jamaa hata akishinda Urais hii katiba ianze kufundishwa tu shuleni liwe SOMO la lazima kuanzia DRS 3 mpaka PhD level
Inaonekana wengi tunaonekana kama tunajua jua vile kumbe mbulula tu
 
Haya sasa wale wanafiki wa lumumba mmetupiwa konde hilo, nawasubiri mnyanyue midomo yenu kujibu, mtu akishakuzidi akili hapa duniani huwezi kumshinda kwa chochote, huyu Lissu atawatapisha nyongo mpaka mkonde.
 
Na kama kweli tunapiga vita ushoga kama vile ulivyo ujambazi basi tuanze kuwakagua watu kama wana marinda!Kama ambavyo jeshi likipata tetesi za uhalifu au silaha zisizo halali wanakwenda kufanya msako kwenye makazi yanayodhaniwa!Basi mtu akihisiwa tu basi apimwe marinda na akikutwa hana sheria ichukue mkondo wake!
 
Wala siyo Lissu aliyeibua hilo bali ni mwandishi wa habari kamuuliza msimamo wake kuhusu hilo.
Alichojibu ndio msimamo wake Lisu.Mwandishi wa habari kazi yake kamaliza katimiza wajibu wake wa kiuandishi vizuri kabisa kama mwandishi wa habari proffessional kauliza swali professiona na amajibiwa na LIsu msimamo wake kwenye hilo.Muuliza swali wala hana kesi yoyote na hakuna wa kumushambulia kwa nini aliuliza.Ni haki yake kuuliz

Lisu Aliyejibu huyo ndie mumiliki na mwenye hatimiliki ya hilo jibu alilojibu
 
Kwa wajinga tu ndio wanaona kasema point

Ukisoma Katiba kile kipengele cha HAKI YA MTU utaona kana kwamba mtu an uhuru wa kufanya chochote.

Lakini mshike mtu makalio ndio utajua huna haki kikatiba pia.
Kama kufilana ni sehemu ya katiba yetu aseme ila asirushe ngumi
 
Kuna Picha inasambazwa yuko kwenye Gay meeting. Huenda ameamua kutupa hilo jiwe ili wanyamaze

Sent from my TECNO CC7 using JamiiForums mobile app
Dah unaona sasa, hii ya ushoga kwa bongo sio hata Jambo la kuliongea maana hata wanaofanya wakiwa hadharani wanapinga.
 
Ndo sio faragha bali hufanyika hadharani!So kwa hilo halikubaliki,lakini tuwezi kuingia vyumbani kuangalia nani kafanya nini!
ni kuhalallisha uhalifu watoto kibao wanaingiliwa kinyume na maumbile na serikali imeshawafunga miaka kibao wako wabakaji hubaka vyumbani ,maofisini nk Ushoga ni uhalifu wa kisheria Tanzania
Uwe unafanyika vyumbani au popote lazima udhibitiwe ndio maana hoteli nyingi Tanzania hazikubali hata siku moja wanaume wawili kulala chumba kimoja.Double ya wanaume watupu haipo!!
 
Back
Top Bottom