Tundu Lissu kushiriki katika Forum ya International Democratic Union

Tundu Lissu kushiriki katika Forum ya International Democratic Union

Hakuna kitu hapo, hicho kikao unaweza kukuta kinafanyiwa garage
 
Lissu mfa maji, hana jipya, kipindi kile amepigwa risasi na wanausalama wa CHADEMA alitembea dunia mzima akiiambia dunia kuwa aliyempiga yeye risasi ni Mh. JPM je kuna jipya lilitokea? Matokeo yake kapigwa %84 kwa %10+, huu ni upuuzi kuamini kuwa Lissu ni kitisho kwa CCM
 
Just wait and see Joe Biden hzo vurugu atakazofanya-jamaa hana urafiki na watu wanaovunja haki za binadamu.Tarehe 10 December Europe itapitisha sheria yao ya vikwazo inayofanana na ya Marekani na Uingereza inayolenga kupambana na Udiktekta duniani.
Nitafurahi sana kuona hiyo sheria itakayopitishwa kuanzia tarehe 10 December itapigania haki za binadamu na kuondoa utawala wa kidikteta duniani kwa kuruhusu maandamano yanayopinga lockdown UK yaendelee bila kuzuiliwa na police au kukamata waandamaji. Na pia sheria hiyo kuruhusu vyombo vya habari kutangaza na kuonyesha maandamano ya anti-vaccine group badala ya kunyamazia kimya.

Endapo sheria hiyo itaruhusu niliyoyaandika hapo juu basi sitaona tatizo Tanzania kuwekea vikwazo vya kiuchumi, sababu hakuna haki za binadamu nchini 🇹🇿.
 
Ndio mana kakimbia nchi?? sasa lini atarudi mana Ndugai na Mahera ndio kwanza wapo na wapo sana, au unakusudia ataongoza Tz kama Rais lakini akiwa Belgium
Kukimbia sio tatizo,tatizo ni hujuma zenu juu ya maisha yake heko kwake kwa kuwa na bahati ya ulinzi kutoka kwa Mungu aliye juu na akili ya kujiongeza juu ya majambazi ya ccm.
 
Sawa.
Kama Lisu ni genius na wise person kwann hao wabelgiji wasimpe ubunge au uraisi akaongoza wananchi wa Ubelgiji??
Unawalazimisha???? Ubunge sio maisha bali ni sehemu ya uwajibikaji wa kulitumikia taifa na zipo kazi nyingi za kufanya zaidi ya ubunge, upo.
 
Unawalazimisha???? Ubunge sio maisha bali ni sehemu ya uwajibikaji wa kulitumikia taifa na zipo kazi nyingi za kufanya zaidi ya ubunge,upo.
Sijawalazimisha.
Kama ulisoma vizuri post yangu iliyojibu hoja yako, ilikuwa na alama ya kuuliza.
Nitakubaliana na wewe kuwa Lissu ni genius na wise person, endapo ataachana na issue za Tanzania ilihali bado yupo ubelgiji.
Pia nitakubaliana na wewe endapo wabelgiji watampa kazi yoyote ya kupigania haki za binadamu za wabelgiji sababu ana uraia wa huko.
 
Mabalaa gani hayo yaliyoletwa na democrasia.yaan wewe kwako unaona bora kua na kikundi cha watu wanaojimilikisha nchi nakuamua watakavyo badala ya nchi kua niya wananchi wote.

Hata hiyo china uayoifanya role model wako nawao wako kwenye mpito tu,kwasababu china imekua jamhuri mwaka 1912 ni miaka mia moja na kidogo tu iliyopita sidhana kama ikifikisha miaka 150 itakua hivi ilivyo.

Tunachokosea sisi ni kujifanya tuna demokrasia kumbe tunafanya uhuni.Bila demokrasia ya kweli usitegemee maisha yatakua na utulivu daima dumu.Sasa hapo kosa sio demokrasia wala mabeberu bali sisi wenyewe.
Bila Shaka tunaongea lugha tofauti.....nachagua kuheshimu maoni yako.....
 
Mkuu usidharau sana nchi za magharibi,maana Sera zao huwa ni Uhuru na haki za binadamu. Imagine kama mfumo wetu ungekuwa Wa haki na uwazi has a katika kipindi cha uchaguzi,isingepata lawama kutoka pande zozote.

Mfano kungekuwa na tume huru ya uchaguzi,katiba inayompa mamlaka mwananchi Leo hii usingesikia malalamiko. Tungekuwa kama nchi ya Ghana,walikuwa Wa kwanza kupata Uhuru barani Africa,na pia ikawa nchi ya kwanza kufuata democrasia za kimagharibi.leo hii huwezi sikia Ghana kina ghasia ana malalamiko baada ya uchaguzi kila kitu kiko fair.
Demokrasia ni mfumo mzuri wa kutawala kwa sababu unahusisha maamuzi ya watu wengi......lakini pia Inawezekana demokrasia ikatumika kama ajenda kwa MATAIFA yenye nguvu kutekeleza ajenda zao kwenye mataifa yanayoendelea.....!!

