Uchaguzi 2020 Tundu Lissu kutinga Chato keshokutwa

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu kutinga Chato keshokutwa

*VIUMBE KARIBA YA MAGUFULI WANAKUJA KWA NADRA SANA, WAKIONDOKA MNASUGUA SANA KUWAPATA TENA.*

Na Bwanku M Bwanku

Mwanamama Mchumi wa Zambia Dambisa Moyo aliyepata kufanya kazi Benki ya Dunia (WB) na kupata tuzo mbalimbali za uandishi wa masuala ya kiuchumi na anayeheshimika kote duniani, ameeleza kwenye kitabu chake alichokiita Dead Aid kwamba matatizo makubwa ya kiuchumi yanayolikumba bara la Afrika ni matokeo ya tatizo la kiuongozi ambao umekuwa ukigharimu bara la Afrika miaka kwa miaka.

Mwanamama Dambisa anasema Afrika licha ya kuathirika na mifumo ya ulimwengu ya kibepari na ubeberu uliojaa unyonyaji ambayo inailazimisha Afrika kukopa sana mikopo ya nje inayowaingiza kwenye mizigo ya madeni (Debt burden) lakini suala la uongozi makini na madhubuti unaopambana na ufisadi, wenye maono ya mbali na wenye misimamo thabiti ni stori isiyoisha kwa Afrika.

Dambisa anasema ili Afrika ijiondoe kwenye minyonyoro hii ipo haja ya Afrika yenyewe kuimarisha mifumo yake ya kiuongozi hasa kuwa na kariba ya viongozi mashujaa, wenye misimamo isiyoyumba na kutetereka, makini, wanaopinga rushwa na watakaotengeneza mifumo ya Afrika kujitegemea hasa kwa kupiga vita ufisadi, rushwa na kuimarisha aina ya uongozi wake utakaowekeza na kuwezesha Afrika kukwepa mnyonyoro wa utegemezi wa mikopo ya nje ambayo kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu imekuwa ikiigharimu Afrika kwa kuiingiza kwenye misaada na mikopo inayoiumiza Afrika aliyoiita 'Dead Aid.'

Mawazo yale aliyoyaota na kuyaeleza Mchumi huyu wa dunia na anayehishimika kote duniani, kwa miaka mitano tu ya uongozi wa Dkt John Pombe Magufuli kuliongoza Taifa la Tanzania inashuhudia mapinduzi makubwa ya kiuongozi na mifumo iliyoshindikana miaka kwa miaka ili kuleta ukombozi wa kiuchumi.

Toka kuingia madarakani kwa Rais Magufuli kumeitoa kimasomaso Afrika na dunia nzima kwa ujumla kwa kushuhudia na kupata mtoto wa kweli wa Afrika aliyekubali kujitoa sadaka na kafara, aliyekubali kufa, aliyekubali kubaki pekee yake na mengine mengi ili kupigania maslahi ya ndugu zake weusi wa Afrika.

Baada ya kuwasoma mashujaa wengi waliolipigania bara la Afrika akina Mwalimu Nyerere, Kwame Nkrumah, Mandela na wengine wengi, Rais Magufuli anaibuka katikati na kuwa moja ya mashujaa wakubwa wa kizazi hiki cha kisasa cha Afrika hasa kwa misimamo yake linapokuja suala la maslahi ya nchi na kupambana na makampuni makubwa na nchi korofi za nje zilizozoea kunyonya mataifa ya Afrika.

Rais aliyejitoa muhanga kupambana na makampuni makubwa na mapapa kwenye sekta ya madini kama Barrick, waliokuwa wanaiba madini pale Buzwagi, Bulyanhulu na North Mara miaka kwa miaka, yeye akasema hapana ni lazima madini yafaidishe Watanzania wa kawaida kwa umiliki na kuruhusu na kutenga maeneo ya wachimbaji wadogo.

