Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kama Serikali ya CCM inapinga kweli ushoga basi ikafute kipengele cha Katiba kinachoinyima Serikali kuingilia faragha ya mtu

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kama Serikali ya CCM inapinga kweli ushoga basi ikafute kipengele cha Katiba kinachoinyima Serikali kuingilia faragha ya mtu

Haya sasa wale wanafiki wa lumumba mmetupiwa konde hilo, nawasubiri mnyanyue midomo yenu kujibu hilo, mtu akishakuzidi akili hapa duniani huwezi kumshinda kwa chochote, huyu Lissu atawatapisha nyongo mpaka mkonde.
Mimi nanyanyua mdomo. Kwahiyo wewe kwa akili yako ndogo, unahisi faragha iliyoongelewa kwenye katiba ni ya wanaume kuingiliana wenyewe kwa wenyewe. Nenda kawaambie wazazi wako nyumbani kwamba, Katiba yetu imeruhusu ushoga kwahiyo namimi nataka kuwa shoga. Nenda kwa kiongozi yoyote wa dini kutokana na imani yako, kamuambie Katiba yetu imeruhusu faragha (ushoga) halafu usikie majibu yao. Nenda kijijini kwenu kwaambie mababu na mabibi zako kwamba katiba yetu imeruhusu ushoga kwahiyo ni jambao jema tu kulifanya. Mkiambiwa Tundu Lissu ni kibaraka wa mabeberu mnakataa, hizi ni sera za kimagharibi siyo utamaduni wetu watanzania. Pumbaf kabisa!!!!
 
Mkuu kama unafanya mahojiano na waandishi/wahariri utawapangia cha kukuuliza?

Lissu hapo anajibu swali aliloulizwa bila kujali ni minor/major issue.

Ndivyo inavyo elekeza hekima ya mahojiano utaulizwa hata usiyopenda kuyajibu na utalazimika kujibu so long umekubali mahojiano.

Ndiyo maana Meko hataki Mdahalo sababu anajua atulizwa yale asiyopenda/asiyoweza kuyajibu.
Bora Meko anayekimbia maswali bongo hii swala la ushoga Ni lakinafiki hasa likitumika ka propaganda na uelewa wa kijamii ulivo.
 
Ngoja ccm watumie hyo propaganda na unajua akili za watanzania zilivo
Yaani mkuu kwamba hiyo ndiyo iwe hoja yao kuu?! Siyo tena mareli, mandege, mabwawa na madaraja?

Ukweli ni kwamba ccm imepoteza ushawishi kwa watu, imekuwa na zaidi ya miaka 59 madarakani na hali ndiyo kama ilivyo huko field.

Kama miaka 59 haikutosha kujenga ushawishi unahisi huu mwezi uliosalia kwa hoja yoyote ile itawabeba?
 
Wao wataibeba juu juu na huku mtaani watu wanaamini tundu lissu anataka kuleta ushoga nchini eti hafai siunajua ccm kwa kubadili Mambo yao.
 
Sijawahi kuona Lissu akikosea.

Lissu spidi uliyonayo ongeza, October tunachukua dora mapema tu.
 
Bora Meko anayekimbia maswali bongo hii swala la ushoga Ni lakinafiki hasa likitumika ka propaganda na uelewa wa kijamii ulivo.
Mkuu watanzania ni zaidi ya unavyo wachukulia. Kama uko 'jikoni' washauri waibebe kama hoja kuu then tuone matokeo.
 
Lakini kwenye Sheria za nchi ushoga unakatazwa kabisa, na hyo haki ya faragha mbona kanitumia sehemu sio sahihi mfano amber rutty Mambo yao yalikuwa binafsi then wakarekodi na kurusha mtandaoni mlitaka aachwe tu.
Sheria na katiba kipi kiko juu?Kwa mujibu wa sheria na katiba,kosa ni kutenda mambo hayo hadharani na ndio maana Lissu anawambia ondoeni kwanza hiyo furaha au katiba itamike moja kwa moja kwa kuwa ushoga[SUP] o[/SUP]
 
Bado darasa linahitajika... Simply kasome Ibara ya 16 ya katiba.
 
Wao wataibeba juu juu na huku mtaani watu wanaamini tundu lissu anataka kuleta ushoga nchini eti hafai siunajua ccm kwa kubadili Mambo yao.
Leo sio mara yake ya kwanza kujibu hivyo, alikuwa na msimamo huo huo alipohojiwa na Steve Sackur kwenye HARDtalk show way back, kwa hiyo ccm wanaijua vizuri.

