Nijuavyo faragha inayozungumziwa ni tendo la ndoa au mapenzi kati ya mwanaume na mwanamke.
Tendo la ndoa likifanyika faragha haina tatizo ndio mahala pake ila likifanyika hadharani ni kosa kijamii nakisheria. Ushoga ukifanyika kwa faragha ni kosa na ukifanyika hadharani ni kosa pia.
Hivyo ushoga hauna habari ya unafanyika kwenye faragha.
Hatuwezi kukaa kimya vijana wetu wakianza vitendo vya ushoga na tukajua tukasema hatuna ushahidi kwasababu wanafanyia faragha hivyo tusiwaonye.
Wanasiasa wanachofanya nikucheza na maneno tu basi ili wasiwaudhi wafadhili wao na wanaobeba ajenda zao.
Ningekua mwanasiasa au mgombea ningeupinga ushoga kwasababu Za kijamii ukiacha mambo ya Sheria n.k. wanasiasa wanaushawishi hivyo wanapaswa kutumia ushawishi wao Kueleza ubaya wa ushoga ili jamii na vijana wasijiingize huko ila unaona wanatafuta mbinu yakutolipinga suala hilo kwa kujificha mara kwenye Sheria mara kwenye haki ili tu kuwafurahisha watoa misaada.
Serikali na wanasiasa upingeni ushoga waziwazi na ielimisheni Jamii iache vitendo hivyo acheni uoga hata Kama waliowatuma nakuwapa fedha niwakali wataelewa watanzani wanamsimamo wao juu ya Hili.
Tunaupinga ushoga kama jamii sheria haziwezi kuzuia ushoga ila Jamii inaweza kuzuia, hawa wanasiasa wanawaza sheria muda wote nakutafuta matobo kwenye Sheria kuhalalisha uovu.
Ushoga haufai kuhalalishwa kwa kucheza na maneno kwa namna yeyote Ile. Siku watoto wa hao wanasiasa watakapotumbukia kwenye ushoga Ndipo watajua hiyo sio faragha ni jambo baya na linafaa kukemewa.
Sent from my Infinix X603 using
JamiiForums mobile app