Ni rahisi aliyeonyesha misimamo ya kutisha kwenye kupambana na mafisadi, wala rushwa na wahujumu uchumi ambao wana mikono mirefu na mtandao mkubwa, mrefu na mpana sana. Leo husikii tena habari za ufisadi Tanzania. Rais aliyechomoa maelfu kwa maelfu ya watumishi hewa na feki waliokuwa wanaliingiza Taifa kwenye hasara ya mabilioni kwa mabilioni kila sekunde.

Nenda kwenye nidhamu ya watumishi wa umma. Hakuna anayeenda kunywa chai masaa 8 sasahivi. Hakuna lugha za hovyo na kuudhi zilizokuwa zinatoka kwenye vinywa vya manesi, madaktari na watumishi wengi sana kwenye ofisi za umma pindi mama zetu na Watanzania mbalimbali walipoenda kupata huduma. Amenyoosha na kukomesha kila aina ya mifumo mibovu, ya hovyo na iliyokuwa inawaamuza mno wananchi wa kawaida wa chini wasio na sauti. Ni Rais halisi wa wanyonge aliyejitoa kwa maneno na vitendo vyake kulinda maslahi ya watu wa chini. Akina kapuku walionyanyasika sana.

Rais aina ya Magufuli wanakuja mara chache sana kwenye uso wa dunia. Mataifa ya wenzetu watu kama Magufuli huachwa watawale mpaka wachoke na mataifa hayo hukataa kuingia mkenge wa demokrasia laana. Urusi na Vladimir Putin wao wamefanya hivyo, China pia wamempa Xi Jinping kutawala mpaka afe na majirani zetu Rwanda wamefanya hivyo.

Yako mataifa yanamlilia Rais Magufuli, wanatamani angekuwa wa kwao asimamie na kuonyesha njia. Rais mwenye maono, asiyeyumba na aliye tayali kusimama kidete kwa maslahi ya wengi. Fikiria Afrika ingekuwa na Marais kariba ya Magufuli, wenye misimamo, vitendo, maono, wachamungu, wazalendo na wa wote, Afrika ingekuwa wapi? Haya mataifa ya nje na makampuni yao yanayoibagaza Afrika na kulifanya shamba la bibi kwa kuvuna kila wanachokitaka wangepata upenyo huo?

Tumtunze, tumlinde na tuzidi kumpa moyo na kumuombea sana Rais Magufuli, huu ni mpango wa Mungu Tanzania. Mungu ana makusudio na Tanzania. Narudia viongozi aina ya Magufuli wanakuja kwa nadra sana na wakipotea mnaweza kusugua sana kuja kuwapata tena.

0657475347
 
Kiuhalisia JPM ni mwepesi sana.

Ni mtu ambaye ukimprovoke anakurupuka kwenye actions zake.

Lissu ameshajua udhaifu wa jamaa ndo maana anamsumbua nao.
Kazi sio kumsumbua Magufuli hiyo sio kazi ya mgombea uraisi
Kazi kubwa ya mgombea uraisi ni kutafuta na kupata kura toka kwa wapiga kura
Kazi kubwa Lisu aliyonayo ni hiyo naona yeye kajipa kazi isiyomhusu ok atasumbua Magufuli so what ? Wakati mwisho wa siku wapiga kura wanampiga chini october 28

Ila unachokisema kina ukweli kutokana na kampeni anazofanya Lisu si mtu anayetafuta kura ni anamtafuta Magufuli ndio maana anaenda CHato akamsimange kwake ni kama mwanamke mumbeya wa mitaani anayesema mimi nitakuja huko huko kwako nikusimange!! Anafika anasimanga weeeee na kujaza watu mtaani akisimanga.Halafu anaondoka anaenda akijisifu eeh leo nimeenda kwake nimemsimanga hadi basi

Lisu haendi Chato KUTAFUTA KURA ANAENDA KUMSIMANGA Magufuli!!!
Lisu ni mswahili fulani hivi he is not a presidential material.

