Tetesi: Tundu Lissu kujiunga ACT Wazalendo, Abdul Nondo naye kuula!

Tetesi: Tundu Lissu kujiunga ACT Wazalendo, Abdul Nondo naye kuula!

Status
Not open for further replies.
Nimeona video ya Lissu ya TAREHE 07/09. Ni dhahiri Lissu atafia Chadema. Katoa video akiwa Ubelgiji, full uniform had Bendera, unajua Chadema imentendea mema kiasi gani! Zito naye kaongea kule tweeter kuhusu uhusiano wake na Lissu. Tuache kuvumisha vitu hivi, ili iweje labda unakoelekeza kudadavua. Kama ni kwenda kuona mgonjwa ni kigezo, kuna wale waliomuuguza kwa zaidi ya mwezi tuwaweke wapi
Mkuu bendera na nguo hazimfanyi mtu kufia chamani. Unamkumbuka aliyewahi kuwa Katibu wa Sekretariat ya CCM anayeshughulikia Itikadi na Propaganda ya CCM? Uliamini kwamba atatoka CCM na kufia nje ya CCM?
 
Naona mmeanza uoga..

CCM mpaka sasa wanaogopa sana LISSU kugombea Urais kupitia CDM na akaungwa mkono na ACT chini ya Zito na Maalim Seif.. Tunajua CCM mnaliogopa sana hili kwa sasa na bila shaka mmeshaanza kuwachonganisha kwa hizi taarifa zenu za kimbea..

Makosa mliyoyafanya na lazima muadbibiwe ni pale mlipovuruga watu kuanzia ndani ya chama na nje ya chama, rushwa haiwezi kuwasaidia tena maana kila mnayempa rushwa mshamvuruga, njia mliyobakiza ni moja tu ya ubabe ambayo kuna kiwango ikifika itawafikisha pabaya sana sana..

Mgogoro ulioko ndani ya CCM na watu walivyovimba huku wakicheka na kupiga makofi kinafiki lazima uwamalize ndio maana mnawoga sana kwa LISSU, ZZK, MBOWE, MNYIKA , MAALIM, JUSSA nk kuwa kitu kimoja na safari hii bila shaka upinzani utacheza karata vizuri na karata hii nzuri ndio kaburi la CCM..na msipokuwa makini mtaumiza watu sana kwa kuwatia vilema na kuua sana ili kulazimisha ushindi..

Membe na Nape hawana cha kupoteza nyuma yao zipo harakati za wachekao na kupiga makofi kinafiki ila rohoni na gizani wanawachora tu na hawa ndio wanakwenda kuiangusha CCM mapema tu kama mbwai iwe mbwai tu tukose wote..Fanyeni reconciliatio mapema ndani ya chama chenu ili angalau kiwe na nguvu ya kupambana kwa hoja na hii combination ya LISSU, ZZK, MBOWE,SEIF,JUSA nk haitawaacha salama bara na visiwani..
 
Ndugu zangu,

Bado ni tetesi lakini hapa JF ni muhimu huu mjadala ukawepo kwa afya ya siasa za nchi.Zitto Kabwe ndiye mwanasiasa pekee aliyemtembelea Tundu Lissu mara tano hospitalini,mara tatu Ubelgiji mara mbili Nairobi.Inasemekana ziara za Ubelgiji zaidi zilijawa na mazungumzo kuhusu hatma ya Lissu kisiasa kwa mazungumzo ya wiki mbili zilizopita kuna uwezekano mkubwa Tundu Lissu akajiunga na ACT Wazalendo ili kuendelea na shughuli za siasa.

Bado haijaeleweka kwanini Lissu anafikiri kuondoka Chadema hizi ndio siasa na mauzauza yake,huenda kuna alama za nyakati zimesomwa.

Zaidi ya hilo kijana Abdul Nondo ambaye miezi michache alitumika na Mbowe ili kufifisha nguvu za Zitto Kigoma sasa rasmi ACT Wazalendo ambapo wakati wowote atapewa majukumu ndani ya chama hicho baada ya kumaliza masomo yake UDSM.

Habari nyingi huanza kama tetesi hapa JF mwishowe hubainika kuwa ni za kweli.

[emoji706] Crap
 
Mkuu Kaka Wakudadavua, kwanza naunga mkono hoja, ila duh...!. Kiukweli hii kali!.

Hata hivyo asante Kaka Wakudadavua, kutudadavulia hii, umetupakulia ikiwa ya moto moto, kwa jinsi unavyopata taarifa za ndani za vyama, nakuvulia kofia, Musiba atasubiri!, hongera unafanya kazi nzuri Kaka Wakudadavua. Asante tena. Na kiukweli nakukubali sana...basi tuu, kwa vile wewe ni Kaka, ungekuwa Dada, uvumilivu ungenishinda!.

P
Shikamoo kaka Pascal....
 
