Tena mkoa wa Mbeya ndio ngome ya CCM .Ukitaka uamini maneno yangu basi jaribu kutathimini ni jimbo gani ndani ya mkoa wa mbeya ukiacha Mbeya mjini limewahi kuongozwa na CHADEMA? Katika mikoa ya nyanda za kusini mkoa wa Mbeya ndio kidogo uliwapa wabunge watatu ambapo ilikuwa jimbo la Mbozi kwa Paschal Yohana Haonga,Jimbo la Momba alikochukua silinde ambaye sasa yupo CCM na Jimbo la Tunduma ambako alikuwa Frenk Mwakajoka. Kwa hiyo ukiangalia kitakwimu na kihistoria unagundua kuwa Mkoa wa Mbeya ndio mkoa ambao wabunge wa CCM hupigiwa Kura kwa wingi sana.
Ukija mkoa wa Rukwa na katavi nako ni ngome ya CCM.ambapo upinzani ulikuwa kidogo sana kwa jimbo la kwela enzi za mfupe alipokuwa anashindana na mzee marehemu Chrisant maji ya Tanga mzindakaya, na alipokuja Daniel Naftal hakuwa tishio hata kidogo na ndio maana aliokuwa nao vijana kama akina James mwanilyela waliokuwa wanakubalika sana hasa kwa kata ya mji mdogo wa Laela wote kwa pamoja na wengine wengi waliikimbia na kuihama CHADEMA.
Kwa hiyo lazima ufahamu kuwa nyanda za juu kusini ni ngome ya CCM na sehemu ambayo kura zake zipo Tayari kwa ajili ya kuipatia na kuipigia CCM kura za ndio kwa kishindo.siasa zetu za nyanda za juu kusini nazifahamu vizuri sana na maeneo yote na kona zote nazifahamu vizuri na utamaduni wake pamoja na mahitaji yake nayafahamu vizuri. Njooni na operation zenu kama sehemu ya kufanya uzurulaji na kutafuna michango ya wafadhili wenu ,lakini hakuna matokeo chanya ya aina yoyote ile mtakayoyapata. Ikumbukwe kuwa nyanda za juu kusini hatuburuzwi wao kudanganywa na hoja nyepesi nyepesi za majukwaani ambazo huwa mnadanganya danganya.