Misri walisema hakuna demokrasia wakahamasisha maandamano yaliyoleta anguko la serikali ya Mubarak.......hao hao tena wakasema uuitishwe uchaguzi mkuu......na wananchi wakawachagua MUSLIM BROTHERHOOD kuwaongoza katika sanduku la kura.........Hao hao waliotaka demokrasia wakamtoa RAISI aliyechaguliwa na wananchi kwa KURA nyingi kwa demokrasia walioitaka wenyewe..........

Mimi nahisi kuna ajenda inajaribu kupenyezwa na mataifa ya MAGHARIBI kwa kichaka cha kupigania demokrasia........

Huo ni mtazamo wangu tu.....
 
Habari hii ni kwa mujibu tweet ya International Democratic Union:

We are pleased to confirm Hon. Tundu Lissu’s participation at the #IDUForum2020. Tundu Lissu is Vice-Chairman of @ChademaTz and was Presidential candidate in the recent elections in #Tanzania, which have been an example for an unfree, unjust and unrightful voting process.

Loser!
 
Demokrasia ni mfumo mzuri wa kutawala kwa sababu unahusisha maamuzi ya watu wengi......lakini pia Inawezekana demokrasia ikatumika kama ajenda kwa MATAIFA yenye nguvu kutekeleza ajenda zao kwenye mataifa yanayoendelea.....!!

Misri walisema hakuna demokrasia wakahamasisha maandamano yaliyoleta anguko la serikali ya Mubarak.......hao hao tena wakasema uuitishwe uchaguzi mkuu......na wananchi wakawachagua MUSLIM BROTHERHOOD kuwaongoza katika sanduku la kura.........Hao hao waliotaka demokrasia wakamtoa RAISI aliyechaguliwa na wananchi kwa KURA nyingi kwa demokrasia walioitaka wenyewe..........

Mimi nahisi kuna ajenda inajaribu kupenyezwa na mataifa ya MAGHARIBI kwa kichaka cha kupigania demokrasia........

Huo ni mtazamo wangu tu.....
Mkuu nakuelewa sana.inawezekana uko sawa.
On my side naona kama kwa hapa kwetu demokrasia imebinywa sana, huna pa kukimbilia. Hii yote inatokana na kutokuwa na katiba nzuri inayomlinda mnyonge,na pia hatuna mahakama ya juu(supreme court). Ambayo MTU mwenye shauri lake angekimbilia huko, maana kisheria majaji huko huwa hawateuliwi na Rais wasingeegemea upande wowote.

Kwa sasa hivi kwa kuwa hatuna kilicho huru, tunawategemea mabeberu kwa kuwa wako more advanced kwenye human right.
Na kwa sababu majority ni Donner countries basi ikiwa kuna ubinywaji Wa demokrasia wanaweza haya kiamua kusitisha msaada Fulani mpaka nchi iwatambue wapinzani,au hawatoi msaada Fulani mpakaka katiba itakaporekebishwA nk.
Mabeberu ndo kimbilio letu likibaki pekee.
 
Huyu wa kwetu aalikwe atasema nini? Labda kuwe na mdahalo unaohusu mambo ya kufedhehesha wanawake ndiyo anaweza.
Si tunawangalia na drama zenu tu, oooh atahutubia bunge la Ulaya na Dunia yote itamsikiliza😂.

👉Sasa hivi tena mmekuja na bango lingine, sisi kazi yetu ni kuwaangalia tu maana tunajua fika kuwa kinachowasumbua ni spana mnazoendelea kupigwa, huku wazungu wakiwa hawana muda kabisa na nyinyi zaidi ya matamko tu😂😂.
 
CCM viongozi wao watashiriki lini au wao ni TBC na ITV tu?
Wao wanajenga nchi ya Tanzania tu! Wakati ule mababu zetu wanamajadiliano vijijini mwetu, wazungu hawakualikwa na walikuwa busy wanajenga nchi zao! Sasa ni zamu yetu, tujenge nchi kwa vitendo!
 
Vipi huyu mama amegawa nafasi yake, kwani Tanzania ilikuwa inawakilishwa na yeye
1606762787208.png


Halafu hao jamaa wasiwasumbue akili kwani wao wana mapartner wao hapa nchini; siyo kwamba wako neutral. Wanaimba wimbo wa mapartner wao tu!

1606763380339.png
 
Kwa mara ya kwanza katika historia, Taifa limepata rais ambae hata international community inamuona he's nothing to offer and share na dunia in terms of intellectuality!

Kagame na udikteta wake wote lakini alikuwa anaalikwa huko duniani kwa sababu watu waliamini ana kitu cha ku-share! The so-called Mabeberu walifahamu pamoja na udikteta wa PK lakini ukimweka mbele atetetea anachokiamini, atakitetea in a more intellectual way, kitu ambacho Dikteta Jiwe hawezi!!
Yeye Jiwe hana maneno! Ni vitendo tu. Mpaka kieleweke!
 
Lissu mfa maji,hana jipya, kipindi kile amepigwa risasi na wanausalama wa CHADEMA alitembea dunia muzima akiiambia dunia kuwa aliyempiga yeye risasi ni Mh.JPM je kuna jipya lilitokea? Matokeo yake kapigwa %84 kwa %10+, huu ni upuuzi kuamini kuwa lissu ni kitisho kwa CCM
Hata wana CHADEMA wanalijua hilo,basi tu kwakua wamemua kushupaza mafuvu yao.
 
Back
Top Bottom