Pitia mtori hapa kijichi, umechambua walivyo, japo kuna muda naenda tofauti nawe kimtizamo ila walivowachambua hawa wawili hijabebwa na mihemko yetu ileeee...
Hawezi kuwa mgombea mwenza wake maana wote wanatokea bara. Mgombea mwenza anapaswa kutoka Znz. Vyovyote iwavyo, Zito ndio anafaa zaidi kugombea urais kwani anamudu uchumi, mambo ya kijamii na demokrasia ana siasa za wastani, shida yake haaminiki. Lisu pia anafaa lakini amejikita kwenye sheria zaidi kuliko uchumi na ana siasa za misimamo mikali. Lissu akiwa rais tunaweza kukutana na tatizo lililopo sasa hivi kuwa na rais anayesimamia jambo moja tu na kusahau maeneo mengine.
 
Imeanza lini hiyo sheria?
Lowasa haikumkumba eeeh?
Inaonesha huna kabisa habari ya kinachoendelea kwenye siasa. Zitto na Tundu wanatoka bara MGOMBEA MWENZA LAZIMA ATOKE UPANDE WA PILI WA MUUNGANO na kuna sheria kwamba ukihamia chama kipya kaa miaka miwli ndo ugombee cheo cha kisiasa.
 
Rubbish, waziri mzima unaandika "mavi" kiwango hiki. Acha utoto wewe ni mtu "mkubwa", tunategemea hekima toka kwako siyo utumbo wa hivi!
Unaonekana mgeni siasani, halafu amesema ni tetesi, unless umejisikia tu kumtusi bila kutafakari hoja yake ya kisiasa zaidi.
Asante
 
Wanasiasa Wa afrika kiujumla, hebu tafakari yanayotokea South Africa ni kwasababu ya wanasiasa tu
Mkuu kwenye wanasiasa ongezea "wanasisa wa Tanzania" ndio maana hata wakionewa huwezi kuona wazungu wansema lolote maana wanajua ni "nyani wamezidiana ujanja"
 
Pitia mtori hapa kijichi, umechambua walivyo, japo kuna muda naenda tofauti nawe kimtizamo ila walivowachambua hawa wawili hijabebwa na mihemko yetu ileeee...

Kila siku niko hivyo hivyo bali maoni yangu huwa hayafikii mihemko yako ya kuleeee.
 
Wanasiasa hawaaminiki hata kidogo!
Nimeona video ya Lissu ya TAREHE 07/09. Ni dhahiri Lissu atafia Chadema. Katoa video akiwa Ubelgiji, full uniform had Bendera, unajua Chadema imentendea mema kiasi gani! Zito naye kaongea kule tweeter kuhusu uhusiano wake na Lissu. Tuache kuvumisha vitu hivi, ili iweje labda unakoelekeza kudadavua. Kama ni kwenda kuona mgonjwa ni kigezo, kuna wale waliomuuguza kwa zaidi ya mwezi tuwaweke wapi
 
Ni kweli mkuu,,nishazinyaka kwa mzee mmoja mtata sana,
 
Mwalimu soma tena hayo makosa ya kimaandishi ujirekebishe, huyu alieandika na Nondo mbona kama hawana mfanano?
Kweli utoto ni utoto tu. Wakati ninasomea taaluma ya uwalimu nilisoma sana msamiati wa Adolescent kwenye saikolojia. Lakini nilipokuwa nikisoma sheria nimesoma sana msamiati wa under eighteen au teenage.
Nimehusishanisha na habari hii. Hii habari ameandika Nonde aliyewahi kujiteka na amepost yeye kwa ID yake. Nonde ana IDs nne humu ndani, na hii ni ID yake pia. Thia is unfair propaganda
 
Wanasiasa wanafanya siasa kama ajira na njia ya ulaji, badala ya kufanya siasa za kuwasaidia wananchi.

Kwa sasa hatutakiwi tu-give - a - fuvk kuhusu hizi hamahama za wanasiasa bali tuwasubiri kunako sanduku la kura tuu.


Nadhani sauti iko vizuri.[emoji350][emoji344]


Unforgetable
Kwani ulikuwa unaelewa tofauti
 
Bila mwenyekiti kufanya maamuzi magumu lissu alishakufa siku ile alipomiminiwa risasi. Maamuzi ya mwenyekiti kumpeleka Nairobi ndio yanamfanya lissu kuishi leo.

Hawezi kumsaliti mwenyekiti.

Hii tetesi ni upuuzi kama upuuzi mwingine
1558091972655.jpg
 
Bwana Tambwe Hiza huyu bila shaka?
Apumzike kwa amani.
Mkuu bendera na nguo hazimfanyi mtu kufia chamani. Unamkumbuka aliyewahi kuwa Katibu wa Sekretariat ya CCM anayeshughulikia Itikadi na Propaganda ya CCM? Uliamini kwamba atatoka CCM na kufia nje ya CCM?
 
Hapo penye kuula, inabidi hii mentality ifutiliwe mbali.

Kugeuza nafasi za kuwatumikia wananchi kama nafasi za kujinufaisha ni kosa linalotugharimu.

Flani " Kaula". tuachane na hii kauli.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom