Tundu Lissu, Lema watangaza mpango wa kurudi Nchini, Lissu ataja kinachomkwamisha

Asante kwa majibu mazuri mh Mjumbe
 

Duu,ila kweli!
 
CCM imetufanya turudi kuishi maisha ya miaka ya 70, mwaka 2022 nakosa umeme kwa masaa 12 kweli? unajua uvumilivu ukizidi sana inakuwa ni ujinga.
Huo siyo "uvumilivu" mkuu FUSO.

Hakuna mwenye uvumilivu wa aina hiyo hapa Tanzania.
Mi nadhani inafaa kutafuta msamiati mwingine katika kulielezea swali hili vyema.
 
Lissu no baba ako?
 
Hao akina Lissu warudi haraka labda kero ya umeme na maji itaisha!! Wamekwamisha vitu vingi sana!
 
Wanabodi nimefuatilia mijadala miwili kati ya Mwenyekiti wa Chadema na Makamu Mwenyekiti kwanza nimegundua watu hawa mawazo yao ni ardhi na mbingu.

Wakati Mbowe akiongelea suala la subra ya maridhiano, Lissu yeye anasema lazima wafanye iwe isiwe kinachomkwamisha ni nauli ya kurudi Bongo.

Kama Lissu hana nauli ya Kurudi Tanzania hela ya kufanya mikutano ataitoa wapi.? Hapa naiona Busara na hekima za Mbowe wanavuta muda wapate kianzi ila Lissu anataka kuwaumbua kwa kutembeza bakuli harakati na njaa haziendi kabisa.

Naomba nimkumbushe Lissu ndege yetu Karibuni kurudi toka Uholanzi tumuombe lifti humo.

Ili Lissu apate Pesa lazima afanye harakati kuchafuke hiki ndiyo kinachomuumiza zaidi si mfanyabiashara kama Mbowe yeye anaishi kwa mifuko ya wahisani.

Hapa unagundua CHADEMA wapo kwa ajili ya matumbo yao zaidi.
 
Hivyo ni visingizio tu mkuu, anavuta muda uchaguzi ukaribie.
Siwezi kumlaumu, katika wanasiasa wakioubeba msalaba wa upinzani awamu iliyopita ni yeye, acha apumzike.
 
Kumuacha mme yataka moyo mpaka leo hawajarudi
 
Njooni mfe, nusu ya viongozi waliofurahia wakati mnaumia bado wapo serikalini.
 
CCM imetufanya turudi kuishi maisha ya miaka ya 70, mwaka 2022 nakosa umeme kwa masaa 12 kweli? unajua uvumilivu ukizidi sana inakuwa ni ujinga.

Najaribu kutafakari tutavumilia haya mpaka lini? Mwisho wa haya ni nini?
 
Karibuni sana ila msije kuharibu kazi ya Heche na makamanda waliokuwa wamebaki nyumbani...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…