Chadema mgombea wenu mliyempa ugombea safari hii kazi mnayo.Mnagharimia safari yake ya kwenda kusimanga mtu nyumbani kwake Chato BADALA YA KUTAFUTA KURA.!!!! Poleni

Wastage of Chadema funds
 
Mgombea urais wa CHADEMA, Bw. Tundu Lissu, keshokutwa Jumanne tarehe 13 Oktoba, ataenda kupiga kampeni kwenye ngome ya Rais Magufuli huko Chato.

Pia, kwa mujibu wake yeye mwenyewe, kabla ya kufanya mkutano wake huo, ataenda kuuangalia uwanja wa kimataifa wa ndege unaojengwa mjini humo.

Could be a moment of high drama.
View attachment 1597061
Polisi watamzuia​
 
Wana CHATO hoyee, ,Magufuli hoyee tupate burudani yetu toka kwa Mtoto wetu wa Nyumbani.Tuburudike na ndugu yetu wa CHATO

 
Kabila la hovyo sana nchini
Safari hii mtawakoma wasukuma kwenye sanduku la kura mumewatukana sana na kuponda vitu vyao vilivyo kwao na kuwadharau toka Magufuli ashike watawaonyesha cha mtema kuni sanduku la kura
 
Safari hii mtawakoma wasukuma kwenye sanduku la kura mumewatukana sana na kuponda vitu vyao vilivyo kwao na kuwadharau toka Magufuli ashike watawaonyesha cha mtema kuni sanduku la kura
Hamtutishi washamba wakubwa nyie
 
Tangu lini Mi-CCM ikaratibu ratiba za Lissu?

Lissu atakwenda pote atakapotaka wala si kwa ratiba wala shinikizo zenu.
 
CHADEMA intelegensia hapo ndipo mnapoyumba sioni umuhimu wowote wa kwenda huko Chato.
Wekezeni maeneo ya kimkakati ambayo mnaungwa mkono ambayo uhakika wa kupata kura za kutosha upo.

Wekezeni nguvu Mwanza,Mara,Arusha,Kilimanjaro,Kigoma,Iringa,Mbeya,Songwe,Rukwa,Katavi,Morogoro,Mtwara na Tanga.
Huko kote washamaliza kazi. Kinachofanywa ni kwenda sehemu ambazo bado zimelala kuhakikisha Magufuli hapati hata 5% ya kura, so they say.
 
Huko kote washamaliza kazi. Kinachofanywa ni kwenda sehemu ambazo bado zimelala kuhakikisha Magufuli hapati hata 5% ya kura, so they say.
nikusaidie kidogo chemistry ya uchaguzi, hadi sasa cdm hawana wagombea katika majimbo 114, yaani 50 ya zanzibar na 64 ya bara na katika hayo majimbo yote hajaenda kupiga kampeni huo ushindi anaupataje? Lissu anapita maeneo yenye wapiga kura wengi angalau aambulie viti maalum vichache naona mwaka huu hadi mkewe atakua mbunge,
 
nikusaidie kidogo chemistry ya uchaguzi, hadi sasa cdm hawana wagombea katika majimbo 114, yaani 50 ya zanzibar na 64 ya bara na katika hayo majimbo yote hajaenda kupiga kampeni huo ushindi anaupataje? Lissu anapita maeneo yenye wapiga kura wengi angalau aambulie viti maalum vichache naona mwaka huu hadi mkewe atakua mbunge,
Nyie wengine sijui mkojeee sijui ndo matoto ya nje ya ndoaaa
 
nikusaidie kidogo chemistry ya uchaguzi, hadi sasa cdm hawana wagombea katika majimbo 114, yaani 50 ya zanzibar na 64 ya bara na katika hayo majimbo yote hajaenda kupiga kampeni huo ushindi anaupataje? Lissu anapita maeneo yenye wapiga kura wengi angalau aambulie viti maalum vichache naona mwaka huu hadi mkewe atakua mbunge,
Mgawanyo wa hivyo viti maalum nao unaweza kuleta tafrani kutokana na uchache wa viti watakavyopata.
 
Back
Top Bottom