Kama unahisi ina mtaji kwao kwa nini hawaibebi kama agenda kwenye mikutano yao? Wamesikika wakimuita msaliti, sio mzalendo, anatumika na mabeberu, atagawa madini kwa wazungu nk nk. Why not this one?
 
Lakini kwenye Sheria za nchi ushoga unakatazwa kabisa, na hyo haki ya faragha mbona kanitumia sehemu sio sahihi mfano amber rutty Mambo yao yalikuwa binafsi then wakarekodi na kurusha mtandaoni mlitaka aachwe tu.
Naona Muheshimiwa hajasema ipo wapi so ni kama katatiizo kadogo
 
Sheria na katiba kipi kiko juu?Kwa mujibu wa sheria na katiba,kosa ni kutenda mambo hayo hadharani na ndio maana Lissu anawambia ondoeni kwanza hiyo furaha au katiba itamike moja kwa moja kwa kuwa ushoga[SUP] o[/SUP]
Sheria yeyote inayokinzana na KATIBA ni BATILI
 
Haya sasa wale wanafiki wa lumumba mmetupiwa konde hilo, nawasubiri mnyanyue midomo yenu kujibu, mtu akishakuzidi akili hapa duniani huwezi kumshinda kwa chochote, huyu Lissu atawatapisha nyongo mpaka mkonde.
Lissu ana akili sana. 1 Lissu = 1,000,000,000,000,000 Lumumbas!
 
Maswali mengine kuya skip to maana wabongo twajijua wenyewe
Haina haja ya kuogopa kujibu kama jibu lipo na halimdiscredit. Kama wabongo wataamua watakavyo acha wafanye kwa utashi wao. Tuache unafiki maisha yasonge.
 
Kama kweli mnapiga Vita kwa dhati suala la ushoga kafuteni kile kipengele,siyo blah blah!
Au tuwaulize kivingine mnadai Lissu akiwa Rais kutakuwa na vitendo vya kishoga, Sasa hivi siwanadai Serikali hairusu ushoga je vitendo hivyo vinafanyika au havifanyiki?. Yaliyowapata akina Amba ruti na wenzie ni kuposti . Haya mambo nifaragha kutokana na katiba yetu watu wafanya wapendavyo na watakavyo.
 
Tundu Lissu akiwa Arusha leo asubuhi imeibuliwa tena hoja ya ushoga na huu ndiyo msimamo alioutoa

"Wanaleta vihoja kuwa naunga mkono ushoga, katiba ya JMT inasema kila mmoja ana haki ya kulindiwa faragha yake, naunga mkono msimamo huo wa Katiba, siyo kazi ya Serikali kuchungulia kwenye vyumba vya watu, kama kweli wanapiga vita ushoga wafute hayo maneno."

Ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kama wataanza kuingilia mambo ya vyumbani kwa watu itafikia kipindi mtu ataulizwa "Wewe mbona hufanyi sawasawa"
Pamoja na Ibara ya 16(1) ya Katiba ya JMT (1977) inayohusu Haki ya Faragha, kifungu (2) cha Ibara hiyo kinaweka maelezo zaidi Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa
ibara hii, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama na nafsi yake, mali yake na maskani yake, yaweza kuingiliwa bila ya kuathiri ibara hii.
isitoshe Haki ya faragha na usalama wa mtu imetafsiriwa zaidi na Sheria ya 1984 Na.15 ib.6.

Maswali ya kujiuliza, ambayo Lissu anafunika kujibu, je ni sahihi ndugu (dada/kaka, mama/mtoto, baba/binti, nk) kufanya tendo la ndoa wakiwa ndani kwani ni faragha?

Lissu ni mpuuzi na mshenzi asiyefaa kuwa Rais ya nchi yenye kuheshimu uumbaji wa Mungu. Baada ya kuumba mbingu na nchi na vilivyomo, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba, (Mwanzo 1:27)
 
Na kama kweli tunapiga vita ushoga kama vile ulivyo ujambazi basi tuanze kuwakagua watu kama wana marinda!Kama ambavyo jeshi likipata tetesi za uhalifu au silaha zisizo halali wanakwenda kufanya msako kwenye makazi yanayodhaniwa!Basi mtu akihisiwa tu basi apimwe marinda na akikutwa hana sheria ichukue mkondo wake!
Wazo zuri,aeleze kayashonea wapi na nani kamshonea
 
Back
Top Bottom